Jinsi wanawake wanavyoathirika mahali pa kazi

    • Author, Megha Mohan
    • Nafasi, Gender and Identity Correspondent
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Faith, mwenye umri wa miaka 24, alikuwa katika mkutano ofisini mahala anapofanyia kazi katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, na alikuwa na wasiwasi. Mkutano ulikuwa umeanza vizuri. Lakini pale Faith alipochekwa kutokana na utani mbaya uliofanywa na wakubwa wake mambo yalianza kubadilika haraka

Mwenzake mwandamizi alitoa pendekezo ambalo Faith alihisi halingeweza kutekelezeka kwa vitendo. Lakini kabla ya Faith kutoa maoni yake, mwenzake alitaja jina lake.

"Na Imani unakubaliana nami!" Washiriki wengine katika chumba cha mkutano waligeuka kumkabili Faith wakati mwenzake aliongeza, "Unakubali, sivyo?"

Faith hakukubali, lakini alihisi kushinikizwa.

"Sikutaka kuonekana kuwa mgumu au wa hali ya juu," Faith ananiambia. "Nilihisi shinikizo la kutabasamu bila kutaka, kukubaliana, ili kutokuwa na usumbufu."

Anasimama kutafakari mahali alipokuwa wakati huo. Miaka miwili tu katika kazi yake ya kwanza katika kampuni inayotafutwa na kati ya wanawake wa kwanza katika kizazi cha familia yake kwenda chuo kikuu, alikuwa na mengi zaidi aliyotaka kufikia.

"Nitaendeleaje ikiwa nitaanza kutokubaliana na wenzangu katika hatua ndogo kama hiyo?" anauliza.

Faith anafahamu kuwa Kenya tayari inakabiliwa na kile ambacho ripoti ya Wanawake katika maeneo ya kazi (Women in the Workplace 2025)inakiita "ngazi iliyovunjika" - kizuizi kikubwa katika hatua ya ushiriki ambayo imechangia kushuka kwa kasi kwa uwakilishi wa wanawake kati ya ngazi ya kuingia na majukumu ya usimamizi wa kazi au uongozi.

Mwaka huu ripoti ya kila mwaka - iliyochapishwa na ushauri wa usimamizi wa McKinsey - imepanuka zaidi ya Amerika Kaskazini na kuzijumuisha Kenya, Nigeria na India, na kugundua kuwa wanawake wameendelea kuwa chini katika kushikilia nyadhifa za uongozi wa juu.

Nchini Kenya, wanawake wanaunda 50% ya majukumu ya ngazi ya kuingia katika sekta kama vile huduma za afya na huduma za kifedha, lakini kiwango hicho kinashuka hadi 26% tu katika ngazi za juu. Mfano huo ni sawa nchini Nigeria na India.

Faith hakumpa changamoto mwenzake katika mkutano huo. Alitabasamu na hakusema chochote.

Sasa kuna neno la uzoefu wa Imani. Wataalam wanaliita "kazi ya kupenda".

'Kazi ya kupenda' ni nini?

"[Hili] ni jina la kufurahisha sana lakini ukweli halisi ni nina la kukatisha tamaa sana," anasema Amy Kean, kutoka kwa kampuni ya ushauri ya mawasiliano ya Good Shout, ambayo iliunda neno hilo kuelezea "kubashiri mambo mara kwa mara ,kufikiria kupita kiasi, kujibadilisha uhalisia wa maumbile yao na kwa wanawake kila siku ili kupendwa mahali pa kazi."

Hali hiyo inaitwa "Shapeshifters: Tunachofanya ili kupendwa Kazini," utafiti wa Kean kutoka Uingereza unasema kwamba 56% ya wanawake wanahisi chini ya shinikizo la kupendwa kazini, ikilinganishwa na 36% tu ya wanaume.

Kulingana na uchunguzi wa wanawake 1,000 kote Uingereza, ripoti hiyo pia inaangazia jinsi mzigo wa kupendwa ulivyo katika mazingira ya kitaaluma.

Inaelezea jinsi wanawake wanavyohisi mara kwa mara hitaji la kulainisha kauli yao kwa kutumia lugha ya kupunguza makali , hata wakati wanapojiamini katika hoja zao. Misemo ya kawaida ni pamoja na: "Je, hiyo ina maana?" au "Samahani, haraka tu..."

Aina hii ya kujihariri kwenye kauli zao mara kwa mara, inaweza kufanywa kama njia ya kujilinda ili kuepuka kuonekana kamamtu mkali au mwenye uthubutu kupita kiasi, anasema Kean

"Pia kuna kipengele cha watu wanaoamnini hili," anaongeza, akimaanisha Uingereza. "Wanawake wa tabaka la wafanyikazi, ambao hawajazoea kujirekebisha katika mipangilio tofauti, pia wanashutumiwa kwa kuwa watu wanaotoa kauli za moja kwa moja na pia watu hawa wanateseka katika ulimwengu wa ushirika."

Kean anasema kuwa kwa wanawake wengi ambao hawajazoea kujitetea katika mazingira yao ya kibinafsi ni zaidi ya suala la kupenda: "Sio rahisi kama kuwa maarufu, ni juu ya kuwa salama, kusikilizwa na kuchukuliwa kwa uzito."

Mapema mwaka huu, Kean aliandaa mkutano wa kilele huko London kwa wanawake wanaohisi shinikizo la kazi ya kupenda, ulioitwa Mwanamke asiyependwa. Zaidi ya wanawake 300 walijitokeza kushiriki uzoefu wao.

Amy Kean anasema kuwa kujihariri mara kwa mara kwa wanawake mahali pa kazi kunaweza kuwa njia ya kujilinda

Ni suala la kimataifa

Utafiti wa Uingereza sio kipekee. Wanasosholojia wanasema shinikizo ambalo wanawake wanahisi kuhusu kupendwa ili kusonga mbele kitaaluma ni jambo linaloshuhudiwa kote ulimwenguni.

Utafiti wa 2024 wa kampuni ya kuajiri ya Textio yenye makao yake makuu nchini Marekani inaunga mkono hili. Katika uchambuzi wa data zake kutoka kwa watu 25,000 katika mashirika 253, iligundua kuwa wanawake walikuwa na uwezekano mkubwa wa kupokea maoni ya utu na kwamba 56% ya wanawake walikuwa wameitwa "wasiopendeza" katika ukaguzi wa utendaji, ukosoaji ambao ni 16% tu ya uliopokewa na wanaume.

Wakati huo huo, wanaume walikuwa na uwezekano mara nne zaidi kuliko jinsia zingine kuitwa "wanaopenda".

"Wanawake hufanya kazi ya kupendeza kwa mchanganyiko wa sababu za kijamii na kitamaduni," anasema Dk Gladys Nyachieo, mwanasosholojia na mhadhiri mwandamizi katika Kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Multimedia cha Kenya. "Wanawake kwa ujumla wanajumuishwa kuwa walezi, kuhudumia na kuweka mahitaji ya wengine mbele ya mahitaji yao wenyewe na hii mara kwa mara huhamishiwa mahali pa kazi," anasema Dk Nyachieo. "Kuna neno lake kwa Kiswahili – Mathe wa ofisi - au mama wa ofisi."

Mathe wa ofisi hufanya kazi ya ziada ili kuweka mahali pa kazi kuwa na mazingira mazuri ya kufanya kazi; ikiwa ni pamoja na kutengeneza chai, kununua vitafunio na kwa ujumla kuwa wa mtu wa kutoa huduma.

Ninauliza ni nini kibaya na hii ikiwa ndivyo mwanamke anataka kufanya.

"Hakuna ubaya juu yake," Dk Nyachieo anasema. "Lakini hutalipwa kwa hilo. Bado utatarajiwa kufanya kazi yako, na ikiwezekana kazi ya ziada."

Suluhisho

Dk Nyachieo anaamini kuwa ili kukabiliana na kazi inayofanana, mabadiliko ya kimfumo lazima yafanyike, ikiwa ni pamoja na kutekeleza sera zinazoruhusu wanawake kubadilika na kuwa na washauri wanaowatetea.

Yeye mwenyewe anawashauri wanawake kadhaa vijana wanaoanza katika kufanya kazi nchini Kenya.

"Ninawachukulia wanawake wachanga kwa uzito sana," Dk Nyachieo anasema. "Ninawaambia ikiwa utatenda kwa kutaka kupendwa kila wakati, hautaenda popote. Lazima ujadiliane mwenyewe."

Mmoja wa washauri wake ni Imani.

"Amenifundisha kutohisi shinikizo la kuwa na tabasamu na mzuri kila wakati," Faith anasema. "Ninalifanyia kazi."[hilo]