Kwanini Jamii hizi bado zinathamini ubikira wa mabinti zao?

Chanzo cha picha, Prashanti Aswani
Fahari ya kuwa bikra kimekuwa kitovu cha uchunguzi na wasiwasi kwa karne nyingi.
Je, tunawezaje kukomesha dhana zinazozunguka suala hili?
Je, mimi ni bikira? aliuliza mtu mmoja kwenye mtandao.
Sarras hakuwa na uhakika wa vile anavyostahili kujibu.
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kutumiwa kile anachoeleza kuwa "picha ya uke".
Wakati huo, Sarras alikuwa msimamizi kwenye ukurasa wa Facebook wa Love Matters Arabic, ambao unatoa elimu ya mahusiano na ngono kwa Kiarabu kwenye mitandao ya kijamii.
"Alisema alikuwa na uhusiano na sasa alikuwa akichumbiwa na alitaka kuhakikisha kuwa yeye ni bikira, "Sarras aeleza.
"Nachukia neno hili: maftuuha"
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Yule mtu wa kwenye mtandao alikuwa anauliza kama Sarras angeweza kuona kizinda chake, kwa maneno mengine kuhakikisha kama yeye ni bikra - kwa sababu ya shinikizo katika jamii yake kuwa bikira kwenye ndoa, na kwa mumewe kushuhudia wazi katika mfumo wa damu ndicho kinachohitaji.
Imani hii kwamba kuhakikisha kuwa ni bikira lazima ushahidi wa wazi kuonekana ni historia ya ngono na msingi wa kupima ubikira, tabia iliyolaaniwa na Shirika la Afya Ulimwenguni mwaka wa 2018 kama ukiukaji wa haki za binadamu.
Vipimo hivyo vinaweza kuchukua aina tofauti.
Kila kitu kuanzia uchunguzi wa kimwili wa kupima ubikira au ulegevu wa uke hadi tambiko za usiku wa harusi ambapo shuka iliyo na damu inatarajiwa kuonekana, na hata kuonyeshwa kwa familia za bibi na bwana harusi.
Licha ya hayo kutokuwa na msingi wa kisayansi - na licha ya ubikira wenyewe kuwa ni muundo wa kijamii usio na ukweli wa kibaolojia - mamilioni duniani kote wanaendelea kuamini kwamba historia ya ngono ya mwanamke imeandikwa kwa namna fulani na kwamba wanawake wote wanatokwa na damu mara ya kwanza kufanya ngono.
Wala, bila shaka, si kweli - lakini imani kama hizo zinaweza kupatikana katika lugha, dini na jamii kote ulimwenguni.
Nilipata tafiti nyingi za kisayansi zinazoondoa dhana hii.
Lakini pia niligundua ulimwengu ambapo baadhi ya madaktari huidhinisha wazo hilo, mashirika mengi ya kutunga sheria huiunga mkono, na ambapo mara nyingi kuna kutozingatiwa kabisa kwa habari sahihi kuhusu kizinda au utango wa mwenye uke katika elimu ya ngono duniani kote.

Chanzo cha picha, Prashanti Aswani
Kizinda ni tishu ndogo ya utando ambayo inaweza kupatikana karibu na ufunguzi wa uke.
Ni ajabu kabisa kwamba kipande kidogo cha tishu kinachoonekana kutokuwa na kusudi kimehusishwa na kusudi lisilo sahihi sana.
Kuna mjadala kati ya jumuiya ya wanasayansi unaohusu kwanza kwa nini kizinda au utando huo upo?
Je, ni mabaki kutoka kwa aina zetu za mamalia wa kabla ya historia zilipoteleza nje ya maji na kuingia nchi kavu?
Je, iko hapo kusaidia bakteria wa kinyesi wasiteleze kwenye uke wakiwa wachanga?
Hakuna anayejua ukweli.
Tishu inaonekana kuwa na madhumuni zaidi katika baadhi ya spishi zingine – kizinda au utando wa sehemu ya uke wa nguruwe wa Guinea huyeyuka kinapoingia kwenye joto na kisha kukua tena kinapokamilika, kwa mfano.
Lakini utando wa mwanamke ni tofauti.
Kwa sisi walio na uke, utando wa sehemu hiyo unaweza kutofautiana sana.
Watu wengi wanaamini kimakosa kwamba kizinda au utando huziba juu ya uke, bila kutambua kwamba hiyo ingemaanisha kuwa mwanamke hataweza kupata hedhi (watu wachache wana hali hii).
Badala yake, utando mwingi una umbo la mwezi au mwezi mpevu, na vinaweza kuchukua aina nyingi za ukonde na unene tofauti.
Wachache wetu tuliambiwa kwamba inaweza kubadilika kulingana na umri, kwamba baadhi yetu hatujazaliwa nayo, au kwamba inaweza kutoweka kabisa tunapoingia ukomavu wa kijinsia.
Au kwamba aina mbalimbali za shughuli zinaweza kunyoosha au kubomoa, kuanzia kwa mazoezi, kupiga punyeto hadi kufanya tendo la ngono.
Lakini hii haimaanishi kuwa kuna uhalali wowote kwa wazo kwamba unaweza kuhakikisha shughuli za ngono zilifanyika kwa kuchunguzi utando wa ukeni.
Utafiti mmoja mdogo wa vijana 36 wajawazito uliochapishwa mwaka wa 2004, kwa mfano, uligundua kuwa wafanyakazi wa matibabu waliweza tu kufanya ‘’matokeo ya uhakika ya kushiriki ngono’’ katika matukio mawili.
Utafiti mwingine wa 2004 uligundua kuwa 52% ya wasichana waliobalehe walioshiriki ngono waliohojiwa hawakuwa na ‘’mabadiliko yoyote yanayotambulika kwenye tishu za kizinda au utando wa kwenye uke’’.
Damu kwenye shuka kama aina ya kipimo cha ubikira kinachotumiwa kote ulimwenguni, pia inatokana na dhana ya uwongo.
Baadhi ya kizinda au utando huweza kuvuja damu zinaponyooshwa kwa mara ya kwanza ikiwa kitendo ni cha ghafla au kama hujatulia, lakini damu yoyote kwa kweli ina uwezekano mkubwa wa kutoka kwa michubuko kwenye ukuta wa uke kwa sababu ya kujamiiana kwa nguvu au ukosefu wakilainishi.
Kutokwa na damu kutokana na ngono ya mara ya kwanza kunaweza kutokea au kusitokee, kama vile kutokwa na damu kutoka kwa ngono wakati wowote kunaweza kutokea au kutotokea.
Sababu za kutokwa na damu wakati wa kujamiiana ni pamoja na kuhisi wasiwasi, kutosisimka kabisa au kupata uchungu kutokana na mambo kama vile maambukizi.
Daktari mmoja wa uzazi alipowachunguza wenzake 41, akiwauliza ikiwa walivuja damu mara ya kwanza walipofanya ngono au la, asilimia 63 kati yao walisema hawakuwa na damu.

Chanzo cha picha, Prashanti Aswani
Lakini katika nchi ambazo zinaendelea kushinikiza ubikira, kuna nafasi ndogo mtazamo huu wa kibaolojia.
Utafiti wa mwaka 2011 katika Chuo Kikuu cha Dicle nchini Uturuki uligundua kuwa 72.1% ya wanafunzi wa kike na 74.2% ya wanaume waliamini kuwa kizinda au utando kinaashiria ubikira.
Asilimia 30.1 ya wanaume walisema kwamba ‘’shuka iliyochafuliwa na damu’’ inapaswa kuonyeshwa kwa familia siku ya ndoa.
Hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa uwezo wa wanawake kufikia afya chanya ya ngono, kuwazuia kuchunguza utambulisho wao wa kijinsia na kusababisha wasiwasi kuhusu ngono.
Utafiti wa kijamii huko Giza, Misri, uligundua kuwa wanawake wengi waliohojiwa walipata wasiwasi na hofu kabla ya usiku wa harusi yao, na maumivu na hofu wakati na baada ya, kwa sababu ya mawazo kuhusu ubikira na kizinda.
Katika uchunguzi wa Lebanon wa wanafunzi wa chuo kikuu kutoka 2013, karibu 43% ya wanawake waliohojiwa walisema hawatafanya ngono kabla ya ndoa kwa hofu ya kutovuja damu usiku wa harusi yao.
Utafiti mwingine kutoka Lebanon, huu wa 2017, uligundua kuwa kati ya wanawake 416 waliohojiwa, karibu 40% yao waliripoti kufanya ngono ya sehemu ya haja kubwa au ya mdomo ili kulinda utando kwa ajili ya ndoa.
Katika utafiti wangu, niligundua machapisho mengi ya mtandaoni ya wanawake walioogopa kwamba kupiga punyeto kumewafanya wapoteze utando wao, au waliogopa sana kujigusa hivi kwamba hawakuwahi kufanya hivyo.
Simulizi ya kizinda au utando haiathiri tu ustawi wa kijinsia wa wanawake na kwa kweli usawa - inaweza kuzuia ufikiaji wao wa haki.
Pakistan imepiga marufuku hivi majuzi tu vipimo vya ubikira kwa walionusurika ubakaji katika kesi mahakamani.
Nchi kadhaa, hasa katika Asia, Mashariki ya Kati na kaskazini na kusini mwa Afrika, bado hufanya tamaduni hii.
Na madaktari wengi duniani kote hutoa faida kubwa ya kutengeneza kizinda kama upasuaji kwa wanawake ambao wamefanya ngono kabla ya ndoa na wanahofia madhara yakigunduliwa.
Kama sheria ambayo itapiga marufuku ukarabati wa kizinda au utando wa uke nchini Uingereza ikifanya kazi katika Bunge, ni wazi baadhi ya madaktari wa upasuaji wanashikilia hadi mwisho kabisa, wanaendelea kutoa huduma hii katika ardhi ya Uingereza.
Daktari mmoja wa upasuaji wa London anaendelea kudai ukarabati wa kizinda unaweza kuwa ‘’wa manufaa kwa wanawake ambao wanaweza kuwa wamepata uharibifu wa uke kwa sababu ya kujamiiana au shughuli nyingi za kimwili’’.
Kwa hivyo unamalizaje dhan ya utando wa uke?
Kuangazia baadhi ya utafiti huu itakuwa mwanzo, kama vile kubadilisha mazoea ya kisheria ambayo yanaidhinisha vipimo vya ubikira na kuzuia wataalamu wa afya kutokana na kupotosha watu.
Suala ni kwamba mengi ya mawazo haya si tu kwamba yameingizwa katika vizazi; yanaungwa mkono na mawazo ambayo si lazima yahitaji au kukiri kile ambacho sayansi inasema.
Ikiwa unaamini katika wazo la kitamaduni la ubikira, na kuunga mkono kukosekana kwa usawa wa kijinsia nyuma yake, mabadiliko ya kijamii yanaweza kutokea ili kukufanya ufikiri vinginevyo.
Wengine wanaamini kwamba njia moja ya kumaliza dhana hiyo mara moja na kwa wote ni kubadili jina ya sehemu hiyo ya uke kabisa.















