Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 31.08.2024
Liverpool wanafikiria kumnunua mlinzi wa Crystal Palace, Marc Guehi, huku Victor Osimhen akitarajiwa kuwa nje ya uwanja wa Napoli.
Liverpool wanaweza kumnunua beki wa kati wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 24, msimu ujao wa joto, wakati atakuwa amebakisha mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake. Guehi alikuwa akilengwa na Newcastle katika dirisha la usajili msimu huu. (Mirror)
Manchester United ilikataa ombi la mkopo kutoka kwa Real Betis kwa winga wa Brazil Antony, 24, na kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 32, siku ya mwisho ya kuhama. (Mail)
Mshambulizi wa Nigeria Victor Osimhen, 25, hatajumuishwa katika kikosi cha Napoli baada ya kushindwa kupata uhamisho wa kwenda Chelsea. (Gianluca di Marzio kwenye X)
Mazungumzo ya kumnunua mshambuliaji wa Chelsea, Deivid Washington kwa pauni milioni 16.8 kwenda Strasbourg yaligonga mwamba baada ya kuhofia uhamisho huo ungechunguzwa kwani klabu zote mbili zinamilikiwa na BlueCo. (L'Equipe - in French)
Imetafsiriwa na Asha Juma