Je ni silaha gani ambazo dunia inanazitoa kwa Ukraine?

Tangu mwanzo wa vita vya Ukraine, Kyiv imekuwa ikipewa zana za kijeshi huku sehemu kubwa ya vifaa vingi vya kijeshi vikitolewa na nchi zaidi ya 30

 Marekani imetangaza usaidizi mpya wenye thamani ya dola bilioni 2.5 (£2bn) wiki hii, vikiwemo vifaru vya kijeshi, lakini hakuna ombi lililotolewa na Ukraine la vifaru vikuu vya mapigano.

Uingereza imesema kuwa itatuma vifaru aina ya Challenger 2 kusaidia katika juhudi za vita nchini Ukraine na Berline inakabiliwa na miito inayoitaka iruhusu vifaru vya kivita vyeney nguvu zaidi vinavyotengenezwa -Leopard 2 vipelekwe Ukraine.

Mahitaji ya Ukraine yamebadilika pakubwa huku vita vikiendelea

Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky anasema kwamba vikosi vyake vinahitaji vifarui vikuu vya magharibi haraka, ili kujikinga dhidi ya mashambulio ya Urusi, na kuwasukuma wanajeshi wa Urusi nje ya maeneo yaliyovamiwa.

Baadhi ya maafisa wa Magharibi yanaamini pia kwamba vikosi vya Urusi kwa sasa viko katika hali dhaifu, na kwamba kuna kipindi cha fursa kwamba vifaru vya kisasa vinaweza kuisaidia Ukraine kusonga mbele.

Uingereza imekubali kutoa vifaru 14 vya aina ya Challenger 2 kwa Ukraine.

 Challenger 2 ni vifaru vikuu vya vita vya jeshi la Uingereza.

Kifaru cha Challenger 2 kilitengenezwa katika miaka ya 1990, lakini ni vya kisasa zaidi kuliko vifaru vinavyopatikana kwa sasa katika jeshi la Ukraine.

 Ukraine ilitumia mkataba wa Warsaw Pact kusaini matumizi ya vifaru vya T-72 kabla ya uvamizi, na tangu Februari 2022 imekwishapokea zaidi ya vifaru aina ya T-72 200 kutoka Poland, Jamuhuri ya Czech na idadi ndogo kutoka nchi kadhaa.

Katika mwezi uliofuatia uvamizi, mataifa ya Magharibi yalikuwa makini kutoa Ukraine mkataba wa Warsaw kuliko viwango vya silaha vya Nato, kwasababu vikosi vya Ukraine tayari vilikuwa vimepewa wakufunzi, vipuli na uwezo wa ukarabati wa silaha hizo.

Kubadilisha na kutumia vifaru vyenye viwango vya Nato kungehitaji usaidizi mkubwa kwa Ukraine ambao Ukraine haikuwa nanavyo.

Sasa, Ukraine inataka vifaru vya Ujerumani Leopard 2, vilivyotumiwa na nchi za Ulaya.

Ujerumani imekuwa ikikabiliwa na shikikizo la kutoa msaada wa vifaru vya Leopard 2, lakini haijafanya hivyo na la muhimu zaidi bado haijatoa ruhusa yake kwa nchi nyingine zenye Leopard 2 kuipatia Ukraine. Vifaru vya kivita vya Leopard 2 ni rahisi zaidi kuvitunza na huhitaji mafuta kidogo kuliko vie vinavyopatikana katika baadhi ya mataifa mengine ya Magharibi.

Ripoti zinasema kuwa Ujerumani haitabadilisha msimamo wake kuhusu vifaru vyake vya Leopard 2 mpaka Marekani itume vifaru vyake vikuu vya Abrams.

Marekani ndio mdhamini kubwa zaidi katika vita vya Ukraine kwa ujumla.

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa hawako tayari kwa hili. "Vifaru vya Abrams ni zana ngumu sana za kivita. Ni ghali. Ni vugumu sana kuzifanyia mazoezi. Vina injini ya jet ," kulingana na mshauri wa ngazi ya juu wa masuala ya usalama katika Pentagon Colin Kahl.

'Magari ya vita'

Wasomi wa masuala ya kivita wanaelezea kwamba mafanikio ya mapambano ya vita yanahitaji vifaa mbali mbali vya kuivita, vinavyosambazwa kwa utratibu , huku kukiwa na usaidizi wa ukarabati wa vifaa katika maeneo ya vita.

Miongoni mwa magari ya kijeshi yaliyotolewa na Marekani kwa Ukraine ni magari ya vita aina ya Stryker .

Alhamisi, Marekani ilitangaza kuwa inasafirisha Strykers 90.