Kifahamu kikosi cha Jeshi la Israel katika milima ya Golan

SX

Chanzo cha picha, IDF

Maelezo ya picha, Wanachama wa Brigadi ya Golan ya Jeshi la Israel
Muda wa kusoma: Dakika 4

Kundi la Hezbollah lilitangaza katika taarifa yake kuhusu moja ya mashambulizi yake ya hivi karibuni dhidi ya Israel, kwamba shambulio la ndege isiyo na rubani ililenga makao makuu ya Brigedi ya Golan katika ngome ya kaskazini ya Acre.

Kikosi cha Israel cha Golan kimepewa jina la Miinuko ya Golan ya Syria na ni miongoni mwa kikosi cha awali cha jeshi la Israel, ndiyo maana pia kinaitwa Brigadi ya Kwanza.

Brigedia hii, ambayo ni ya kikosi cha wanajeshi wa ardhini, ni moja ya vikosi muhimu kwa jeshi la Israel. Dhamira ya kikosi hiki ni kujiimarisha kwenye mpaka wa Syria na Israel, kwenye mabonde na vilima vya Galilaya ya kusini.

Pia unaweza kusoma

Kuanzishwa kwa Kikosi cha Golan

ds

Chanzo cha picha, IDF

Maelezo ya picha, Nembo ya Brigedia ya Golan

Brigedi hiyo ilianzishwa Februari 22, 1948, baada ya David Ben-Gurion kuchukua wadhifa wa waziri mkuu wa kwanza wa Israel. Kikosi hiki kiligawanywa katika brigedi mbili, Golan na Carmeli, kutoka brigedi ya Livanoni, iliyokuwa ikipigana kwenye mpaka wa Lebanon.

Kikosi cha Golan kilijumuisha askari kutoka shirika la walowezi la Haganah, na vikosi kutoka kote Israel, na kilikuwa na silaha za hali ya juu.

Haganah lilikuwa kundi la wanamgambo la Israel lililoanzishwa mwaka 1920 ambalo dhamira yake ilikuwa kulinda maisha na mali ya Wayahudi dhidi ya mashambulizi ya Waarabu. Kundi hili lilikuwa mwanzilishi mkuu wa jeshi la Israel, na viongozi wake walishika nyadhifa za kisiasa na kijeshi mmoja baada ya mwingine.

Askari wa kwanza wa brigadi hii walikuwa wakulima wahamiaji, kwa hivyo, nembo ya brigadi ya Golan ni mti wenye mizizi mingi wenye rangi ya manjano, ambayo inaashiria uhusiano na ardhi.

Mti huu unaashiria ni mzeituni. Rangi ya kijani kibichi inaashiria vilima vya kijani kibichi vya mkoa wa Galilaya, na rangi ya manjano inaashiria jangwa la Negev ambapo Brigadi ya Golan ilipigana mwaka 1948.

Brigedi hiyo ina maelfu ya wanajeshi, wanaoaminiwa kuwa na mafunzo bora miongoni mwa vikosi vya Jeshi la Israel, na baadhi ya vitengo vyake hupitia mafunzo makali na magumu.

Kikosi cha Golan ni sehemu ya Kitengo cha 36 cha Jeshi la Israel na kipo chini ya Kamandi ya Kaskazini.

Kikosi hiki ndicho kikosi pekee ambacho kinaendelea kufanya kazi tangu kuanzishwa kwa jeshi la Israel na kimegawanyika katika vikosi vinne: Kikosi cha Hebokim Harashon, Kikosi cha Barak, Kikosi cha Gideon na Kikosi cha Reconnaissance.

Muundo wa Kikosi cha Golan

FDC

Chanzo cha picha, IDF

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kikosi cha Habokim Harashun: Mwaka 1948, jeshi la Israel lilituma kikosi hiki - kukabiliana na kuzuia kusonga mbele kwa jeshi la Misri kwenye jangwa la Negev.

Kikosi cha Barak: Kilianzishwa kabla ya kuundwa kwa serikali ya Israel. Jina la kikosi limechukuliwa kutoka kwa Barak bin Abi Naam, ambaye alikuwa mmoja wa majaji wa wana wa Israel na jina lake limetajwa katika Biblia. Tangu 1948, kikosi hiki kimekuwepo katika vita vyote ambavyo Brigadi ya Golani ilishiriki.

Kikosi cha Gideon: Kikosi hiki kimepewa jina la mmoja wa majaji wa wana wa Israel, ambaye jina lake limetajwa katika kitabu cha Judges na kitabu cha kwanza cha Samuel. Tangu 1948, kikosi hiki kimeshiriki katika vita kadhaa vya brigadi ya Golan.

Kikosi cha Reconnaissance: Kikosi hiki hakina jina maalumu. Kilianzishwa mwaka 2001 na kimekuwepo katika vita vyote vya Brigadi ya Golan tangu wakati huo.

Sharti la kujiunga na kikosi hiki ni kufaulu vipimo na tathmini za kimwili na kiakili, askari wenye uwezo bora wa kimwili na kiakili ndio huchaguliwa kuhudumu humo. Kazi za kikosi hiki ni siri.

Operesheni kubwa zaidi

C

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vifaru vya Israel vimechora nyota

Mara tu baada ya kuanzishwa kwake, Brigedi ya Golan ilishiriki katika vita vya 1948 na kujaribu kuzuia kusonga mbele kwa majeshi ya Syria, Lebanon, Jordan na Iraq.

Katika vita vya 1967, kikosi hiki kilishiriki katika vita dhidi ya majeshi ya Waarabu kwenye mipaka ya Jordan na Syria .

Kikosi hiki pia kilishiriki katika vita vya 1982 nchini Lebanon, ambavyo vilisababisha kukaliwa kwa mabavu kusini mwa nchi hiyo, na kuchukua jukumu muhimu katika Vita vya Qala Shaqif, na kuingia katika vitongoji vya Beirut. Brigedi ya Golan pia ilishiriki Vita vya Lebanon vya 2006.

Kikosi hiki kwa sasa kinashiriki kwenye vita vya Gaza tangu Oktoba 7, 2023.

Imetafsirwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Seif Abdalla