Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita vya Ukraine: Olaf Scholz asema Vladimir Putin haichukulii vita ya Ukraine kama kosa
Rais wa Urusi Vladimir Putin haelewi kuwa uvamizi wa Ukraine ni kosa, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema, baada ya viongozi hao kufanya mazungumzo kwa njia ya simu siku ya Jumanne.
Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano, Bw Scholz alisema kuwa alimtaka Bw Putin kuondoa vikosi vyake na kuingia upya katika mazungumzo na Ukraine wakati wa mazungumzo yao ya simu ya dakika 90.
Aliitolea wito kwa Urusi kuheshimu mamlaka ya Ukraine.
Kansela wa Ujerumani amekabiliwa na shinikizo la kuongeza usaidizi kwa ajili ya Kyiv.
Bw Scholz alisema kuondoka kwa vikosi vya Urusi nchini Ukraine itakuwa njia pekee ya "amani kuwa na fursa katika kanda hiyo ".
Ingawa alisema kuwa Bw Putin "kwa bahati mbaya "hajabadili msimamo wake kuhusu uvamizi, Bw Scholz alisisitizia umuhimu wa kuendelea kuzungumza naye.
"Ni sahihi kusemezana na kusema nini cha kusema katika suala hili ," Bw Scholz alisema.
Alidai pia kwamba silaha ambazo Ujerumani iliipatia Ukraine "zimeleta mafanikio ya uhakika" na "kuleta mabadiliko tofauti" mashariki mwa Ukraine.
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, ameikosoa Ujerumani kwa kutotuma silaha zaidi.
Aliandika kwenye ukurasa wa Twitter Jumanne kwamba Ukraine inahitaji usaidizi zaidi wa kijeshi, kuwakomboa watu na kuwanusuru na mauaji ya kimbari’’.
"Hakuna hoja hata moja ya busara kuhusu ni kwanini silaha hizi haziwezi kuletwa, ni hofu tu na visingizio. Kile ambacho Berlin inaogopa cha Kyiv sio ?" aliongeza.
Ikizungumza kuhusu mazungumzo ya simu na Bw Scholz, Kremlin iliilaumu Ukraine kwa kuendelea kwa ghasia.
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine katika mwezi Februari umekuwa changamoto kwa msimamo wa muda mrefu wa kidipmomasia wa Berlin kuihusu Moscow – ambayo imekuwa ikiitegemea hivi karibuni kwa uchumi wake wa mafuta na gesi.
Na mapema mwaka huu, Bw Scholz alibatilisha sera ya miongo kadhaa ya jeshi ya la Ujerumani ya kubana matumizi, kwa kutangaza kwamba nchi hiyo itahitaji matumizi ya 2% ya pato la ndani la taifa(GDP) kwa ajili ya matumizi ya jeshi, ili kuweza kutekeleza malengo ya Nato.
kielelezo cha udhamini msaada wa kijeshi kwa Ukraine:
Kufikia mwezi Agosti Ujerumani ilikuwa imetoa msaada wa zaidi ya dola bilioni $1.2 wa kijeshi kwa Kyiv – kiwango muhimu, lakini ambacho ni cha chini sana kuliko kiwango cha msaada unaotolewa na Uingereza na Marekani, na hata cha chini kuliko Poland, ambalo ni taifa lenye uchumi mdogo zaidi.
Jumatano waziri wa ulinzi wa Ujerumani Christine Lambrecht aliahidi silaha zaidi kwa Ukraine, jenereta zaidi , nguo za baridi, na mahema ambayo tayari alihidi kuyatoa wiki iliyopita huku msimu wa baridi ukikaribia.
Akizungumza na shirika la habari la Reuters, Bi Lambrecht alielezea mashambulizi yanayoendelea Ukraine ya kukabiliana na uvamizi kutoka Urusi kama mafanikio ya "ajabu", ingawa alisisitiza kuwa ni mapema kubashiri ni vipi Urusi itajibu.
"Hii inathibitisha kuwa vikosi vya Ukraine vimejipanga vyema sana kimkakati , na wana uwezo wa kuzuwia mashambulizi jambo ambalo wengi hawakufikilia wana uwezo wa kulifanya," alisema.