Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya: Liverpool, Man City zinamtaka Diomande
Liverpool na Manchester City zinamfuatilia kwa karibu winga wa RB Leipzig na Ivory Coast Yan Diomande, mwenye umri wa miaka 19. (Caughtoffside)
Axel Disasi wa Chelsea anawindwa na Lyon, ambao wanapenda kumsajili kwa mkopo beki huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27. (L'Equipe)
Aston Villa wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Strasbourg, M-Argentina mwenye umri wa miaka 23 Joaquin Panichelli, huku Chelsea na West Ham pia wakimfuatilia. (Teamtalk)
Leeds wamewasiliana na Como kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Jamhuri ya Czech mwenye umri wa miaka 23 Martin Baturina, ingawa timu ya Italia inaonekana kusita kumuuza. (Fabrizio Romano via Yorkshire Post)
West Ham na Crystal Palace wanamfuatilia beki wa Lens, Samson Baidoo, mwenye umri wa miaka 21, kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Teamtalk)
Nyota wa Hungary Alex Toth, 20, anayesakwa na Newcastle, anaweza kugharimu karibu pauni milioni 15, lakini kwa kuwa ana mkataba na Ferencvaros hadi 2027, klabu hiyo inaweza kuongeza bei yake. (Chronicle)
Newcastle pia wanatazama nchini Brazil kutafuta vipaji vipya vya vijana wa Amerika Kusini, wakipanga kufanya biashara msimu wa kiangazi mwaka ujao. (ESPN)
Liverpool wanapanga kutoa ofa ya pauni milioni 38 kumsajili beki wa Galatasaray na Ivory Coast Wilfried Singo, mwenye umri wa miaka 24. (Fotomac and Foot-Sur7 via SportWitness)