Je, kompyuta ya ajabu inayotabiri timu itakayoshinda taji la Uingereza inafanyaje kazi?

Ni jambo ambalo wachambuzi wa masuala ya michezo wameanza kulifikiria, kwa sababu timu ya Arsenal imeshinda kwa mara ya nane mfululizo, na siku ya Jumamosi walichukua nafasi ya kwanza katika ligi ya Uingereza. Kila mwaka, inapofika mwisho wa ligi, utabiri hufanywa na kompyuta ambayo hutumiwa kutabiri michezo.

Liverpool waliokuwa wanaongoza, walitoka sare na Manchester United siku chache zilizopita, na hivyo kushika nafasi ya pili, huku Manchester City, wanaotetea ubingwa, wakiwa katika nafasi ya tatu.

Inazidi kuwa vigumu kutabiri nani atashinda ligi ikiwa imesalia mechi saba.

Kwa hiyo kompyuta inayotabiri timu itakayotwaa kombe inaashiria timu ambayo inadhani itatwaa kombe hilo, na swali ni jinsi inavyokadiria mshindi.

Kompyuta hii bora mara 100,000 huunda upya mechi za timu zote, kwa kutumia vigezo vya data kutabiri vyema matokeo ya msimu uliosalia.

Huhesabu uwezekano wa timu kumaliza katika nafasi zao ama chini au juu.

Pia huhesabu watakaoshinda, watakaoshindwa na watakaotoka sare, kwa kuzingatia matokeo ya zamani.

Kwa hivyo ilipotokea, kompyuta ilitabiri kuwa timu tatu za juu kwenye ligi zitakuwa mbele kwa alama mbili, na ligi itachukuliwa kwa tofauti ya mabao.

Kulingana na kompyuta, Arsenal itashinda Ligi ya Primia baada ya miaka 20. Pia ilitabiri kuwa timu ya Liverpool itakuwa sawa kwa pointi na Arsenal, lakini tofauti ya mabao itakuwa 10.

Vile vile, ilitabiri kuwa Manchester City inatarajiwa kuwa nyuma kwa pointi mbili.

Utabiri alioutoa kwa timu hizo ni kwamba Manchester City ina nafasi ya 17.3 kutwaa taji hilo kwa mara ya nne mfululizo, huku Liverpool ikiwa na nafasi 30.3 kutwaa kombe hilo, na Arsenal ina nafasi ya 52.3.

“Matokeo siku zote yanategemea timu ina nini, lakini kwa kuwa kompyuta hii imetumika kwa muda mrefu, ni nzuri kwa utabiri wa muda mfupi,” alisema Mohamed Ahmed Deysane, ambaye anatoa maoni yake kuhusu mchezo huo.

"Watu wanavutiwa sana na utabiri wa hii kompyuta, kwa sababu inazingatia – mambo kama wachambuzi - wachezaji waliojeruhiwa, wanaoanza mchezo uwanjani, nafasi na uwanja wa kucheza," Deysane aliongeza.

Timu tatu zitakazosalia kwenye Ligi ya Primia, alisema kulingana na kompyuta hii, zitakuwa Luton, Burnley na Sheffield United.

Imefasiriwa na Asha Juma