Jinsi Ukraine ilivyobadilika katika kipindi cha miaka mitatu

Chanzo cha picha, Getty Images
Vita nchini Ukraine vimekuwa vikiendelea kwa miaka mitatu sasa, na kila rasilimali inahitajika ili kushinda. Kwa upande wa Ukraine hali kuhusu silaha na pesa ilionekana kuwa thabiti zaidi hasa kutokana na msaada wa washirika wake.
Idhaa ya BBC Ukraine imekusanya takwimu muhimu zinazoonyesha jinsi Ukraine imefanikiwa kuendelea kuonyesha uimara wake katika kipindi cha miaka mitatu ya vita na jinsi inavyoingia mwaka wa nne, ambapo haitarajiwi tena kupata ushindi au kufanya mashambulizi ya kujilinda badala yake ni kuingia katika makubaliano ya amani.
Kupungua kwa idadi ya watu

Chanzo cha picha, Getty Images
Sensa ya idadi ya watu nchini Ukraine ilifanyika mnamo 2001. Kabla ya uvamizi wa Urusi, watu milioni 41-42 waliishi Ukraine (ukiondoa Crimea iliyokaliwa na sehemu za mikoa ya Donetsk na Luhansk), kulingana na makadirio mbalimbali.
Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, tangu Februari 2022, idadi ya watu wa Ukraine imepungua kwa zaidi ya milioni 10, yaani, robo ya watu wote.
Wataalamu wanazidi kuamini kuwa kupungua kwa idadi ya watu, ni jambo lisiloweza kuepukika, na, kwa hakika, hii tayari linatokea.
Kufikia Julai 2024, watu milioni 30 waliishi katika eneo linalodhibitiwa na Ukraine, kulingana na takwimu kutoka kwa kampuni tatu za rununu za Ukraine.
Kwa mujibu wa ripoti ya CIA iliyotolewa mwishoni mwa 2024, kiwango cha vifo nchini Ukraine ni takribani 18.6 kwa kila watu elfu moja. Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi duniani.
Urusi iliorodheshwa kuwa nchi ya tisa katika ripoti hii, ikiwa na kiwango cha vifo vya watu 14 kwa kila watu elfu moja.
Kulingana na takwimu za CIA ya 2024, Ukraine pia ina kiwango cha chini zaidi cha watoto waliozaliwa duniani - watoto sita kwa kila watu elfu moja- nchi hii ikishika nafasi ya 228 katika orodha hii.
Raia na wanajeshi majeruhi

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kulingana na UN, idadi ya vifo vya raia nchini Ukraine imeongezeka sana mnamo 2024.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kisiasa Rosemary DiCarlo, idadi ya vifo na majeruhi kutokana na hatua za kijeshi za Urusi imeongezeka kwa 30% ikilinganishwa na mwaka uliopita. Takwimu hizi zilitolewa wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo Januari 2025.
Umoja wa Mataifa ulitilia maanani sana ongezeko la vifo vya watoto majeruhi vilivyorekodiwa katika robo tatu ya kwanza ya mwaka 2024.
Kulingana na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa (OHCHR), takriban watu 12,456 wameuawa tangu kuanza kwa uvamizi nchini Urusi, wakiwemo watoto 669.
Mwaka mmoja uliopita, Umoja wa Mataifa uliripoti vifo vya raia 10,191.
Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba takwimu zinaonyesha vifo vilivyothibitishwa tu, na kwamba idadi halisi ya waathiriwa inaweza kuwa kubwa zaidi.
Majeruhi kati ya jeshi
Wakati wa miaka mitatu ya vita, mamlaka ya Ukraine ilitoa kwa uchache takwimu juu ya majeruhi wa kijeshi mara chache.
Hata hivyo, mapema Februari 2025, Rais Zelensky alitaja takwimu hizi katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Uingereza Piers Morgan.
Alipoulizwa kuhusu hasara wakati wa vita, na hasa kuhusu kauli za Rais wa Marekani Donald Trump kwamba Ukraine ilipoteza wanajeshi 400,000, Rais Zelensky alisema kwamba idadi ya waliouawa katika jeshi la Ukraine ilikuwa 45,100.
Mwaka mmoja uliopita, Rais Zelensky alizungumza juu ya wanajeshi elfu 31 waliokufa. Wengine elfu 390 walikuwa majeruhi.
Wakimbizi wa ndani ya Ukraine
Kulingana na Wizara ya Sera ya Kijamii, mwanzoni mwa Desemba 2024, wakimbizi wa ndani milioni 4.9 walikuwa wamesajiliwa nchini Ukraine.
Kati ya hawa, milioni 3.6 ni watu ambao walikimbia makazi yao baada ya kuanza kwa uvamizi.
Milioni 2.5 kati yao hawawezi kurudi nyumbani kwao kwa sababu nyumba zao zimeharibiwa, ziko katika eneo la mapigano yanaloendelea, au ni katika eneo linalokaliwa kwa muda.
Wakimbizi waliokimbilia nje ya nchi

Chanzo cha picha, Getty Images
Kulingana na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), kufikia katikati ya Januari 2025, karibu wakimbizi milioni 6.9 kutoka Ukraine walisajiliwa duniani kote. Kati ya hawa, milioni 6.3 waliishia Ulaya.
Mwanzoni, idadi kubwa zaidi ya Waukraine waliokimbia vita walikwenda Poland, lakini baadaye Ujerumani ikawa inaongoza.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya Waukraine 993,000 kwa sasa wanafurahia ulinzi wa muda nchini Poland, ingawa ni milioni 1.9 tu ndio wamepokea hadhi hii wakati wa vita.
Kulingana na UN, karibu watu milioni 1.269 wa Ukraine waliishia Urusi na Belarusi.
Matumizi ya vita
Kama Idhaa ya Ukraine ya BBC ilivyofahamishwa na Wizara ya Fedha ya Ukraine, matumizi ya bajeti ya usalama na ulinzi kwa mwaka 2024 yalifikia karibu (dola bilioni 51.9). Hiyo ni wastani, siku ya vita iligharimu karibu (dola milioni 142).
Zaidi ya shilingi trilioni 2.2 (dola bilioni 49) zimetengwa kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi mnamo mwaka 2025, ambayo ni 26.3% ya Pato la Taifa.
Mfano wa zamani na kinachotokea Ukraine
Tofauti na wanaume msituni kwenye mpaka wa Kursk, wao hufuata habari. Kubadilika kwa mipango ya kidiplomasia na ya kimkakati ya Donald Trump, yaliyoanza katika mkutano wa usalama wa Munich siku 10 tu zilizopita, yanawakumbusha juu ya mpango mbaya wa waziri mkuu wa Uingereza Neville Chamberlain huko Munich mnamo 1938, na kuilazimisha Czechoslovakia kusalimu amri kwa Adolf Hitler.
"Inafanana kabisa," Maxsym alisema. "Magharibi inampa mvamizi fursa ya kumiliki baadhi ya maeneo. Mataifa ya Magharibi yanafanya makubaliano na mvamizi, na Marekani ikiwa katika nafasi ya Uingereza."
"Ni wakati hatari sana kwa ulimwengu mzima, sio tu kwa Ukraine," Maxsym aliendelea. "Tunaweza kuona kwamba Ulaya inaanza kuamka ... lakini kama walitaka kuwa tayari kwa vita, wanapaswa [kuwa] wameanza miaka michache iliyopita."
Dmytro alikubali kuhusu hatari zilizo mbele yake.
"Nadhani Donald Trump anataka kuwa kama Neville Chamberlain… Bw. Trump anapaswa kuzingatia zaidi kuwa kama Winston Churchill."
Athari ya Trump

Chanzo cha picha, Getty Images
Raos Donald Trump wa Mrekani anataka malipo. Alidai dola nusu trilioni za kuwa na haki ya madini kutoka Ukraine. Zelensky alikataa mpango huo, akisema hangeweza kuuza nchi yake. Anataka dhamana ya usalama badala ya makubaliano yoyote.
Kwa faragha, wanasiasa na wanadiplomasia wa Ulaya wanatambua kwamba, pamoja na Joe Biden, waliipa Ukraine msaada wa kijeshi na kifedha wa kutosha kutopoteza kwa Urusi, lakini haijashinda.
Hoja ya zaidi ya hayo ni kwamba Urusi, iliyodhoofishwa na vikwazo na kuondolewa kwa nguvu kazi huku majenerali wake wakifuja maisha ya raia wa nchi hiyo, hatimaye itapoteza vita vya chuki. Huo ni mbali na uhalisia wa mambo ulivyo.
Vita kawaida huisha kwa makubaliano. Kujisalimisha bila masharti kwa Ujerumani mnamo 1945 ilikuwa nadra. Malalamiko dhidi ya Trump ni kwamba hana mpango wenye uhalisia, hivyo amefuata hysia kuwa karibu na Vladimir Putin, mtu anayemvutia.
Trump anaonekana kuamini kuwa viongozi wenye nguvu kutoka mataifa yenye nguvu zaidi wanaweza kuupeleka ulimwengu jinsi wanavyotaka wao.
Makubaliano ambayo Trump tayari ametoa kwa Putin yanaimarisha wazo kwamba kipaumbele chake cha juu ni kurekebisha uhusiano na Urusi.
Kumkabili Putin

Chanzo cha picha, Getty Images
Mpango mzuri ingekuwa ni Pamoja na kujumuisha njia ya kumfanya Putin aondoe mawazo yaliyoko ndani yake ya kijiografia.
Mojawapo ni kwamba uhuru wa Ukraine lazima ufutwe na udhibiti wa nchi kurudi kwa Kremlin, kama ilivyokuwa nyakati za Usvieti na kabla ya hapo katika himaya ya Czars ya Urusi.
Ni vigumu kuona jinsi hiyo itakavyotokea. Wazo hilo ni vigumu kutimizika kama vile Ukraine kusalimisha uhuru wake kwa Moscow. Usalama wa Ulaya unapinduliwa na vita vya Ukraine.












