Vinicius: "Ligi iliyokuwa ya Ronaldo na Messi leo ni ya wabaguzi wa rangi":

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Vinícius alisema kwamba "Uhispania inafahamika kama nchi ya ubaguzi baada ya nyimbo za matusi kuelekezwa kwake huko Valencia.

Mchezaji wa soka wa Brazil Vinícius Júnior, kutoka Real Madrid, alisema Jumapili hii kwamba "La Liga ni ya wabaguzi wa rangi", baada kushangiliwa kwa nyimbo za kibaguzi huko Valencia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kufanya fujo katika dakika ya 97 ya mchezo baada ya kuzozana na Hugo Duro.

Mapema katika mchezo huo, Vin ícius ambaye alikuwa amekasirika alijaribu kuvuta hisia za mwamuzi, kwa wafuasi wa Valencia na shabiki mmoja.

"Michuano ambayo hapo awali ilikuwa ya Ronaldinho, Ronaldo, Cristiano na Messi, leo ni ya wabaguzi wa rangi," mwanasoka huyo aliandika kwenye Instagram.

"Haikuwa mara ya kwanza, wala ya pili, wala ya tatu. Ubaguzi wa rangi ni jambo la kawaida kwenye La Liga . Laliga inaamini kuwa ni jambo la kawaida, Shirikisho pia na wapinzani wanahimiza," alisema.

"[Hispania ni] taifa zuri, ambalo lilinikaribisha mimi na ambalo lilinipenda, lakini lilikubali kupeleka ulimwengu sura ya nchi ya kibaguzi.

Samahani kwa Wahispania ambao hawakubaliani na hili, lakini leo nchini Brazil, Uhispania inajulikana kama nchi ya wabaguzi wa rangi ," aliendelea.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Majibu ya La Liga

Katika taarifa yake, La Liga ilisema kwamba "imekuwa ikipigana na aina hii ya tabia kwa miaka mingi na kukuza maadili chanya ya michezo, sio tu uwanjani, lakini pia nje ya mchezo."

Pia alidai kwamba aliwasilisha ripoti tisa za ubaguzi wa rangi katika misimu miwili iliyopita kwa mamlaka za kisheria nchini Uhispania.

Rais wa La Liga, Javier Tebas, pia aliitetea taasisi hiyo.

Alisema kuwa amekuwa akikabiliana vikali na ubaguzi wa rangi "kwa ukali wote", kwamba daima huwatambua wahusika na kuwapeleka mbele ya vyombo vinavyotoa adhabu kwa wahusika. "Haijalishi ni wachache kiasi gani, kila mara huwa wanachukuliwa hatua ," alisema.

Alisema kuwa matusi ya kibaguzi yameripotiwa mara 9 msimu huu, 8 kati yake yakielekezwa kwa Vinícius, mmoja wa wachezaji zaidi ya 200 weusi ambao wanashiriki katika ligi za daraja la kwanza na la pili.

Real Madrid imeshutumu "uhalifu wa chuki

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Real Madrid ilitangaza kwamba "imekuwa ikipambana dhidi ya aina hii ya tabia kwa miaka mingi na kuboresha maadii mema ya mchezo2, sio tu uwanjani bali pia nje yake." "uhalifu wa chuki".

Klabu hiyo ilitoa taarifa ambayo " inachukulia kuwa aina hii ya shambulio pia ni uhalifu wa chuki."

Kulingana na sheria ya Uhispania inaweza kupelekea kutolewa kwa faini na vifungo vya jela vya kati ya mwaka 1 na 4 kwa uhalifu huu.

Waendesha mashtaka wa Uhispania sasa wataamua kama wataanzisha uchunguzi wa makosa ya jinai.

Kwa upande wake, Ligi iliapa kuchunguza na kuchukua "hatua stahiki za kisheria" iwapo itabainika kuwa kulikuwa na uhalifu wa chuki, na imewataka watu kuripoti matukio hayo ya ubaguzi.

Wakati huo huo, Valencia alionyesha kwamba polisi "wamemtambua shabiki ambaye alitoa ishara za kibaguzi" na kwamba "klabu pia inashirikiana pamoja na polisi kuthibitisha utambulisho wa wahalifu wengine wowote."

Klabu hiyo ilitangaza kwamba imefungua kesi ya kinidhamu na kwamba " itatoa adhabu kali kwa wahusika, ikiwa ni pamoja na kusimamishwa daima kuingia katika viwanja vya mechi kwa mashabiki wanaohusika."

"Uwanja umekuwa wazimu"

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ancelotti aliikosoa La Liga kwa ubaguzi dhidi ya mchezaji wake

Mshambuliaji huyo Brazil amekuwa akilengwa na matusi ya kibaguzi mara nyingi katika msimu huu wa La Liga.

Mechi ilisitishwa kwa muda katika kipindi cha pili pale mshambuliaji huyo wa Real Madrid alipojibu kwa hasira tukio lililotokea uwanjani dhidi yake.

Wakati huo, alitolewa kwa kadi nyekundu kwa mara ya kwanza kwenye La Liga kwa kuhusika katika ugomvi.

Baada ya mechi mkufunzi wake, Carlo Ancelotti , alisema kuwa hataki kuzungumzia soka bali aelekeze kauli zake kwenye kile kilichotokea kwa mshambuliaji huyo. Alisisitiza kuwa "huwezi kucheza kandanda hivi" na kwamba "njia pekee [ya kukomesha ubaguzi wa rangi] ni kusimamisha mchezo", jambo ambalo alimuuliza mwamuzi.

"Kilichotokea leo kimetokea nyakati nyingine, lakini sio hivi. Haikubaliki," alisema Muitaliano huyo. "Hapa si kwamba mtu amepatwa na kichaa. Hapa uwanja umekuwa wazimu" .

"Ni uwanja ambao unamtukana mchezaji kwa ubaguzi wa rangi, na mechi lazima ikome. Ningesema hivyohivyo tukishinda 3-0, hakuna namna nyingine," aliongeza.

Kocha wa klabu ya Madrid alikiri kuwa Vinícius alihuzunishwa na kilichotokea, lakini akatetea majibu ya Mbrazil huyo uwanjani, akisema kwamba ilikuwa "kawaida" kwa kuzingatia mazingira.

"Ligi ya Uhispania ina tatizo, ambalo si Vinícius. Vinícius ni muathirika wa tatizo kubwa sana,"alithibitisha.

"Kwangu mimi, Vinícius ndiye mchezaji muhimu zaidi duniani, mwenye nguvu zaidi duniani. Ligi ina tatizo, matukio haya ya ubaguzi wa rangi lazima yasimamishe mchezo," Ancelotti alisisitiza.

"Kauli za kusikitisha za Ancelotti"

La Liga ilisema itachunguza tukio hilo, huku Valencia ilichapisha taarifa kwenye tovuti yake ambapo ililaani "aina zote za matusi, mashambulizi au kutostahili katika soka", ikijutia kilichotokea na kuripoti kwamba itachunguza tukio hilo.

"Ingawa hiki ni kipindi cha pekee, matusi kwa mchezaji yeyote kutoka timu pinzani hayana nafasi katika soka na hayaendani na maadili na utambulisho wa Valencia CF. Klabu inachunguza kilichotokea na itachukua hatua kali zaidi. ", alisema.

Hata hivyo, msemaji wa Valencia, Javier Solís, alisema baada ya kumsikiliza kocha wa Real Madrid "mbele ya kauli za Ancelotti za kusikitisha sana , amewataja mashabiki wote wa Mestalla kama wabaguzi wa rangi, ambao klabu haiwezi kuwavumilia."

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vinícius alitolewa nje baada ya kuzozana na Hugo Duro, kutoka Valencia.

‘Kauli za kusikitisha za Ancelotti’

Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva , alijibu kile kilichotokea katika mashindano ya soka ya Uhispania na kutaka hatua zichukuliwe kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika michezo.

"Nataka kueleza mshikamano wangu na Vinícius Júnior, kijana ambaye bila shaka ni mchezaji bora wa Real Madrid, na ambaye anateseka mara kwa mara. Natumai FIFA na vyombo vingine vitachukua hatua kuzuia ubaguzi wa rangi kuchukua nafasi ya soka," aliandika rais huyo Twitter.

Wakati huo huo, Mwingereza Rio Ferdinand, mchezaji wa zamani wa Manchester United, alihoji kutoungwa mkono kwa Vinícius.

“Ndugu, unahitaji ulinzi... ni nani anayemlinda Vinícius Júnior nchini Uhispania?” aliandika kwenye Instagram.

"Je, ni mara ngapi tunahitaji kumuona kijana huyu akifanyiwa hivi? Naona uchungu, naona karaha, naona anahitaji msaada (...) na mamlaka hazimsaidii.

"Watu wanahitaji kuja pamoja na kudai haki zaidi kutoka kwa mamlaka zinazoendesha mchezo wetu," aliongeza.

"Hakuna anayestahiki hili, lakini wanaliruhusu. Kuna haja ya kuwa na mbinu ya umoja kwa hili, vinginevyo litafagiliwa chini ya zulia TENA."

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambulizi wa Real Madrid, Vinícius Júnior akimnyooshea kidole mtu kwenye uwanja kabla ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa tukio lingine.

Mlindalango wa Real Madrid Thibaut Courtois alisema alisikia "sauti za tumbili" karibu dakika ya 20 na akasema angeenda na Vinícius ikiwa mchezaji mwenzake angeamua kuacha kucheza.

"Kama angesema 'naondoka', ningeenda naye, kwa sababu ni jambo ambalo hatuwezi kuvumilia," Courtois alisema.

Rais wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF), Ednaldo Rodrigues, pia alieleza kuchukizwa kwake na tukio hilo.

"Tutaishi hadi lini, katika karne ya 21, vipindi kama vile ambavyo tumeshuhudia, kwa mara nyingine tena, kwenye La Liga?" aliandika katika taarifa iliyotolewa na CBF kwenye Instagram.