Je Rais wa Sri lanka Gotabaya Rajapakse atajiuzulu?

Ofisi ya Waziri mkuu nchini Sri Lanka imesema leo kwamba Rais Gotabhaya Rajapaksa amethibitisha kwamba atajiuzuru kama ilivyotangazwa awali.

 Kikatiba, kama rais akijiuzuru, Spika atafahamishwa kwa maandishi.

Spika Mahinda Yapa Abeywardena alitangaza usiku wa tarehe 9 Julai kwamba Rais Gotabhaya Rajapaksa ametangaza kuwa atajiuzuru tarehe 13 Julai.

 Hii ilikuja baada ya viongozi wa vyama vya kisiasa bungeni baada ya wanamgambo kuteka kasri ya rais na ofisi ya rais.

Lakini je Rais ataondoka mamlakani kweli tarehe 13 Julai ? baadhi ya vyama vimeonyesha kuwa na wasi wasi juu ya hilo.

Wakili maarufu nchini Sri Lanka Nagahananda Kodituvakku alitoa kwenye vyombo vya habari tangazo na kusema, "Tulimg’oa mamlakani Gotabhaya Rajapaksa kupitia njia isiyo ya ghasia . Lakini hakwenda. Yapa Abeywardena alitoa wito na kusema anakujia na aliniambia hili kwa njia ya simu . Hakuna taarifa iliyowasilishwa kwako. Hapana, ni uongo, ni ufisadi .""Uwe mwenye akili juu ya kile unachotaka kukifanya ."Alisema.

 "Watu wanahangaika, huku watu waliomo katika ofisi yar ais na katika kasi yake wanafurahia sana maisha yao. Wanacheza katika eno la mazoezi ya mwili pale, Wanacheza katika kidimbwi cha kuogelea.

 Wana wakati mzuri sana. Lakini naweza kukwambia kuwa nis awa na kuona bahari kabla ya kukumbwa na tsunami. Huwezi kuiona tsunami ikija kutoka umbali wa mita 30 kutoka juu. Hii ni sawa kabisa na kinachoendelea." Alionya

Tangazo la Rais

Eneo halisi alikojificha Bado halijafichuliwa baada ya wanamgambo kuvamia kasri ya rais

Na ofisi yar ais tarehe 9 Julai. Jana tarehe 10, rais ambaye hajatoa kauli yoyote kuhsu kuchukuliwa kwa ofisi ya Rais na Kasri yake, alituma ujumbe kwenye mtandao wa Facebook kuhusu kuwasili kwa meli ya gesi nchini Sri Lanka.

Ulisema, " Meli ya kwanza iliyobeba tani 3,700 za gesi imewasili kwenye fukwe za nchi, na hivyo kumaliza mzozo wa gesi ."

Pia ulisema kwamba meli ya pili iliyobeba tani 3,740 za gesi itawasili leo tarehe 11.

 Akizungumzia kuhusu swala hili, Nagahanda Kodituvakku alihoji, "Je mtu aliyeondoka mamlaka hufanya kazi hivi? Je mtu aliyefukuzwa na watu anafanya hivi? Huu ni uongo. Alishutumu.

 Wakati huo huo, Wizara ya ulinzi, ilisisitiza kuwa taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya habari ya kijamii kwamba idadi kubwa ya wanajeshi wanakwenda katika ameneo yenye upinzani dhidi yar ais ni za uongo.

 Msemaji wa jeshi alitangaza kuwa Jenerali Shavendra Silva, ambaye ni mkuu wa baraza la ulinzi, alikanusha vikali taarifa hizo.

Rais yuko wapi?

Dkt Omalpe Sobitha Thero, Mkuu wa jimbo Sri Lanka Kusini, aliuliza ni wapi alipo Rais Rajapaska.

"Ni tatizo kubwa iwapo rais hataonekana kwa siku chache zijazo. Je Bw. Gotabha Rajapakse anajiandaa kujiuzulu?" Aliuliza.

Watu wengi wamekuwa wakiuliza maswali kuhusu ni wapi aliko, hususan Waziri wa ulinzi, wapi aliko Rais? Bw . Gotabaya Rajapaksa yuko wapi?"

Nini kinafanyika?

Elewa matarajio ya watu

Chama cha wanasheria wa Sri Lanka liliziomba pande zote zinazohasimiana kuelewa matarajio ya watu wan chi hiyo.

Chama hicho kilisisitiza kwamba kama hili halitafanyika, nchi itatumbukia kwenye mzozo mbaya zaidi.

 Rais wa chama cha mawakili wa Sri Lanka Bar Mwanasheria Sally Peiris alisisitiza kwamba "kwa ajili ya uthabiti wa kijamii wan chi hii, uchaguzi wa mrithi war ais hauwezi kucheleweshwa. Tunamba Rais wa sasa, Waziri mkuu, pamoja na spik ana wabunge kukamilisha mchakati wa kumchagua mrithi wa rais bila kuchelewa ." Waliomba.

"Elewa kile ambacho watu wa nchi hii wanakitaka. Tunaziomba pande zote husika kuelewa matarajio ya watu wa nchi hii ." Alisema.

Nini kinatokea baada ya kujiuzuru kwa rais?

Iwapo Rais atajiuzuru, barua ya kujiuzuru lazima iwasilishwe kwa Spika. Halafu kazi ya urais inakuwa wazi.

Kulingana na katiba, wakati ofisi ya rais inapokuwa wazi , Waziri mkuu huwa Kaimu Rais. Kama Waziri Mkuu hawezi kufanya hivyo, Spika anaweza kuwa Kaimu Rais.

 Itawezekana kisheria kwa Wabunge kuweza kumxteua rais katika kipindi cha siku 30 cha uteuzi wake na kwa kawaida huwa anachaguliwa kwa kura ya siri bungeni.

Kushinda kura hiyo, atatakiwa kupata zaidi ya 50% ya kura. Ili kuchaguliw akuwa rais, mgombea lazima apate kura 113 kati ya wabunge 225 wa bunge la Sri Lanka.