Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Utafutaji wa namba za bahati nasibu zinazoendesha maisha yetu
- Author, Chris Baraniuk
- Nafasi, BBC
- Muda wa kusoma: Dakika 4
Ulimwengu wetu unatumia nambari zinazozalishwa kwa bahati nasibu na bila ya nambari hizo, sehemu ya maisha ya sasa inaweza kuharibika.
Turudi nyuma kidogo. Kundi la marafiki zake lilijitahidi kumwelezea muuza duka kile wanachotaka, redio ambayo sauti yake inakwama kwama. Muuza duka hakujua la kusema.
"Nadhani alifikiri sisi ni wendawazimu," anakumbuka Mads Haahr. Ilikuwa 1997. Yeye na marafiki zake walikuwa katika duka la Radio Shack huko Berkeley, California.
Baada ya kumshawishi, mfanyabiashara huyo alikubali kuwaruhusu Haahr na marafiki zake wasikilize mojawapo ya redio ya bei nafuu zaidi aliyokuwa nayo.
Walipokuwa wakiingiza betri kwenye redio hiyo, sauti ya kelele ilisikika. Ilikuwa na kelele kama kuzimu. "Tulifurahi," anasema Haahr.
Redio hiyo ndogo, ilikuwa karibu kuwatajirisha. Haahr na marafiki zake watatu walikuwa wakifanya kazi kwenye programu ya kamari.
Haahr alitaka kuwa na uwezo wa kuzalisha nambari za bahati nasibu. Mitiririko usiokwisha wa tarakimu ambazo zingeamua mchezo wa kamari ya mtandaoni.
Kelele inayotolewa na redio hiyo, ni ishara ya kelele inayoundwa na umeme na shughuli za sumakuumeme katika angahewa ya dunia.
Mpango wa Haahr, ni kuifanya kompyuta isikilize kelele hizo, na kuzibadilisha kuwa nambari na kisha kuzitumia kutengeneza mifuatano ya nambari za bahati nasibu - mfano, 4107567387.
Kuna baadhi ya mambo ambayo kompyuta, kwa umahiri wake wote, haiwezi kufanyi vizuri - na mojawapo ni kubahatisha.
Kwa muda mrefu watu wametafuta vyanzo mbalimbali ili kuzalisha namba za bahati nasibu. Katika utafutaji huu, wametumia matukio ambayo hayawezi kutabiriwa. Kama sauti za dhoruba za radi ama matone ya mvua.
Mwishowe, redio ndogo ya kijivu haikumfanya Haahr na marafiki zake kuwa matajiri hata kidogo. Biashara ya michezo ya kubahatisha mtandaoni ilienea.
Lakini uzalishaji wa nambari za bahati nasibu waliamini bado ni muhimu. Kwa hivyo Haahr alianzisha random.org, ambapo hutoa nambari za bahati nasibu tangu. Na kuna wageni wengi wanatembelea tangu wakati huo.
"Ninaweza kutaja Ofisi ya Meya wa San Francisco," anasema Haahr. "Wanatumia huduma yetu kupata washindi ambao wamebahatika kupata nyumba za bei nafuu."
Watumiaji wengine ni pamoja na watu wanaoendesha kamari. Wanachagua nambari za kushinda kila wiki kwenye tovuti ya Haahr.
Hata wanasayansi, hutumia nambari hizo za mtandaoni kuwapasisha washiriki katika mitihani. Kampuni za biashara zinazotoa zawadi kwa wateja, pia huchagua washindi wao kwa usaidizi wa random.org.
"Watu huitumia kwa uchunguzi wa madawa," anaongeza Haahr. "Kuchagua wafanyakazi bila mpangilio." Tovuti pia ina kituo cha kuchagua nenosiri la bahati nasibu. Na baadhi ya huduma za kamari za mtandaoni zinategemea random.org.
Tunazitumia bila kujua
Iwapo hujawahi kuingia kwenye bahati nasibu au huna nia ya kushiriki katika jaribio la bahati nasibu, unaweza kufikiri kwamba nambari za namna hiyo hazikuhusu. Lakini si kweli.
Kila unapochagua neno jipya la siri, hata lile unalotengeneza mwenyewe, kompyuta huongeza taarifa katika neno hilo. Kumaanisha kwamba, mtu akidukua hifadhidata na kuiba nenosiri lako, hawezi kulichambua kwa urahisi na kulitumia kufikia akaunti yako.
Sehemu hiyo ya taarifa iliyoongezwa inatokana na nambari ya bahati nasibu.
"Tunazitumia kila siku bila kujua," anasema Alan Woodward, mtaalam wa usalama wa kompyuta katika Chuo Kikuu cha Surrey.
Unapotembelea tovuti inayoanza na "https://", kwa mfano, unaiomba kompyuta yako na seva inayohifadhi tovuti, itengeneze nambari, izibadilishe na kuwa taarifa wakati unapoendelea kuitumia tovuti.
Orodha ya mambo ambayo watu wametumia katika kutafuta nambari za bahati nasibu ni ya ajabu sana. Mhandisi mmoja wa programu aligundua alipokuwa anatembea siku ya mvua kwamba matone ya mvua yanayoanguka kwenye miwani yake yanaweza kutoa nambari hizo.
Mtu mwingine alijaribu kunasa shughuli za samaki kwenye tanki la samaki kama msingi wa kutengeneza nambari hizo. Njia nyingine ilitegemea tabia isiyotabirika ya paka.