Naomi Osaka: Mchezaji nambari mbili duniani aliwashangaza wengi kwa kujiondoa mashindanoni

Chanzo cha picha, Getty Images
Bingwa namba mbili duniani katika mchezo wa tenisi upadne wa wanawake Naomi Osaka amejiondoa kwenye michuano ya wazi ya Ufaransa (French Open)
Katika mtandao wa Twitter akitangaza hatua hiyo, Osaka ambaye ni raia wa Japan pia alisema "amesumbuliwa na msongo wa mawazo" tangu kushinda taji lake la kwanza la Grand Slam mnamo 2018.
Osaka mwenye umri wa miaka 23 alisema wiki iliyopita hatazungumza na vyombo vya habari kulinda afya yake ya akili.
''Sikutaka kuwa kikwazo,'' mshindi huyo mara nne alisema
Siku ya Jumapili, Osaka alishinda mechi yake ya ufunguzi dhidi ya mchezaji kutoka Romania Patricia Maria Tig na kupigwa faini ya dola 15,000 kwa kutozungumza na vyombo vya habari baada ya mechi.
Baada ya muda taarifa ya pamoja ya waandaaji wa michuano ya Grand Slam walisema Osaka anaweza kuondolewa kwenye michuano hiyo akiendelea kuwakwepa wanahabari.
Hatua hiyo ilimfanya Osaka kutangaza kujiondoa siku ya Jumatatu, akisema ''atakuwa nje ya uwanja kwa muda''.
''Muda mwafaka ukifika ninataka kufanya kujadili namna ya kuweka mazingira mazuri kwa wachezaji, vyombo vya habari na mashabii,'' aliongeza.
Shirikisho la mchezo wa Tenisi Ufaransa Gilles Moretton alisema kujiondoa kwake ni jambo la ''bahati mbaya''
''Tunasema pola na tunamsikitikia Naomi,'' Moretton aliongeza. '' Tunamtakia afya njema ya haraka, na tunatarajia kuwa na Naomi katika michuano ya mwakani.
"Kama Grand Slams zote, WTA, ATP na ITF, tunabaki kujitolea sana kwa ustawi wa wanariadha wote na kuendelea kuboresha kila hali ya uzoefu wa wachezaji kwenye mashindano yetu, pamoja na vyombo vya habari, kama ambavyo tumekuwa tukijitahidi kila mara kufanya. "
Ni hali ambayo sikuifikiria - Taarifa ya Osaka
"Hii sio hali ambayo niliwahi kufikiria au kukusudia wakati nilipochapisha siku chache zilizopita. Nadhani sasa jambo bora zaidi kwa mashindano, wachezaji wengine na ustawi wangu ni kwamba ninajiondoa ili kila mtu arejee kuzingatia tenisi ikiendelea huko Paris.
"Sikutaka kuwa kikwazo na ninakubali muda wangu haukuwa muafaka na ujumbe wangu ungekuwa wazi zaidi. Muhimu zaidi, sitawahi kudharau afya ya akili au kutumia neno hilo kirahisi rahisi.
"Ukweli ni kwamba nimepata shida nyingi za msongo tangu US Open mnamo 2018 na nimekuwa na wakati mgumu sana kukabiliana na hilo.
"Mtu yeyote ambaye ananijua na mtu yeyote ambaye ameniona kwenye mashindano atagundua kuwa mara nyingi nimevaa headphones kwani hiyo inasaidia kupunguza wasiwasi wangu mbele ya watu
"Ingawa tenisi imekuwa ikinipendeza kila wakati (na ninataka kuomba radhi kwa waandishi wote wa habari nimewaumiza), mimi kwa kawaida sio mzungumzaji wa kwa umma na nina wasiwasi mwingi kabla ya kuzungumza na vyombo vya habari vya ulimwengu.
''Ninapata wasiwasi mara zote ninapofikiri kutoa majibu mazuri niwezavyo.
"Kwa hivyo hapa Paris nilikuwa tayari nikihisi hatari na wasiwasi, kwa hivyo nilifikiri ni bora kukwepa mikutano ya waandishi wa habari. Nilitangaza mapema kwa sababu nahisi kama sheria zimepitwa na wakati katika sehemu kadhaa na nilitaka kuonesha hilo.
''Niliandika binafsi kuomba kwa radhi kwa waratibu wa michuano kuomba radhi na kusema kuwa nitakuwa na furaha zaidi kuzungumza nao baada ya michuano.
Nyota wa michezo wamemuunga mkono Osaka
Martina Navratilova: "Nina huzuni sana juu ya Naomi Osaka. Natumai kweli atakuwa sawa. Kama wanariadha tumefundishwa kutunza miili yetu, na labda hali ya akili na hisia. Hii ni juu ya zaidi ya kufanya au kutofanya Mkutano wa waandishi wa habari. Kila la heri Naomi - sisi sote tunakuunga mkono "
Stephen Curry, Mcheza kikapu wa Kimarekani: "Haupaswi kamwe kufanya uamuzi kama huu. Kwa hivyo inavutia kuchukua njia nzuri wakati mamlaka hailindi kilicho chao wenyewe. Heshima heshima kwa hilo!."
Wanamichezo wa tenis na nje ya mchezo huo, wamepongeza msimamo wa Osaka baada ya kuutangaza siku ya Jumatano, ingawa wengi walisema kuzungumza na wanahabari ni ''sehemu ya majukumu.''
Sheria za Grand Slam zinasema kuwa mchezaji atatozwa faini ya mpaka dola 20,000 kwa kushindwa kuzungumza na wanahabari, huku shirikisho la mchezo huo kwa wanawake (WTA) likisema kuwa wachezaji ''wana jukumu kwa mchezo huo na mashabiki wa mchezo'' kuzungumza na wanahabari wakati wa michuano.












