'Tulioana miaka 20 baada ya kubadilishiwa wazazi hospitali tukiwa vichanga'

.
Maelezo ya picha, Jim na Margeret walibadilishiwa wazazi wakiwa watoto kabla ya fursa kujitokeza na kuoana miaka 20 baadaye.

Jim na Margeret Mitchell walibadilishwa wakiwa watoto kabla ya kuoana kwa miaka 20 sasa.

Wengine wanaamni kwamba kukutana na mwezi huwa kumeandikwa katika nyota.

Lakini wanandoa hao Jim na Margeret Mitchell wana sababu zaidi ya kuamini kuhusu hatma yao.

Ajali iliyotokea baada ya kuzaliwa iliwaunganisha, kabla ya fursa nyingine karibia miongo miwili kuwaunganisha kwa maisha yao yote.

Wikiendi hii wawili hao wanasheherekea miaka 50 ya ndoa yao na baadhi ya sababu zilizowakutanisha.

Mama yao Jim na Margeret Mitchell waligundua kwamba kulikuwa na kitu tofauti kuhusu watoto wao.

Wote walizaliwa katika hospitali ya Lennox Casttle katika mji wa Lennoztown , kaskazimi mwa Uingereza tarehe 15 mwezi septemba na 17 mwaka 1952.

Nyakati hizo , kitengo cha kujifungulia akina mama kilifanya makosa: Wauguzi waliwakabidhi watoto hao kwa akina mama ambao kila mmoja alimchukua mtoto wa mwenzie

Margeret , ambaye amefikisha umri wa miaka 70 siku ya Alhamisi alisema: Kina mama wote walikuwa wakiitwa Margeret. Hivyobasi kukawa na utata kuhusu wakunga waliowabadilisha watoto hao.

Hili lilitokea muda mfupi kabla ya Watoto kuanza kuvaa bracelet zilizokuwa na majina yao, ijapokuwa akina mama hao waligundua tatizo hilo dakika chache baadaye.

Jim alienda na wazazi wake kuishi Arden, kusini mwa Glasgow, na Margaret akapelekwa nyumbani kwao huko Knightswood, kaskazini-magharibi mwa jiji hilo la Scotland, ambako aliishi na familia yake.

Muda mfupi baadaye, wazazi wa Margaret walinunua nyumba umbali kiasi cha mwendo wa dakika 30 tu kutoka kwa Jim.

Wenzi hao walipofikisha miaka 18, hatima iliingilia tena.

Jim, mhandisi aliyestaafu, alisema: "Rafiki yake alikuwa akioa na alikuwa na wageni nyumbani kwake Queen's Park huko Glasgow."

"Rafiki wa Margaret Pat alimuoa rafiki yangu David. Hapo ndipo tulipokutana kwa mara ya kwanza."

.

Chanzo cha picha, Margeret Mitchell

Maelezo ya picha, Margeret na mamake akiwa mtoto
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Jim alikuwa na nywele ndefu na alikuwa "tofauti" na wavulana ambao Margaret alikuwa amefahamiana nao.

"Tulizungumza kwenye eneo la mapokezi. Nilifikiri alikuwa amependeza akiwa amevalia gauni lake dogo la kupendeza, kwa hivyo nikapata ujasiri wa kumuuliza iwapo tunaweza kuonana."

"Nilifurahi sana kwamba alikubali kwa sababu alikuwa msichana mrembo zaidi."

Baada ya miezi miwili ya kuchumbiana, akina mama hao walianza kushuku kwamba kulikuwa na kitu kisicho cha kawaida.

"Ni mama yake Jim ambaye alikumbuka kipindi hicho hospitalini. Aliweka maelezo tofauti pamoja na kutambua: siku zetu za kuzaliwa zilikuwa karibu sana, jina langu la mwisho lilikuwa Rafferty na baba yangu alikuwa afisa wa polisi," Margaret alieleza.

Mama hao wawili hatimaye walikutana kwa mara ya kwanza tangu kubadilishana watoto katika wodi ya uzazi na kustaajabishwa na mapenzi ya watoto wao.

Jim na Margaret walifunga ndoa mwaka wa 1972 na sasa wanaishi East Kilbride, nje kidogo ya Glasgow. Wamestaafu wakiwa na watoto wawili na wajukuu .

.

Chanzo cha picha, Margeret Mitchell

Maelezo ya picha, Jim alikuwa na nywele ndefu na alikuwa tofauti na wavulana ambao alikuwa akichumbiana nao

Margaret, mtendaji mkuu wa zamani wa mauzo, anaamini kwamba kama haikuwa bahati , huenda asingechagua kuchumbiana na Jim.

"Alikuwa tofauti na wavulana ambao nilikuwa na mahusiano nao. Alikuwa na nywele ndefu sana, lakini alikuwa mkarimu, anayejali na tofauti kabisa," alisema.

Kuanzia siku wakiwa na kifungua kinywa kitandani, walikiambia kipindi cha Good Morning Scotland cha Radio ya BBC siri zao za ndoa ya muda mrefu na yenye furaha.

Margaret alisema, "Ni kuhusu tu kuelewana kila siku inavyokuja."

Jim aliongeza, "Unajua, una heka heka zako, lakini jambo bora zaidi kuhusu kuanguka ni kupenda tena."

.

Chanzo cha picha, Margeret Mitchell

Maelezo ya picha, Jim na Margeret katika harusi yao miaka 50 iliopita