Je, kunusa jasho la watu wengine kunaweza kudhibiti wasiwasi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Utafiti uliofanywa na watafiti nchini Uswidi kwa usaidizi wa watu waliojitolea unaonyesha kuwa kunusa harufu za mwili wa watu wengine kunaweza kusaidia katika kutibu wasiwasi wa kijamii.
Watafiti walitumia jasho la kwapa katika majaribio ya utafiti huo.
Utafiti unapendekeza kunusa harufu ya wengine huwezesha njia za ubongo zinazohusiana na hisia, ambazo zinaweza kuwa na athari ya kutuliza.
Hata hivyo, bado ni mapema sana kudhibitisha nadharia hii.
Timu ya watafiti inayofanya kazi katika utafiti huu itawasilisha baadhi ya matokeo yake katika mkutano wa matibabu katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, wiki hii.
Kwa nini na jinsi gani tunaweza kuvuta harufu ya miili ya watu wengine?
Watoto huzaliwa wakiwa na hisia kali za kunusa na hupendelea kunusa harufu ya mama yao na harufu ya maziwa ya mama.
Hisia ya harufu hutusaidia kuhisi hatari katika chakula na moshi wa moto, kwa mfano, pamoja na kuingiliana na mazingira yetu na kila mmoja.
Harufu pia hufanya milo iwe ya kupendeza zaidi na husaidia kurejesha kumbukumbu.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Harufu hubainika na vipokezi katika sehemu ya juu ya pua ambayo hupeleka ishara kwa mfumo wa ubongo, sehemu inayohusika na kumbukumbu na hisia.
Watafiti wa Sweden wanaonyesha kwamba harufu ya mwili wa binadamu inaweza kufichua hali ya kihisia ya mtu wakati yeye ana furaha au wasiwasi, kwa mfano - inaweza hata kumfanya kuwa na athari sawa na hali hiyo ya kihisia kwa wengine ambao havuta harufu hiyo.
Watafiti waliwataka watu waliojitolea kutoa jasho la kwapa, ambalo lilitolewa na mwili wakati wa kutazama sinema ya kutisha au sinema ya kuchekesha.
Wanawake 48 walio na wasiwasi wa kijamii walikubali kunusa sampuli hizi wakati wakipokea matibabu ya kitamaduni kwa tatizo linaloitwa "mindfulness and meditation" yaani "kuzingatia na kutafakari," ambayo inahusisha kuwahimiza wagonjwa kuzingatia wakati uliopo na kuangazia zaidi ya mawazo hasi.
Baadhi ya wanawake hao walipewa harufu ya jasho huku mwingine wakinusa hewa ya wazi.
Matokeo yake yalikuwa maendeleo zaidi katika matibabu ya kisaikolojia ya jadi kwa wale waliosikia harufu ya jasho.
Kiongozi wa timu ya watafiti inayoandaa utafiti huu, Elisa Vigna, katika Taasisi ya Karolinska huko Stockholm, alisema,
"Jasho linalotolewa na mwili wa mtu mwenye furaha lilikuwa na athari sawa na jasho linalotolewa na mtu aliyeogopa kutoka kwenye eneo la tukio yaani filamu ya kutisha. Inaweza kuwa inahusiana na ishara za kemikali za binadamu za jasho kwa ujumla." ambayo inaweza kuwajibika matibabu yenye tija.
Aliongeza: "Inaweza kuwa uwepo wa mtu mwingine katika sehemu moja ambayo ina athari sawa, lakini tunahitaji kuhakikisha kuwa, na hii ndio tunayojaribu kwa sasa katika mpango kazi wa ufuatiliaji. lakini tuko wapi kutokana na jasho ambalo hutolewa na wale wanaotazama sinema kutokuwa msisimko."
Je, jasho ni nini, na huwa na harufu kila wakati?
Jasho mara nyingi halina harufu, lakini tezi za jasho kwenye kwapa na eneo la kinena mara nyingi hutoa misombo ambayo hutoa harufu ya mwili.
Bakteria juu ya ngozi karibu na kituta cha kuotea nywele huingiliana na misombo hii ya kibiolojia na harufu ya mwili hutolewa.
"Tunajua kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya hisia ya kunusa na afya ya kihisia," alisema Duncan Bock, wa shirika la hisani la Fifth Sense, ambalo huongeza ufahamu wa matatizo ya harufu na ladha.
"Kupoteza uwezo wa kunusa watu, kama vile mwenza au watoto, kunaweza kusababisha mfadhaiko au hisia ya kutengwa," aliongeza.
Aliendelea: "Wakati utafiti huu ni wa awali, bila shaka bado kuna haja ya kuufanyia kazi zaidi. Inatia moyo sana kuona utafiti zaidi juu ya umuhimu wa hisi ya kunusa kwa afya bora ya akili."














