Tetesi za soka Ulaya Jumapili: Liverpool, Arsenal na ManCity mbioni kumsajili Anthony Gordon

Muda wa kusoma: Dakika 2

Liverpool ndio walio mstari wa mbele katika mbio na Manchester City na Arsenal kumsajili winga wa zamani wa Newcastle United Everton Anthony Gordon, 24, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza atagharimu pauni milioni 95. (Caughtoffside)

Hatua hiyo imekuja huku Mohamed Salah, 33, akionekana kujiandaa kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu, huku Ligi ya Saudia ikipanga kusonga mbele na mipango ya kumnasa mshambuliaji huyo wa Misri. (TeamTalk)

Liverpool pia wako kwenye vita vingine, wakati huu na Manchester United, kuhusu mshambuliaji wa Wolves, Mateus Mane, 18, msimu huu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye asili ya Ureno ana thamani ya £50m na ​​klabu yake. (Fichajes),

Tottenham ilikataa maombi kutoka kwa Aston Villa na Chelsea mwezi uliopita kuhusu kiungo wao wa kati wa Uswidi Lucas Bergvall, 20. (Athletic - Subscription Required)

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amedhamiria kumsajili beki wa kati wa Ufaransa Castello Lukeba, 23, kutoka RB Leipzig, huku klabu hiyo ya Ujerumani ikiwa tayari kumuuza kwa £52.1m. (Sports Boom via Teamtalk)

Arsenal pia inamtafuta winga wa RB Leipzig mwenye umri wa miaka 20 kutoka Norway Antonio Nusa, ambaye thamani yake ni kati ya euro 50-60m (£43m-£52m). (Fussball Daten - In Germany}

Aston Villa wamempanga mlinda lango wa Manchester City James Trafford, 23, kama mbadala wa Emiliano Martinez iwapo mchezaji huyo nambari moja wa Argentina mwenye umri wa miaka 33 ataondoka msimu huu. (Football Insider}

Maskauti wa Manchester United walikuwa San Siro Jumamosi kumtazama beki wa kushoto wa Inter Milan, 28, Federico Dimarco na mlinzi wa kati wa Ufaransa Pierre Kalulu, 25, wa Juventus. (Calciomercato - In Itali)

"Ndoto moja" ya kiungo wa Liverpool Dominik Szoboszlai, 25, ni kuichezea Real Madrid, asema kocha wa timu ya taifa ya nahodha wa Hungary Marco Rossi. (Marca - In Spanish)

Enzo Maresca anasalia kuwa mgombea anayeongoza kuchukua nafasi ya Pep Guardiola atakapoondoka Manchester City na hajafanya mazungumzo na Tottenham kuhusu kibarua cha meneja wao wa kudumu baada ya Thomas Frank kuondoka. (Fabrizio Romano)