Mfalme Charles III: Maisha katika picha

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Mrithi aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika ufalme wa Uingereza sasa ni Mfalme. Akiwa na umri wa miaka 73, ni mtu mwenye umri mkubwa zaidi katika historia ya Uingereza kuwahi kuwa mfalme. Hizi ni nyakati muhimu ambazo muhimu katika maisha ya Mfalme King Charles III.

G

Chanzo cha picha, Mirrorpix/Getty Images

Maelezo ya picha, Charles Philip Arthur George alizaliwa 14 Novemba 1948, na alikuwa na miaka mitano na ushee tu wakati mama yake alivishwa taji la Malkia
G

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Alikuwa na umri wa mwaka mmoja tu wakati alipopata uzoefu wa kwanza ambao uligeuka na kuwa msururu wa kutengana na wazazi wake, wakati mama yake aliposafiri kwa ndege kuelekea Malta kuungana na Mwanamfalme Philip ambaye alikuwa bado anahudumu kama afisa wa kikosi cha majini
G

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Charles mdogo mara kwa mara aliachwa chini ya uangalizi wa mhudumu wa chekechea katika nyakati alizotengana na wazazi wake waliosafiri
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Akielemishwa nyumbani hadi alipofikia umri wa miaka minane, Charles alikuwa mrithi wa ufalme wa kwanza kuhudhuria shule - hapa anaonekana akicheza soka mwaka 1957
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alifurahia uhusiano wa karibu sana na bibi yake, mama yake na Malkia
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika hatua ya kumfanya awe mkakamavu, Charles alitumwa kumaliza miaka yake ya masomo katika Gordonstoun, Uskochi, lakini alionewa na kuwaomba wazazi wake aondoke
G

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Kwanza Charles alisomea Akiolojia na Anthropolojia na baadaye alisoma Historia katika Trinity College, Cambridge -alikuwa mrithi wa kwanza katika ufalme kukamilisha kozi ya shahada
G

Chanzo cha picha, Central Press/ Getty Images

Maelezo ya picha, Julai 1969, Charles alitangazwa kama Mwanamfalme wa Wales katika sherehe iliyofanyika katika Kasri la Caernarfon, ambapo alitoa hotuba yake katika lugha zote Kiwelsh na Kiingereza
G

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Alifuata utamaduni wa familia wa huduma kwa jeshi, akiwa rubani mwenye taaluma katika RAF Cranwell kabla ya kuhamia katika chuo cha Royal Naval College at Dartmouth
G

Chanzo cha picha, Central Press/getty Images

Maelezo ya picha, Alifanya mafunzo makali ya kijeshi na kupata cheo cha "Mwanaume wa Kitendo" kwani msururu wa mazoezi ya kijeshi, alijitupa nje ya ndege, alikwepa kutoka katika manowari ya kijeshi na kufunzwa kama dereva na komando
G

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Baada ya kuhudumu katika vyombo mbali mbali vya majini, Charles achukua uongozi wa kusaka machimbo katika HMS Bronington katika muhula wa mwisho katika kikosi cha majini cha Uingereza - Royal Navy
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alivyokaribia kuadhimisha miaka 30 ya kuzaliwa, Mwanamfalme wa Wales alikuja kufahamika kama mtu anayependa anasa.
 Hulton Archive / Getty Images

Chanzo cha picha, Hulton Archive / Getty Images

Maelezo ya picha, Mmoja wa waseja stahiki zaidi, alipigwa picha akicheza polo, akiogelea na kuvinjari katika upepo baharini
G

Chanzo cha picha, Hulton Royals Collection / Getty Images

Maelezo ya picha, Pia alihusishwa kimapenzi na wanawake kadhaa, akiwemo Camilla Parker Bowles
G

Chanzo cha picha, Hulton Archive / Getty Images

Maelezo ya picha, Ingawa kulikuwa na mjadala mwingi wakati huo kuhusu kumtafutia Mwanamfalme "kazi halisi", alifanya ziara za kifalme na alijiuhusisha katika kazi ya msaada, na kuanzisha Wakfu wa Mwanamfalme - Prince's Trust katika mwaka 1976
In 1981, after intense press speculation, it was announced that Charles was engaged to Lady Diana Spencer

Chanzo cha picha, Hulton Archive / Getty Images

Maelezo ya picha, Katika 1981, baada ya tetesi za kila mara za vyombo vya habari, ilitangazwa kwamba Charles alikuwa anamchumbia msichana Lady Diana Spencer
G

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Miezi mitano baadaye walioana katika Kanisa kuu la St Paul - watu wanaokadiriwa kuwa 600,000 walijaa mitaa ya london kushuhudia sehemu tu ya siku yao ya harusi
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanandoa wakipigwa picha kando ya Mto Dee in karibu na Kasri la Balmoral , katika Uskochi, katika siku yao ya mwisho ya fungate
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Licha ya kuwasili kwa watoto wawili, Mwanamfalme, Prince William mwaka 1982 na kaka yake Mwanamfalme Harry mwaka 1984, ndoa yao ilikuwa mashakani na Charles na Diana wakatakiliana rasmi katika mwezi Julai 1996, kwasababu ya "tofauti zisizowezakupatanishwa "
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kufuatia kifo cha ghafla cha Diana katika ajali ya gari mjini Paris katika mwaka 1997, Charles alisisitiza kwamba apewe mazishi ya kifalme
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kifo cha Diana kiliulazimisha ufalme kufikiria upya kuhusu sura yake na Charles alilazimika kujifunza upya mabadiliko, na kujitokeza kama baba mweney kuwajali na kusaidia sana wanawe na kama mrithi wa ufalme wa kisasa
G

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Akishutumiwa kuwa mtu asiyeonekana na asiye na hisia baada ya kifo cha Diana, Charles alijaribu kuonyesha picha mpya na kuchangamana na watu
G

Chanzo cha picha, Tim Graham Photo Library via Getty Images

Maelezo ya picha, Amekuwa mzungumzaji wa wazi kuhusu masuala kadhaa, akielezea uungaji mkono kwa kilimo cha mimea asilia na tiba mbadal, na kuonyesha pingamizi kwa mimea ya GMO
G

Chanzo cha picha, Shutterstock

Maelezo ya picha, Kipindi kigumu cha usanifu majengo wa kisasa, luwaza yake kwa ajili ajili ya mpango wa mji ulifanikiwa katika kwa muudo wa kijiji cha Poundbury, katika Dorset
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, katika mwaka 2002, aliongea kwa huzuni kumuhusu nyanya yake "aliyefanya maajabu" -Mama yake Malkia - ambaye alifariki kwa amani akiwa na umri wa miaka 101 . Alisimama mbele ya jeneza lake wakati jeneza lake lilipokuwa limewekwa kwa ajili ya kutazamwa kwa mwili wake katika Westminster Hall mjini London.
G

Chanzo cha picha, Wireimage / Getty Images

Maelezo ya picha, Kwa mika mingi Charles aliimarisha kuwa uhusiano wake na Camilla Parker Bowles, na wawili hao waloitangaza uchumba wao mwaka 2005, baada ya kukutana mwaka 1970
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Alikuwa mtu wa kwanza katika familia ya Ufalme kufunga ndoa ya kiserikali - Bibi Parker Bowles alikuwa Duchess wa Cornwall, na wakati Charles aliporithi ufalme akawa Malkia consort
G

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Mwaka 2011, mwanaye mkubwa wa kiume, Mwanamfalme William, alimuoa Kate Middleton katika Westminster Abbey
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mjukuu wa kwanza wa Mfalme Mwanamfalme George na Bintimfalme Charlotte walizaliwa 2013 na 2015
G

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mfalme Charles III akimuingiza ndani ya kanisa Meghan Markle dwakati alipoolewa na Mwanamfalme Harry mwaka 2018
G

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Mfalme alionekana amesikitika nyuma yajeneza la Mwanamfalme Philip wakati wa mazishi katika Kasri la Windsor Castle mwaka 2021
G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Charles alikuwa Mfalme wakati mtizamo wa umma kuhusu ufalme unabadilika