Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Tottenham itafanikiwa kumrejesha Ivan Toney EPL?
Meneja wa Tottenham Thomas Frank anataka kuungana tena na mshambuliaji wa Al-Ahli na England Ivan Toney mwenye umri wa miaka 29 - ambaye alicheza chini yake katika klabu ya Brentford. (Sportsport)
Mshambuliaji wa Real Madrid wa Brazil Rodrygo, 24, pia yuko kwenye orodha ya washambuliaji wanaolengwa na Tottenham. (Teamtalk)
Arsenal imeweka thamani ya euro 150m (£132m) kwa kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 26, ambaye anashangiliwa na Real Madrid. (Fichajes - kwa Kihispania)
Chelsea imeulizia mchezaji wa Como Nico Paz, 21, lakini inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Real Madrid, ambao wanaweza kutaka kumsajili tena kiungo huyo wa Argentina. (TBR Football)
Newcastle "haijatoa" tamko lolote baada ya kauli ya Sandro Tonali kuhusu mustakabali wake, na hhaitaanza mazungumzo rasmi kuhusu mkataba mpya wa kiungo huyo kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 25 hadi baadaye msimu huu. (Mail Plus - usajili unahitajika)
Newcastle wako kwenye mazungumzo na mlinzi wa Uholanzi Sven Botman, 25, kuhusu kandarasi mpya, lakini mlinzi wa Uswidi Emil Krafth, 31, anavutiwa na FC Copenhagen. (Mail Plus - usajili unahitajika)
Barcelona inapanga kuwasiliana rasmi na klabu ya Manchester United kuhusu mkataba wa kudumu kwa mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 28. (Teamtalk)
Napoli huenda ikafufua nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United na Uingereza Kobbie Mainoo, 20, mwezi Januari. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Chelsea, Tottenham, Manchester City, Leeds, Everton, Barcelona na Real Madrid ni miongoni mwa vilabu vingine vinavyovutiwa na Mainoo. (Caught Offside)
Borussia Dortmund wanataka kumsajili tena winga wa Uingereza Jadon Sancho, 25, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Aston Villa kutoka Manchester United. (Football Insider)
Real Madrid ina matumaini ya kumsajili mlinzi wa Bayern Munich na Ufaransa Dayot Upamecano, 27, kwa uhamisho wa bure mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Sky Germany - kwa Kijerumani)
Atletico Madrid inamfuatilia beki wa Chelsea Mhispania Marc Cucurella, 27, lakini haina mpango wa kumsajili hadi msimu ujao wa joto. (Fichajes - kwa Kihispania)
Ajax wamewasiliana na meneja wao wa zamani - na mkufunzi wa zamani wa Manchester United - Erik ten Hag ili kurejea baada ya kumsimamisha kazi kocha mkuu John Heitinga. (Fabrizio Romano)