'Huku ukipoteza pesa, tangazo litapelekwa mpaka redioni mpaka uzipate pesa zako'

Maelezo ya video, Je umewahi kufanyiwa ukarimu? hilo jambo la kawaida kwa wengi waishio Zanzibar

Je umewahi kufanyiwa ukarimu ambao huenda ungetamani kurudisha fadhila? Basi hilo jambo la kawaida kwa Wananchi wengi waishio Visiwani Zanzibar.

Kwa miaka mingi visiwa hivyo vimefahamika kwa kuwa na watu wakarimu na wenye hofu ya Mungu pale wanapojitoa katika kuwasaidia wengine wapatapo shida fulani hasa wageni.

Mwandishi wa BBC @frankmavura ametembelea visiwa hivyo akiwa katika kazi zake za uandishi na kukutana ana kwa ana na ukarimu wa watu visiwani humo.