Bezos -Sánchez: Je, hii ndio harusi ya mwaka?

Amazon Founder Jeff Bezos and Lauren Sánchez attend the amfAR gala Cannes 2025 presented by Chopard at Hotel du Cap-Eden-Roc on May 22, 2025 in Cap d'Antibes, France.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 7

Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos na mchumba wake Lauren Sánchez wanatarajiwa kufunga ndoa wiki hii katika sherehe ya kifahari ya siku tatu nchini Italia. Harusi hiyo itakayogharimu mamilioni ya pesa inatazamiwa kuendelea licha ya kukumbwa na utata, yakiwemo maandamano, siku chache kabla ya harusi yao.

Hii itakuwa ndoa ya pili kwa bilionea huyo na mtangazaji mwenza wa zamani kwenye Fox TV na kipindi cha kitaifa cha mazungumzo cha ABC The View.

Wapenzi hao wamekuwa pamoja kwa miaka kadhaa na walichumbiana mnamo Mei 2023.

Amazon founder Jeff Bezos and Lauren Sánchez leave the Aman Venice hotel on Wednesday - Bezos is inside a boat and holding Sánchez's hand as she stands outside the boat

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jeff Bezos na Lauren Sánchez wakiondoka katika mgahawa wa Aman Venice hotel siku ya Jumatano

Maelezo kuhusu harusi hiyo hayajathibitishwa - lakini mpango wa awali uliripotiwa kujumuisha hafla kuu siku ya Jumamosi katika ukumbi wa kifahari wa Scuola Grande della Misericordia, ambao ni ukumbi wa kihistoria katikati mwa jiji.

Hata hivyo, malalamiko ya wananchi kuhusu ubadhirifu na usumbufu uliosababishwa na harusi ya bilionea huyo yanaonekana kuwashinikiza waandalizi kubadili eneo hilo.

Protesters display a banner saying 'No Space for Bezos!' on the Rialto Bridge during a protest on 13 June 2025 against Amazon founder Jeff Bezos's upcoming wedding to Lauren Sánchez being held in the city - picture by Manuel Silvestri

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waandamanaji wakionyesha mabango yanayosomeka 'Hakuna nafasi Bezos! katika daraja la Rialto mjini Venice

"Tunajivunia sana hili! Sisi ni walal hoi, hatuna pesa, hatuna chochote," Tommaso Cacciari, kutoka kundi linalojiita No Space for Bezos, aliambia BBC.

"Sisi ni raia wa kawaida na tuliweza kumhamisha mmoja wa watu wenye nguvu zaidi duniani - mabilionea wote - nje ya jiji."

Jeff Bezos akiwapungia watu mkono akiondoka Aman Venice Juni 25, 2025- Guglielmo Mangiapane

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jeff Bezos akiondoka Mgahawa wa Aman Venice siku ya Jumatatno

Mamlaka ya Jiji na maafiwa wake wamewakosea vikali wanaharakati, wakihoji kuwa hafla za hadi kubwa namna hiyo ni chanzo cha mapato.

"Hawa waandamanaji wanafanya kana kwamba wanalimiliki jiji hili, lakini sio hivyo," Simone Venturini, mshauri wa jiji wa masuala ya maendeleo ya kiuchumi aliiambia BBC. "Hakuna mtu anayepaswa kuamua ni nai atafunga ndoa hapao."

Lauren Sánchez and Jeff Bezos attend the 2024 Vanity Fair Oscar After Party Arrivals at Wallis Annenberg Center for the Performing Arts on 10 March 2024 in Beverly Hills, California.

Chanzo cha picha, Robert Smith / Patrick McMullan via Getty Images

Mwaka huu, Jarida la Forbes lilimuorodhesha Bezos, 61, kama mtu wa nne tajiri zaidi duniani, na kukadiri utajiri wake kuwa dola bilioni 227 za Kimarekani.

Bezoz ni mwanzilishi wa kampuni kubwa ya biashara ya mtandaoni ya Amazon na kampuni ya teknolojia ya Blue Origin.

Wanandoa hao wana watoto saba kwa jumla kutoka kwa uhusiano wao wa awali.

Bezos ana tatoto watatu wa kiume na binti aliyemuasili kutoka kwa ndoa yake na MacKenzie Scott. Wawili hao walitangaza kutalakiana mnamo 2019 kwenye Twitter (sasa X) baada ya miaka 25 pamoja.

Jeff and wife MacKenzie Bezos (now MacKenzie Scott) at the 2018 Vanity Fair Oscar Party in Beverly Hills, California - photo by Danny Moloshok on 4 March 2018

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wakati Jeff Bezos na mtalaka wake MacKenzie

Walifikia makubaliano ya kuwana utajiri wa takribani $35bn. Scott alisalia na asilimia nne ya ya bishara ya Amazon, aliyowa ya thamani ya karibu dola bilioni 35.6 ukiachia mali zingine walizokuwa nazo .

Lauren Sánchez, 55, ni rubani na mwanzilishi wa kampuni ya Black Ops Aviation, Kampuni ya kwanza ya filamu na utayarishaji wa filamu ya anga inayomilikiwa na wanawake na kuendeshwa, kulingana na akaunti ya X ya Blue Origin.

Ana mtoto mmoja wa kiume na mpenzi wake wa zamani, mchezaji wa zamani wa Ligi ya Soka ya Kitaifa (NFL) Tony Gonzalez, na watoto wawili kutoka kwa ndoa yake ya kwanza na Patrick Whitesell, Mkuu mtendaji wa kampuni inayosimamia vyombo vya habari na burudani. Walioana kwa miaka 14.

People work outside Venice's Scuola Grande di Santa Maria della Misericordia while boats are moored and sail in the canal alongside it on 22 June 2025 - picture by Yara Nardi

Chanzo cha picha, Reuters

Ni akina nani wanaandana kupinga harusi?

A large banner against Amazon founder Jeff Bezos lies on the ground, placed by Greenpeace Italy activists and UK activist group Everyone Hates Elon, in St Mark's Square in Venice, Italy, on 23 June 2025.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wnaharakati wanaweka mabango dhidi ya Bezos mjini Venice
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hafla hiyo inayotarajiwa kuhudhuriwa na watu mashuhuri inapingwa na wanaharakati tofauti ikiwa ni pamoja na wenyeji ambao wanalalamikiwa idadi kubwa ya watalii wanaozuru Venice, wengine ni wanaharakati wa kutetea mabadiliko ya hali ya hewa na wale wanaopinga hatua ya Bezos kumuunga mkono Donald Trump.

Wanaharakati huko Venice pia wameanzisha msururu wa maandamano dhidi ya Bezos, huku kukiwa na wasiwasi kwamba sherehe hiyo inaweza kufunga sehemu za mji huo maarufu.

Baadhi ya wenyeji wanaona sherehe hiyo kama ishara nyingine ya unyonyaji unaoendelea wa Venice huku kukiwa na wasiwasi wa utalii kupita kiasi na kupungua kwa idadi ya watu.

Idadi ya wakazi wake ni chini ya 49,000, kinyume na 175,000 mwaka wa 1950.

Wanaharakati wa mazingira Greenpeace wanampinga Bezos ishara ya "mapendeleo na uchafuzi wa mazingira" inayochochea zaidi "pengo la ukosefu wa usawa na athari ya hali ya hewa kati ya matajiri wakubwa na sisi wengine".

Siku ya Jumatatu, wanaharakati kutoka Greenpeace na kundi linalojiita Every Hates Elon walizindua bango kubwa ya Bezos huko Piazza San Marco katika St Marks Square, wakipinga matajiri wakubwa kwa kauli mbiu: "Ikiwa unaweza kukodisha Venice kwa ajili ya harusi yako basi unaweza kulipa kodi zaidi.''

Members of security stand near Madonna dell’Orto church on 25 June 2025, ahead of the expected wedding of Amazon founder Jeff Bezos and Lauren Sánchez - picture by Yara Nardi

Chanzo cha picha, Reuters

Sherehe zinasemekana zitaanza Alhamisi usiku kwa mkusanyiko wa wazi huko Madonna dell'Orto, kanisa la kale katika eneo la Cannaregio, linalojulikana kwa maisha yake ya usiku ya kupendeza.

Ukumbi wa Jiji la Venice ulitoa agizo siku ya Jumatano kuzingira eneo hilo, katika jaribio la kuwatenganisha wageni na wanaharakati ambao wamekuwa wakiandamana kwa wiki kadhaa.

Ni nani aliyealikwa?

Ivanka Trump, daughter of US President Donald Trump, walks with her husband Jared Kushner at Venice airport.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Binti wa Rais wa Marekani Donald Trump, Ivanka Trump, na mume wake Jared Kushner wameonekana katika uwanja wa ndege wa Venice

Takriban wageni 200 wamealikwa. Baadhi wameanza kuwasili kwa ajili ya harusi hiyo, kama vile mwanamitindo Diane von Furstenberg, pamoja na bintiye Donald Trump Ivanka na mkwe Jared Kushner, ambao wameonekana kwenye uwanja wa ndege.

Wageni katika karamu ya Sánchez ya Paris ya bachelorette mnamo Mei walijumuisha nyota wa filamu za uhalisia Kim Kardashian na Kris Jenner, mwimbaji Katy Perry, muigizaji na mtayarishaji Eva Longoria, mfadhili Natasha Poonawalla na mwenyeji wa Fox Sports Charissa Thompson.

Wote wanatarajiwa kuhudhuria.

Wageni wengine mashuhuri wanaodaiwa kuhudhuria ni pamoja na mtangazaji wa TV Oprah Winfrey, mwigizaji wa rock Mick Jagger na muigizaji Leonardo DiCaprio.

(L-R) Kerianne Flynn, Katy Perry, Lauren Sánchez, Aisha Bowe, Gayle King and Amanda Nguyen in front of Blue Origin's New Shepard NS-31 rocket, following a short mission into orbit after taking off from Launch Site One in Van Horn, Texas, on 14 April 2025

Chanzo cha picha, EPA-EFE / REX / Shutterstock

Maelezo ya picha, Muimbaji Katy Perry (wa pili kutoka kushoto) alijiunga na ziara fupi ya Blue Origin anataraji kuwa miongoni mwa wageni waalikwa.

Kulingana na vyombo vya habari vya Italia, karibu hoteli zote za kifahari zimekodishwa kwa ajili ya hafla hiyo.

Ndege za kibinafsi zinatarajiwa kusongamana katika uwanja wa ndege wa Venice, huku meli za kifahari zikitarajiwa kutia nanga bandarini.

Hoteli tano zimekodishwa zote na kunaripoti kuwa wanajeshi wa zamani wa majini wa Marekani wakiajiriwa kutoa ulinzi.

Sherehe za harusi zinatarajiwa kugharimu hadi $55.69m, kulingana na Luca Zaia, rais wa serikali ya mkoa wa Veneto, ambayo inajumuisha Venice.

Kim Kardashian leaves court after testifying in the trial of 10 people accused of stealing millions of dollars worth of jewellery from her when she was allegedly held at gunpoint in her apartment during Paris fashion week in 2016 - photo by Piroschka van de Wouw on 13 May 2025

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kim Kardashian anatarajiwa kuhudhuria harusi hiyo inayotarajiwa kufanyika mjini Venice

Harusi ya Jeff Bezos sio hafla ya kwanza kubwa ya aina hii kufanyika mjini Venice.

Mnamo mwaka wa 2014, muigizaji George Clooney alifunga ndoa na wakili wa haki za binadamu Amal Alamuddin katika harusi ya kupendeza iliyoshuhudia watu mashuhuri wakitua katika jiji hilo la Italia.

Tofauti na harusi ya Bezos, hafla ya Clooney haikukumbwa na ghasia.