Utamaduni wa kutabiri jinsia ya mtoto tumboni kwa kumtazama mjamzito nchini Pakistan

SAAAAADS
Maelezo ya picha, Amberin Zulfiqar, Firdous and Asma Naaz

Mchezo wa magongo (hoki) ndio mchezo wa kitaifa nchini Pakistan, lakini katika jamii hiyo, mchezo wa kutabiri ikiwa mtoto ni wa kiume au wa kike huenda ndio wa zamani zaidi kuliko huo wa magongo.

Utabiri huu unaweza kusababisha maumivu bila kujua au kuongeza matarajio kwa mama wajawazito. Nilizungumza na wanawake wachache ambao wamenieleza uzoefu wao.

Kutazama ngozi

Mwanamke mfanyabiashara Ambrin Zulfiqar ana ujauzito wa miezi tisa. Akielezea uzoefu wake, anasema kwamba watu walijaribu sana kutabiri jinsia ya mtoto wao ambaye hajazaliwa.

Ndipo watu wakasema kwa vile ngozi yake inang'aa, atapata mvulana. Anasema watu hawaelewi kuwa huwezi kujua kama ni mvulana au msichana kwa kuangalia.

Bize sana, utakuwa na binti

Asmanaz ni mama aliyejifungua karibuni. Anasema kwamba watu wanaofanya kazi naye ofisini walisema kuwa tabia yake ilimfanya wafikirie kuwa atapata mtoto wa kike.

Alihisi ajabu sana kusikia kwanini mtu anamtazama kuanzia juu hadi chini na kutoa maoni yake iwapo atakuwa na binti au mtoto wa kiume.

Kwa upande mwingine, kwa mujibu wa mwanamke mwingine Firdous, mama mkwe wake alimwambia kuwa amekuwa bize sana, safari hii utapata binti na akapata mtoto wa kike.

wwwwqwqwq

Upi ukweli kuhusu utabiri huu?

Ili kujua ukweli kuhusu utabiri uliotolewa kuhusu 'wakike au wakiume', nilkwenda kwa mshauri wa magonjwa ya wanawake katika Hospitali ya Kimataifa ya Shifa Islamabad, Dkt. Shahnaz Nawaz, na kumuuliza maswali machache.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kutamani chakula kitamu au chenye viungo: Dk Shahnaz anaeleza kuwa ni kawaida kutamani chakula kitamu au chenye chumvi nyingi wakati wa ujauzito, lakini haiwezi kukuambia jinsia ya mtoto.

'Ikiwa mwanamke anatamani peremende, inamaanisha kuwa kiwango chake cha sukari kwenye damu ni kidogo. Ikiwa kuna ukosefu wa chumvi katika mwili, kunaweza kumfanya awe na hamu ya kula chakula cha chumvi au chenye viungo vingi, yaani, inategemea kile kinachopungua katika mwili wakati wa ujauzito.'

Kuketi au kusimama kwa namna fulani: Kulingana na Dkt. Shahnaz, hakuna utafiti unaoweza kubainisha iwapo mwanamke mjamzito anayeketi kwa namna fulani atakuwa na mvulana au msichana.

Ngozi kung’aa, mistari ya shingo au chunusi: Kuhusu hilo Dk Shahnaz anasema wakati wa ujauzito, mwili huzalisha homoni nyingi iwe mtoto wa kike au wa kiume, ambazo husababisha ngozi ya mjamzito kuvimba. Kuhusu chunusi au mistari kwenye shingo pia yanaweza kuonekana. Haina uhusiano wowote na kuwa na mtoto wa kike au kiume.

Kichefuchefu kwa wingi: Kulingana na Dkt. Shahnaz, kichefuchefu kupindukia huhusiana na homoni ambazo hutolewa kwa wingi kwenye plasenta na kufikia kilele chake baada ya wiki 12. Na kisha huanza kupungua.

Kufikia wiki ya 16, viwango vya homoni hupungua sana na kichefuchefu kukoma. Hata hivyo, kila mimba ni tofauti, mwanamke huyo huyo anaweza kuwa na kichefuchefu zaidi katija mimba mmoja na kupunguza kichefuchefu mimba ijayo.

ghf
Maelezo ya picha, Dkt. Shahnaz

Vipimo vya maabara

Kipimo cha Ultrasound: Kwa mujibu wa Dkt. Shahnaz, huu ni mtihani usio wa lazima kwa sababu haufichui chochote kuhusu afya ya mama au mtoto, lakini baadhi ya wanawake wanakuwa kwenye shinikizo kubwa la kuzaa mtoto wa kiume kiasi kwamba wanapogundua kuwa wanajifungua msichana - matokeo yake, hutoa mimba isivyo salama, ambazo zinaweza kuhatarisha maisha.

Dkt. Shahnaz anasema kipimo cha ultrasound kinaweza kufanyika baada ya wiki 12 za ujauzito lakini kwa matokeo bora Zaidi kinaweza kufanyika baada ya wiki 14 na kinaweza kubaini iwapo ni mvulana au msichana.

Kipimo cha NIPT: Katika kipimo hiki, sampuli ya damu ya mama mjamzito inachukuliwa kwa sababu wakati wa ujauzito, DNA ya mtoto huingia kwenye damu ya mama.

Hii inaweza kuamua jinsia ya mtoto. Kipimo hiki ni ghali kabisa na kwa sasa hakuna kituo cha kipimo hiki nchini Pakistan.

Uchambuzi wa Chromosomal: Kipimo cha uchanganuzi wa kromosomu kinaweza pia kujua jinsia ya mtoto.

Kwa mujibu wa Dkt. Shahnaz, kutabiri jinsia ya mtoto mbele ya akina mama wajawazito kunaweza kuongeza matarajio yao, ambapo inaweza kumsababishia maumivu ikiwa matarajio hayo hayakufikiwa.

Dk Shahnaz anasema kutokana na ukosefu wa elimu, watu hufikiri kwamba ni juu ya mwanamke kupata mvulana au msichana.

'Kwa kawaida wanawake wana wana kromosomu XX (chembechembe za jeni) na wanaume wana XY. Mwanamke anaweza kutoa chromosome ya X tu ya kuzaa mtoto, ikiwa chromosome ya X pia inapokelewa kutoka upande wa kiume, itakuwa msichana na ikiwa Y itapokelewa, basi itakuwa mvulana. Ingawa hakuna uwezo mwanamme kuamua kutoa kromosomu ya X au ya Y.