Kenya na Tanzania katika orodha ya nchi 10 bora zenye mamilionea wengi wa dola Afrika

TH

 Kenya na Tanzania zimo kwenye orodha ya nchi kumi zenye mamilionea wengi wa dola barani Afrika.Kenya ipo katika nafasi ya tano ilhali Tanzania inashikilia nafasi ta saba katika orodha hiyo inayoongozw na Afrika Kusini .

Hayo yametolewa katika ripoti mpya ya utajiri iliyotolewa na kampuni ya utafiti ya New World Wealth and Henley & Partners. 

Ripoti ya hivi punde ya Henley Global Citizen, ambayo hufuatilia mienendo ya uhamiaji wa utajiri wa watu binafsi duniani kote, inaonyesha Nairobi ina watu 5,000 wenye thamani ya juu (HNWI) wakiwa na angalau $1 milioni (Sh120 milioni).

Dar es salaam nchini Tanzania ina watu 1300 wenye utajiri mkubwa zaidi ikishikilia nafasi ya 12 Afrika kwa miji yenye matajiri wengi zaidi .

th

Chanzo cha picha, New World Wealth and Henley & Partners.

Maelezo ya picha, Mataifa yenye watu wenye utajiri mkubwa zaidi Afrika

Ripoti hiyo inaonyesha kitovu cha biashara cha Afrika Kusini Johannesburg kina mamilionea wa dola 15,200 - wengi zaidi barani Afrika - ikifuatiwa na mji mkuu wa Misri Cairo, ambao una watu matajiri zaidi 7,800.

Mji mwingine wa Afrika Kusini, Cape Town, ni wa tatu kwa ukubwa idadi ya watu matajiri kwenye wenye kipato cha juu , HNWI 6,800 ikifuatiwa na jiji lenye watu wengi zaidi la Nigeria, Lagos, ambalo lina 6,300.

Walakini, hakuna jiji la Kiafrika lililoingia kwenye orodha ya miji 20 bora ulimwenguni ambayo ina idadi kubwa ya mamilionea wa dola. Orodha hiyo ilitawaliwa na miji ya Marekani.

th

Chanzo cha picha, New World Wealth and Henley & Partners.

Maelezo ya picha, Miji ya Afrika yenye watu matajiri zaidi
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Jiji lenye watu wengi zaidi nchini Marekani, New York, lina mkusanyiko mkubwa zaidi wa mamilionea wa dola duniani, nyumbani kwa watu 345,600, wenye kipato cha juu zaidi ikifuatiwa na Tokyo na San Francisco Bay Area yenye 304,900 na 276,400, mtawalia.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Henley & Partners Juerg Steffen alibainisha kuwa miji 14 kati ya 20 tajiri zaidi duniani iko katika nchi ambazo zinaandaa programu rasmi za uhamiaji wa uwekezaji, na kuhimiza kikamilifu uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni kama malipo ya makazi au uraia.

Ripoti hiyo inaonyesha Nairobi pia ni nyumbani kwa mamilionea 240, ambao wana utajiri wa zaidi ya dola milioni 10 (Sh1.2 bilioni), na mamilionea 11, ambao wana thamani ya zaidi ya $ 100 milioni (Sh12 bilioni). Mji mkuu wa Kenya, hata hivyo, hauna bilionea wa dola.

"Kuweza kujihami, familia yako, au biashara yako hadi jiji linalofaa zaidi au kuwa na chaguo bora kati ya makazi mengi kote ulimwenguni ni kipengele muhimu zaidi cha utajiri wa kimataifa na upangaji wa urithi kwa wateja wa kibinafsi," alisema. 

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Idadi ya mamilionea wa dola jijini Nairobi, hata hivyo, imeshuka kwa asilimia 7 katika kipindi cha miezi sita hadi Juni, ikisisitiza matatizo ya kiuchumi yanayowakabili wawekezaji huku kukiwa na mazingira magumu ya kiuchumi yanayotokana na mfumuko wa bei.

Mfumuko wa bei - ambao ulifikia kiwango cha juu cha miaka mitano mwezi uliopita - umeathiri vibaya matumizi, na kusababisha ukuaji wa sekta binafsi kupungua kwa miezi mitano mfululizo hadi Julai.

Utendaji duni wa sekta ya kibinafsi umewaathiri vibaya wawekezaji matajiri, ambao wengi wao walipunguza uwekezaji katika maandalizi ya uchaguzi wa Agosti.

Kenya ina mamilionea wa dola 8,500, kulingana na Ripoti ya Utajiri ya Afrika 2022, ambayo ilitolewa na kampuni hiyo mwezi Aprili. Hii ina maana kwamba Nairobi ni nyumbani kwa asilimia 59 ya watu wenye kipato cha juu zaidi ikisisitiza hadhi yake kama kitovu cha uchumi wa Kenya.