Mpaka hatari zaidi duniani kati ya nchi mbili

Chanzo cha picha, AFP
Kuishi kwenye mpaka nyeti unaojulikana kama LoC, kunamaanisha kuishi katikati ya amani tete na ukingo wa vita. Huu ni mpaka hatari kati ya India na Pakistan.
Baada ya shambulio la hivi karibuni huko Polgam, Kashmir, nchi hizo mbili kwa mara nyingine tena zimefikia ukingo wa mzozo. Katika pande zote mbili, mashambulizi yalifanyika kwenye Laini ya Udhibiti; Hii iliharibu nyumba na kuua watu.
Inaripotiwa kuwa angalau watu 16 waliuawa upande wa India, huku Pakistan ikidai raia 40. Haiko wazi ni wangapi walikufa moja kwa moja kutokana na shambulio hilo.
Anam Zakaria, mwandishi wa Pakistani nchini Canada, aliiambia BBC: "Familia huko LoC ziko hatarini kutokana na mvutano mkubwa kati ya India na Pakistan. Kila mara mapigano yanapoanza tena, wengi hukimbilia kambi, mifugo na maisha hupotea, miundombinu nyumba, hospitali, shule huharibiwa.
Hali ya hatari na ukosefu wa usalama una madhara makubwa kwa uhalisia wao wa kila siku."
Mpaka baina ya India na Pakistan una urefu wa kilomita 3,323. Hii inajumuisha sehemu maalumu ama mstari wa udhibiti yenye urefu wa kilomita 740. Pia wana mpaka wa kimataifa (IB) wenye takriban kilomita 2,400. LoC iliitwa hivyo baada ya vita vya kwanza vya India na Pakistan, mnamo 1949 kuweka mstari maalumu wa kusitisha mapigano chini ya Mkataba wa Simla uliotiwa saini mwaka 1972. Mstari ama 'laini' inayopita Kashmir, inayodhibitiwa kikamilifu na kwa kiasi na nchi zote mbili, inabaki kuwa moja ya mipaka hatari na yenye ulinzi mkali zaidi duniani.
Migogoro haijawahi kutoweka katika eneo hilo; kusitisha mapigano hudumu tu hadi pale mzozo unaofuata utokee. Ukiukaji wa kusitisha mapigano unaweza kuanzia "mapigano ya kiwango cha chini hadi uvamizi na unyakuzi mkubwa wa ardhi na mashambulizi makubwa," alisema Hapimon Jacob, mtaalamu wa sera za kigeni katika Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru mjini Delhi (JNU).
Unyakuzi wa ardhi unaweza kujumuisha kukaliwa kwa nguvu kwa maeneo muhimu, kama vile vilele vya milima, vituo kadhaa, au maeneo ya kinga.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mpaka baina ya India na Pakistan una urefu wa kilomita 3,323. Hii inajumuisha sehemu maalumu ama mstari wa udhibiti yenye urefu wa kilomita 740. Pia wana mpaka wa kimataifa (IB) wenye takriban kilomita 2,400. LoC iliitwa hivyo baada ya vita vya kwanza vya India na Pakistan, mnamo 1949 kuweka mstari maalumu wa kusitisha mapigano chini ya Mkataba wa Simla uliotiwa saini mwaka 1972. Mstari ama 'laini' inayopita Kashmir, inayodhibitiwa kikamilifu na kwa kiasi na nchi zote mbili, inabaki kuwa moja ya mipaka hatari na yenye ulinzi mkali zaidi duniani.
Migogoro haijawahi kutoweka katika eneo hilo; kusitisha mapigano hudumu tu hadi pale mzozo unaofuata utokee. Ukiukaji wa kusitisha mapigano unaweza kuanzia "mapigano ya kiwango cha chini hadi uvamizi na unyakuzi mkubwa wa ardhi na mashambulizi makubwa," alisema Hapimon Jacob, mtaalamu wa sera za kigeni katika Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru mjini Delhi (JNU).
Unyakuzi wa ardhi unaweza kujumuisha kukaliwa kwa nguvu kwa maeneo muhimu, kama vile vilele vya milima, vituo kadhaa, au maeneo ya kinga.

Chanzo cha picha, AFP
Kulingana na wataalamu wengi, LoC ni mfano wa "mpaka uliopatikana kwa damu na ulioundwa na mzozo." Na kama mwandishi Zakaria anavyosema, "ulitengenezwa na India na Pakistan, na kuzingirwa na silaha bila kuzingatia Wakashmiri,".
Vita vya mpakani kama hivyo si jambo geni Kusini mwa Asia. Sumantra Bose, profesa wa siasa za kimataifa kutoka London School of Economics, anasema kwamba kinachojulikana zaidi kama 'Green Line', eneo la kusitisha mapigano ya mwaka 1949 ndiyo mpaka kati ya Israel na Ukingo wa Magharibi.
Na utulivu wa muda mfupi baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwaka 2021 kati ya majirani hao wawili wenye silaha za nyuklia, haishangazi, umeporomoka kwa urahisi baada ya uhasama wa hivi karibuni.
"Maendeleo ya sasa katika mipaka ya ndani na mipaka ya Kimataifa (IB) ni muhimu kwani kumekuwa na miaka minne ya amani kiasi mpakani," alisema Surya Valliapan Krishna, mtaalamu katika Taasisi ya Carnegie India ya uchambuzi wa changamoto nchini India.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kutokuwa na uhakika wa hali hiyo kunaongezeka katika eneo hilo la mpaka. Kwa upande wake, Jacob anasema kwamba kwa "sababu isiyo ya kawaida" ukiukaji wa kusitisha mapigano karibu na LoC haujaingia kwenye majadiliano na mijadala kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa mzozo kati ya nchi hizo mbili. Katika kitabu chake, Line on Fire: Ceasefire, Jacob anajadili jinsi "nchi mbili zenye uwezo wa nyuklia na matumizi ya silaha za hali ya juu kama vile mizinga ya milimita 105, mizinga ya milimita 130 na 155, na makombora yanayoelekezwa ya kupambana na vifaru ambayo husababisha vifo vya raia na wanajeshi," Anaandika Jacob.
India mara nyingi hutumia kisingizio cha ulinzi kuingiza wanamgambo Kashmir inayodhibitiwa na India, ambayo imeshuhudia zaidi ya miaka 30 ya uasi wa kutumia silaha dhidi ya uvamizi wa India. Pakistan, kwa upande wake, inaishutumu India kwa kufyatua risasi kiholela kwenye maeneo ya raia. Inabishana kuwa ukiukaji wa kusitisha mapigano kwenye mpaka wa India na Pakistan ni matokeo ya ukosefu wa mkakati wa kisiasa wa kiwango cha juu pamoja na ujanja wa kijeshi wa ndani.
Uhasama mara nyingi huanzishwa na makamanda walio mtari wa mbele ama kwa idhini toka juu ama bila idhini
Baadhi ya wataalamu wanaamini ni wakati wa kurejea wazo lililowekwa kando karibu miaka 20 iliyopita: kugeuza LoC kuwa mpaka rasmi, unaotambulika kimataifa. Wengine wanasema uwezekano huo haujawahi kuwa wa kweli. "Wazo hilo haliwezekani kabisa, ni njia iliyofungwa. Kwa miongo kadhaa, ramani za India zimeonyesha eneo lote la jimbo la zamani la Jammu na Kashmir kama sehemu ya India," Sumantra Bose aliiambia BBC.
"Kwa Pakistan, kufanya LoC kuwa sehemu ya mpaka wa kimataifa kunamaanisha kusuluhisha mzozo wa Kashmir, kwa masharti ya India. Kila serikali na kiongozi wa Pakistani, wa kiraia au wa kijeshi, amekataa hili katika miaka 70 iliyopita," alisema.
Kwa wale walio katika eneo hilo, ilileta mzunguko mwingine wa vurugu na kutokuwa na uhakika wa usalama wao. "Huwezi kujua nini kitatokea baadaye. Hakuna anayetaka kulala kuelekea katika eneo hili usiku wa leo," mfanyakazi wa hoteli huko Kashmir inayodhibitiwa na Pakistan aliiambia BBC.