Yanayojiri ndani ya kambi ya wafungwa wa vita wa Kirusi nchini Ukraine

Russian prisoners of war at a facility in western Ukraine
Maelezo ya picha, Mamia ya wanajeshi wa Urusi waliokamatwa, askari na mamluki wanazuiliwa katika vituo nchini Ukraine
    • Author, James Waterhouse
    • Nafasi, BBC Ukraine correspondent

Makombora ya Kirusi kwa mara nyingine yalikuwa yakiichokoza Ukraine kutoka angani tulipokuwa tukiingia kwenye kituo hiki cha wafungwa wa vita magharibi mwa nchi.

Mamia ya wanajeshi wa Urusi waliokamatwa, askari na mamluki wanazuiliwa katika majengo haya machafu moja ya maeneo 50 karibu na Ukraine.

Sauti za makombora ya kikosi cha anga cha Ukraine zilisikika kwa mbali tulipokuwa tukiingizwa kwenye chumba cha chini cha ardhi, ili kukutana na kuona wafungwa kadhaa wakijilinda kutokana na shambulio la Urusi.

Mabadilishano ya wafungwa yamekuwa kipengele cha kawaida cha vita hivi na kwa Kyiv ni muhimu kwao kuendelea. Ukraine ilisema mwezi huu imefanikisha kuachiliwa kwa wanaume na wanawake 1,762 kufikia sasa katika ubadilishaji wa wafungwa. Hizi ni shughuli nyeti sana, mara nyingi huchukua miezi kupanga.

Chini ya Mikataba ya Geneva, wafungwa wa vita hawapaswi kuoneshwa hadharani kwenye gwaride mbele ya Umma.

Tuliruhusiwa kukaribia tunayemtaka na tukaomba idhini yao. Lakini walinzi walikuwa pamoja nasi popote tulipokwenda na inaelekea watu hao walikuwa wakizungumza kwa uhuru.

Wengi walificha nyuso zao ili kulinda zaidi utambulisho wao.

Wafungwa hao wanaruhusiwa kupigiwa simu mara moja kila baada ya wiki mbili, kwa mujibu wawalinzi

Novemba mwaka jana, ripoti ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa iliandika dhuluma zilizofanywa na pande zote mbili, kulingana na mahojiano na wafungwa ambao walizungumzia matendo ya mateso na unyanyasaji.

Hapa walinzi walionekana kuwa na shauku ya kuonesha wanawatendea wema wafungwa.

Mpiganaji mmoja alisema amekuwa akifanya kazi na kikundi cha mamluki.

Alikuwa ameletwa katika kituo hiki siku tatu zilizopita, baada ya kuchukuliwa mfungwa karibu na mji wa mashariki wa Soledar, uliotekwa mwezi uliopita na majeshi ya Urusi.

Wachache walitazama kwa dharau. Tulikutana na macho ya mfungwa mmoja ambaye alisema alitekwa katika mkoa wa Luhansk mnamo 29 Desemba.

"Natumai nitabadilishwa na kwamba sitalazimika kurejea jeshini," alisema.

"Je, ikiwa huna chaguo?" Niliuliza.

Alinyamaza kwa sekunde: "Nina mawazo fulani. Ningeweza kurudi kwa kujisalimisha kwa hiari."

Kuondoka kwenye makao hayo ikawa wazi kwamba nusu ya wafungwa walikuwa wamejeruhiwa.

Wengine walikuwa wamefungwa mikono au miguu. Wengine walitembea kwa taabu sana.

Kijana mmoja alishikwa na hisia alipoeleza jinsi alivyopoteza mguu wake katika mlipuko wa guruneti.

Wafungwa wa vita wa Kirusi huunda seti za samani

Tulipokaribia sauti ya mashine ya kukandamiza, mstari mdogo wa wazalishaji ulionekana ambapo wafungwa wa vita walikuwa wakitengeneza seti za samani.

Walifanya kazi, tena wakiwa wameinamisha vichwa vyao chini.

Kampuni ya ndani ilikuwa na kandarasi na kituo hicho, tuliambiwa, na hiyo ilimaanisha kwamba wafungwa waliweza kupata pesa pia, nyingi za kutumia kununua sigara na peremende.

Wafungwa wengi wa vita wanalazimishwa kuwa na kazi kama hii. Inavyoonekana, maafisa wa Urusi tu ndio walikuwa na chaguo.

Wakati wa chakula cha mchana wafungwa waliandamana hadi kwenye kantini ya muda kwenye ghorofa ya juu. Kupitia dirishani bendera ya Kiukreni ilipigwa na upepo baridi.

Walikula haraka na kwa ukimya, lakini kwa sauti ya kula. Kisha, meza kwa meza, walisimama pamoja na kupiga kelele kwa Kiukreni: "Asante kwa chakula cha mchana.

Wafungwa hula mkate, supu ya mahindi, bakuli la shayiri na nyama
Maelezo ya picha, Wafungwa hula mkate, supu ya mahindi, bakuli la shayiri na nyama
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wafungwa hapa wanalazimishwa kutazama televisheni kwa lugha ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na filamu za historia ya Ukrainia na jiji la kusini la Mariupol, ambalo lilidhoofishwa kutokana na kuzingirwa na Urusi na mashambulizi ya mabomu yaliyodumu kwa miezi kadhaa.

Baadhi ya askari wa Kiukreni waliokuwa walioutetea mji wa Mariupol walikuwa sehemu ya mabadilishano ya mwisho.

Tulimuuliza mfungwa mmoja ikiwa alielewa alichokuwa akitazama.

Alisema. "Naona ni elimu." Hakukuwa na uwezekano wa kusema chochote kisichopendeza.

Inawezekana kabisa kwamba baadhi ya Warusi katika chumba hawakuweza kuelewa mpango ambao walikuwa wanapaswa kutazama, na huenda hawakutaka.

Wafungwa hao wanaruhusiwa kupiga simu moja kila baada ya wiki mbili, kulingana na walinzi. Kwa familia zao huko Urusi, simu hizi mara nyingi huwa nafasi ya kwanza ya kujua kwamba watoto wao wametekwa.

"Uko wapi? Nimeliuliza nusu ya jiji kuhusu wewe!" mama wa kijana mmoja alisikika kwenye simu.

"Mama, ngoja. Niko kifungoni, siwezi kusema zaidi."

"Pamoja na Waukraine ?" Alisema, kabla ya kuangua kilio.

"Ni hayo tu, Mama.," alimwambia, huku mlinzi akiwa amesimama nyuma yake. "Jambo muhimu zaidi ni kwamba niko hai na mwenye afya."

Baadhi ya simu za wafungwa ziliita bila kupokelewa, na kuwaacha wakitumaini kupata nafasi nyingine kwenye simu na kubadilishana wafungwa siku zijazo.