Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ukraine yachangisha pesa kwa ajili ya meli za kamikaze. Je zina uwezo gani ?
Ukraine imeanza kuchanghisha fedha kwa ajili ya kutengeneza meli kubwa zaidi na ya kwanza yenye boti, yenye uwezo pia kuwa kutumiwa na ndege za kivita kufanya mashambulizi, Rais Volodymyr Zelensky amesema katika chaneli yake rasmi ya Telegram.
Bw Zelensky amesema kuwa, Ukraine inahitaji droni kwa ajili ya "kulinda maji ya bahari zetu na kuiweka miji yetu katika hali ya amani dhidi ya makombora ya Urusi yanayopigwa kutoka kweney meli ."
Kulingana naye, wanajeshi wa Ukraine watatumia boti hizo kufungua njia kwa ajili ya meli za usafiri wa abiria na nafaka kutoka kwenye bandari za Ukraine.
UNITED24 ni mradi ulioandaliwa na maafisa wa Ukraine ili kuchangisha fedha za kuisaidia nchi hiyo. Wavuti wa mhradi huo unasema mradi huo ulianzishwa na Rais Volodymyr Zelensky.
Ni silaha za kujitegemea
Wavuti wa mradi wa UNITED24 ulichapisha taarifa kuhusu uwezo na sifa za droni za kamikaze. Tunazungumzia kuhusu kifaa kidogo chenye uwezo wa kupiga Enei lililolengwa kwa kujilipua chenyewe. Kifaa cha aina hiyo mara kwa mara huitwa "kamikaze".
Urefu wa meli hizi ni mita 5.5 , masafa - kilomita 800, kasi ya kufika eneo lililolengwa - kilomita 80 kwa saa, uzito kifuniko kinacholipuka - kilogramu 200.
Kwa kulinganisha, ukubwa wa kifuniko cha vilipuzi cha kombora la Harpoon ni kilogramu 225. Kifuniko cha kombora la Ukraine linaloongozwa - Neptune cruise kina uzito wa kilo 150.
Kwa kuangalia sifa ya utendaji, droni hudhibitiwa kwa kutumia sehemu tatu za video. Hali kadhalika, ina ifaa ambavyo vinaiunganisha na mfumo wa setilaiti - autopilot.
Kulingana na taarifa iliyochapishwa na Ukraine, droni zitaweza kufanya upelelezi, ujasusi, kusindikiza meli za kikosi cha majini, kulinda meli za biashara, na kulinda mwambao dhidi ya makundi yenye hujuma.
Uvamizi wa Sevastopol
Jinsi droni hizi zilivyoonekana kwenye video , zinafanana na ile ambayo wanablogi wa Urusi wa najeshi waliyodai mwezi wa Septemba ilisombwa hadi ufukweni karibu na eneo la Sevastopol
Hakuna aliyebaini ni nani aliyekuwa mmiliki wake.
Aidha picha ambayo ilionekana kwenye mtandao baada ya mashambulizi dhidi ya meli za Urusi kwenye meli ya Bahari nyeusi ya Urusi, kwenye njia ya Sevastopol Oktoba 29, 2022 ilitumiwa katika wavuti wa kuchangisha fedha kuonyesha kile kinachopweza kufanywa na silaha hiyo.
Huku Waziri wa ulinzi wa Urusi akikiri kwamba ni meli ya Ivan Golubets pekee iliyoharibika, kwa kuzingatia rekodi za video , baadhi ya wataalamu wanasema hatahivyo kwamba maboti pia yalishambulia meli ya Admiral Grigorovich- ya meli ya bahari nyeusi, iliyokuwa imesheheni makombora ya Caliber.
Ukraine bado Ukraine haijathibitisha uhusika wa vyombo vyake vya majini katika mashambulio hay ana bado haijathibitisha kuhusu kuonekana kwa boti yake katika mwambao wa Crimea.
Je ni Ukraine inatengeneza silaha hizi za majini au ni msaada kwa washirika wake?
Kulingana na wavuti wa Ukraine, vifaa hivyo ni "vya kipekee vinavyotengenezwa na Ukraine ." Katika kuthibitisha maneno haya, video inaonyesha mchakato wa utengenzwaji wa vifaa hivi – ukataji wa vyuma, kuunganishwa na uwekwaji wa mifumo ya kielekroniki.
Hatahivyo, hakuna maelezo ya mradi huu yaliyotolewa.
Wakayti huo huo, mwezi Mei 2022, moja ya orodha za usaidizi wa kijeshi kwa Ukraine ilijumuisha "maboti yanayojiendesha ya walinzi wa mwambao." Aina ya maboti hayo na namba zake havikuelezwa.
Kulingana na vyyanzo vya wazi, nchini Marekani, aina kadhaa za meli zisizokuwa na wahudumu zinatengenezwa. Miongoni mwake ni droni za majini zinazowe kujiendesha LUSV, MUSV na XLUUV.
Hatahivyo, zote hizi zinatofautiana na droni za kamikaze, ambazi ni maboti ya Ukraine.
Droni za majini
Katika miaka ya hivi karibuni, Ukraine imekuwa ikitumia mifumo inayojiendesha ya anga katika vikosi vyake vya anga na majini, lakini hili lilidhihirika kwa mara ya kwanza katika vikosi vyake vya anga - ambapo zaidi iliangaliwa mifumo yake ya Bayraktar TB2 -droni zinazopaa.
Hatahivto, kama alivyosema kamanda wa kikosi cha wanamaji wa Ukraine ,Rear Admiral Oleksiy Neizhpapa, mwezi mei 2021, ilipangwa kuziwezesha meli zisizokuwa na rubani za majini kwa uwezo zaidi. Alizungumzia hili , alipokuwa akiwasilisha wazo la kla utengenezwaji wa meli hizi kwa vikosi vya kwenye jukwa la "Ukraine 30. Usalama wa nchi ."
Je droni za majini zinaweza kuwa na ufanisi kiasi gani
Ufanisi wa zana kama hizo dhidi ya meli za kivita unaweza kuwa hali ya juu kuliko ule wa zile ambazo hutumiwa kwa mapigano, kwa mfano , wakati wa Vita kuu ya pili ya dunia.
Meli za kisasa zina ulinzi wa kiwango kidogo dhidi ya silaha kama vile – makombora, bunduki na mabomu. Inakuwa vigumu kuipiga meli ya mapigano ya zamani kwa droni ya baharinbi kuliko ilivyo kwa meli za kisasa.
Ukweli ni kwamba wakati wa Vita kuu ya II ya dunia, mifumo muhimu ambayo ilihakikisha kunusurika kwa meli ilikuwa ni ile iliyokuwa huru. Kwa mfano, mtambo wa nishati, mitambo iliyosafirisha makombora na vituo vya kuongoza mapigano vilikuwa muhimu na vililindwa zaidi.
Na zaidi ya hayo, kutokana na uwezo wa kujiendesha, kushindwa , kwa mfano kwa bunduki moja hakukuifanya ishindwe kutekeleza mashambulizi kama ilivyopangwa. Kupigwa katika sehemu moja kusingeizuia, kungeifanya isalie kuwa na uwezo wa kupigana.
Ni vigumu kwa meli ya kisasa kutekeleza kazi iliyopangwa, kwani kila upande wake huwa ni muhimu katika utendaji, kupoteza kwa kiungo chake kunaweza kuizuia kuwa na uwezo wa mapigano. Haiwezekani kusafirisha meli nzima ya kisasa kutokana na na uzani wake.