'Siogopi kufa': Bingwa wa kwanza wa tenisi aliyetangaza ana Virusi vya Ukimwi

xx

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 6

Mwaka 1988, maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yalianza kwa kuhamasisha ufahamu kuhusu ugonjwa huu ambao umetikisa jamii ulimwenguni. Mwaka huo, mchezaji wa tenisi wa Marekani Arthur Ashe aligundua ameathirika.

Kihistoria unyanyapaa uliomkumba Ashe, akiweka hali yake kuwa siri alianza kuwa mwanaharakati wa kuhamasisha kuhusu ugonjwa huu uliokuwa umezuka.

Mwezi wa Aprili ,1992, Arthur Ashe aliingia ukumbini kuhutubia wanahabari kuhusu kuwa mchezaji wa kwanza wa tenisi mweusi kuchaguliwa kwenye timu ya Davis cup ya Marekani au kuhusu ushindi wake wa awali katika Wimbledon, US Open au Australian Open.

Alikuwa ameweka jina lake katika historia kama mshindi wa kwanza mweusi wa michuano mikubwa, lakini kubanwa na mshtuko wa moyo uliomsababisha kufanyiwa upasuaji mara nyingi, alistaafu kucheza mchezo huo miaka 12 mapema, akiwa na umri wa miaka 36.

Lakini wanahabari walikuwa wana fununu kuhusu hali yake ya afya ,wakati ulimwengu ulikuwa na uwoga kutokana na ugonjwa ambao hauna tiba.

Mwanahabari wa idhaa ya USA Today Doug Smith, rafiki yake wa utotoni ,alimuuliza Ashe kuhusiana na kile alichokuwa amekisikia.

Siku ifuatayo aliamua kuweka bayana kuhusiana na alichoathirika na kile watu wake wa karibu walikuwa wamekiweka siri tangu mwaka 1988: Ni muathiriwa wa Ukimwi.

Aliamini kwamba aliambukizwa ugonjwa huo kutokana na kuongezwa damu mishipani wakati wa upasuaji mwaka wa 1983, miaka miwili kabla ya uchangiaji damu kuchunguzwa virusi vya UKIMWI nchini Marekani.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Habari hizo mbaya zilishtua taifa, lakini zilichukua mkondo mwingine na kuchochea mjadala kuhusu data za kibinafsi na maadili ya vyombo vya habari kutaka kuingilia habari za kibinafsi.

Katika mkutano huo, Ashe alisoma taarifa: "Nina hasira kwamba niliwekwa ... katika nafasi isiyoweza kuepukika ya kulazimika kusema uwongo ikiwa nilitaka kulinda faragha yangu na hakika hakukuwa na hitaji la lazima la kiafya au la kimwili kutangaza hali yangu ya kiafya".

Katika kitabu cha kumbukumbu yake, Days of Grace, Ashe aliandika: "Zaidi ya barua 700 zilifika USA Today kuhusu suala la haki yangu ya faragha, na karibu asilimia 95% walipinga vikali msimamo wa gazeti hilo."

Baadhi ya wanaharakati wa Ukimwi walikosoa hamu ya Ashe ya usiri kuhusu afya yake, kwani walitaka watu mashuhuri kupanua majadiliano zaidi ya lengo la jumuiya ya wapenzi wa jinsi moja LGBT+.

Wengine walihisi kwamba angekuwa msemaji mzuri wa kuhamasisha watu, haswa miongoni mwa watu wa jinsia tofauti na vikundi vya wachache: barua moja ilifikia kusema kwamba Magic Johnson, mchezaji wa NBA ambaye alifichua utambuzi wake wa Ukimwi miezi mitano tu mapema, angeweza kuokolewa. Ashe alizungumza mapema.

Alipoulizwa katika mkutano wa waandishi wa habari kwa nini hakutangaza hadharani mwaka wa 1988, Ashe alisema: "Jibu ni rahisi. Kukubalika kwa maambukizo ya Ukimwi wakati huo sio rahisi na mimi na mke wangu tulitaka ibaki iwe siri ."

Alielezea namna ilikuwa vigumu kumuelezea binti yake wa miaka mitano kuhusiana na kinacho muathiri na ilimbidi mkewe Jeanne awasilishe kwa niaba yake.

Vigezo vya data za kibinafsi

Mhariri wa michezo wa idhaa wa USA Today Gene Policinski hakuwa na shaka kuhusiana na uamuzi wake wa kufanya taarifa hiyo.Alimwambia mwanahabari wa BBC's Tom Brook: "Huyu ni mchezaji mahiri wa karne ya 20.Na jina lake linajulikana ulimwenguni na kufanya hali yake ya afya kuwa ni habari ambazo haziwezi kuepukika."

Na akaongezea kutaja kuwa haoni ni hatia.

Akiwa katika ziara yake Wimbledon,Ashe alieleza kuwa kuna wakati alitamani kutangaza hali yake ya maisha lakini alipoona hali yake ya afya bado ana nguvu akaamua ni bora aendelee na kazi zake bila misukosuko inayoambatana na watu wakijua anachougua haswa unyanyapaa.

Hatimaye, suala la habari za kibinafsi lilisambaa na Ashe aliuliza maswali ya hali ilivyo.

Aliwapa changamoto waandishi wa habari kuchunguza hisia zao, akiuliza, "Je, ni vigezo gani vya habari za kibinafsi? Ni nini? Ni nani anayeviweka? Na vinatolewa kwa mamlaka ya nani? Kwangu, au kwa Mmarekani mwingine yeyote, ni nini kitakatifu na kisichoweza kuepukika?"

Hii ilikuwa mbali na msimamo wa kwanza wa umma Ashe alichukua juu ya suala pana la kijamii. Ingawa ustadi wake wa kimichezo ulimsaidia kuvunja vizuizi vya uwanjani kwa wanariadha weusi, alitumia muda wake mwingi nje ya korti kufanya kampeni ya mabadiliko.

Alizaliwa huko Richmond, Virginia mnamo 1943, alikuwa amejiingiza katika ulimwengu wa michezo na msomaji wa vitabu baada ya mama yake kufariki akiwa na umri wa miaka sita tu. "Udhibiti ni muhimu sana kwangu," aliiambia Redgrave. "Unakua mweusi huko Amerika kusini mwishoni mwa miaka ya 1940 na 1950, huna udhibiti. Sheria za ubaguzi wa wazungu zinakuambia wapi kwenda shule, basi unaweza kupanda, wapi unaweza kupanda basi, teksi gani. kuchukua, kile unachoweza kusema maisha yako yamezingirwa na marufuku tele.

Lakini Ashe hakutaka kuwa mwanaharakati wa kuhamasisha kuhusu ugonjwa wa Ukimwi alipendelea kujikita zaidi kwenye tenisi, licha ya wito wa kumtaka atumie nafasi yake ya umma kuendeleza harakati za kutetea haki za raia.

Ilisababisha baadhi ya watu kumshutumu kuwa "Uncle Tom", au mtu ambaye ni mshiriki katika ukandamizaji wa asili. Lakini baada ya miaka mingi ya kudhibitiwa na mfumo wa ubaguzi wa rangi, Ashe hakuhisi kukombolewa na haki za kiraia za miaka ya 1960. Aliambia BBC kwamba alikuwa na "wana itikadi weusi wanaojaribu kuniambia la kufanya", na kuongeza: "Wakati wote, ninajiambia, 'Hey ni lini nitapata kuamua ninachotaka kufanya?' Kwa hivyo nimekuwa nikilinda vikali, na mtu yeyote, kwa kutaka kwangu kufanya na kudhibiti maisha yangu kama nilivyoona inafaa."

Alipoulizwa kuhusu mlipuko wa hadharani wa nyota mwenzake wa tenisi, John McEnroe, Ashe alisema: "McEnroe alikuwa na uhuru wa kihisia kuwa kijana mchachari. Sikuwahi kuwa na uhuru huo wa kihisia. Ikiwa ningekuwa hivyo, nina hakika, tenisi. ulimwengu ungenitoa ndani yake ... kwa sababu ya rangi yangu."

Hatimaye, Ashe alihitaji kufanya mambo kwa njia yake mwenyewe, na alitumia nafasi yake kama mchezaji wa michezo wa kiwango cha dunia kuhamasisha masuala kadhaa. Wakati wa kilele cha taaluma yake, alikabiliana na utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini kwa miaka mingi, na mwaka 1973, alisafiri kwenda mashindano ya Tenisi ya Afrika Kusini kwa makubaliano kwamba mashindano hayo yangekuwa na ushirikiano wa watu wa rangi zote. mbali na mwangaza wa vyombo vya habari duniani, pia alijitolea kufadhili kituo cha tenisi kwa Waafrika Weusi wa Afrika Kusini huko Soweto.

Ashe alijisikia kwa namna ya kipekee kuhusu ushiriki wa watu wa rangi zote katika tenisi hapa nyumbani. Kama mwanzilishi mwenza wa Ligi ya Tenisi ya Watoto ya Taifa mwaka 1969, lengo lake lilikuwa kuhakikisha kwamba watoto wa asili mbalimbali wanapata fursa ya kucheza tenisi, na sio tu wale wenye uanachama wa vilabu vya nchi.

Na ingawa alianza kwa uoga katika kushiriki kwake, kwa muda Ashe alikuja kuwa sauti moja ya nguvu zaidi katika mapambano ya haki na usawa nchini Marekani. Katika filamu ya Citizen Ashe, kiongozi wa haki za raia na mchezaji muhimu 1968 Mexico Olympics black power protests, Dkt. Harry Edwards, alisema kuhusu nyota huyo wa tenisi, “Unapotoa mbali ustaarabu, upole, akili, na utulivu, tamko lake lingekuwa lenye msimamo mkali kuliko langu.”

Baada ya Ashe kupata mshtuko wa moyo mara kadhaa, alijiunga na bodi ya Shirika la Moyo la Marekani. Na baada ya kufichua kuwa alikuwa na ugonjwa wa UKIMWI, haikuwa ajabu wakati kampeni mpya ilianza.

Mbali na kutokea kwenye vyombo vya habari akiondoa dhana potofu kuhusu ugonjwa huo, alianzisha wakfu wa Arthur Ashe kwa ajili ya Kukabiliana na ungojwa wa UKIMWI. Katika Siku ya Dunia ya UKIMWI ya Disemba 1992, alizungumza na Shirika la Afya Duniani.

Ashe alifariki mwezi Februari 1993 kutokana na kichomi iliyosababishwa na UKIMWI, miaka miwili kabla ya aina mpya ya dawa za kupunguza makali ya ukimwi (ARVs) kuanza kupatikana ambazo zingewawezesha watu waliokuwa na virusi kuishi maisha marefu na yenye afya.

Alimwambia Redgrave mwaka 1992: “Sijali kufa. Kila wakati kuna matumaini na lazima uishi maisha yako kana kwamba kuna matumaini, au kutakuwa na matumaini. Matumaini hayapaswi kuwa matumaini ya ubinafsi. Kwangu mimi, matumaini ni, labda hakuna tiba ya UKIMWI kwa wakati wangu, lakini kwa hakika kwa wengine wote.”

Imetafsiriwa na Maryam Mjahid na kuhaririwa na Seif Abdalla