Je, wajua kanisa kubwa zaidi barani Afrika lilikuwa nchini Somalia?

Kanisa la Mogadishu
Maelezo ya picha, Kanisa la Mogadishu

Kanisa maarufu la Mogadishu Cathedral nchini Somalia lilijengwa mwaka 1928, na lilikuwa kubwa zaidi barani Afrika, lakini liliharibiwa vibaya baada ya 1991, serikali kuu ilipoanguka.

Askofu wa mwisho aliyeongoza kanisa hilo aliitwa Salvatore Colombo ambaye aliuawa mwaka 1989 alipokuwa akitoa hotuba kanisani.

Padre Colombo, ambaye alikuwa na umri wa miaka 66 alipouawa, alizikwa mjini Mogadishu. Baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mwili wake ulifukuliwa na kutolewa dhahabu kutoka kwa meno yake. Baadaye mabaki yake yalichukuliwa na kuzikwa tena huko Milan, Italia.

Mauaji ya Papa Colombo bado hayajatatuliwa. Hakuna papa mwingine baada yake aliyeteuliwa kwenye kiti cha enzi.

tt

Kanisa hilo liliundwa na Antonio Vandone, mbunifu kutoka Italia.

Somalia ilikuwa nchi ya Kiislamu ambapo koloni lisilo la Kiislamu lilikuja kwa nguvu. Kuanzishwa kwa kanisa kuliamriwa na Cesare Maria De Vecchi, ambaye alikuwa mtawala wa maeneo ya kusini mwa Somalia chini ya udhibiti wa Somaliland ya Italia.

Kusudi lake lilikuwa kukuza Ukristo. Cesare Maria alitaka Wasomali wengi kubadili dini na kuwa Wakristo. Ili kufikia lengo hilo alijenga kanisa kubwa ambalo lilifananishwa na lile la Italia, hasa Sicily.

Karibu Wakristo 8,500 waliishi Somalia mwaka wa 1950.

Wanajeshi wa Italia waliofunga ndoa na Wasomali walisababisha kuongezeka kwa idadi ya Wasomali na Waitaliano ambao wanaamini Ukristo.

Baada ya kupungua kwa ushawishi wa Italia nchini Somalia katikati ya karne ya 20, idadi ya Wakristo wanaoishi Somalia ilipungua.

Kanisa hilo hapo awali lilikuwa ishara ya Mogadishu huku minara yake ikionekana lakini ilipoharibiwa ikawa makazi ya watu waliokimbia makwao.

Mipango ya kukarabati kanisa hilo iliibuka mnamo 2013 lakini hakuna ujenzi mpya ambao umeanzishwa.