Jinsi imani 7 kuhusu mahusiano zinavyokosolewa

Je, ni mara ngapi umeketi na rafiki yako kuzungumzia uhusiano, wao, wako, au hata wa wanandoa wengine?

Au labda umefurahia maonyesho ya ukweli ambapo lengo ni kupata mpenzi.

Kwa wengi wetu, mienendo ya uhusiano wa kimapenzi inavutia kabisa.

Lakini kwa nini? kipindi cha Saa ya Mwanamke cha BBC kilimuuliza Susanna Abse, rais wa Baraza la Uingereza la Psychoanalytic.

Kitabu chake "Tell Me the Truth About Love: 13 Tales from the Therapist's Couch" kinatokana na uzoefu wake wa zaidi ya miaka 30 wa kutoa ushauri kwa wanandoa wanaokabiliwa na vikwazo katika maisha yao ya mapenzi.

"Mahusiano ni msingi wa maisha yetu. Hutupa furaha zaidi na hutusababishia maumivu zaidi mambo yanapoenda mramba," anasema Abse.

"Kila uhusiano ni tofauti na kuweka sheria kuhusu jinsi watu wanavyoendesha maisha yao ya mapenzi mara nyingi haisaidii. Hata hivyo, mara nyingi ni muhimu kuwa na hamu na kuhoji uhusiano wetu na watu wengine.

"Kutokana na hili, inaeleweka kwamba tunataka kusoma na kutazama maudhui ambayo yanaonyesha maisha yetu wenyewe, na labda hutusaidia kuelewa mambo ambayo wakati mwingine yanaonekana kuwa magumu sana kuelewa."

Kulingana na Abse, kuna hadithi fulani za kizamani ambazo zinaendelea kujirudia, na mara chache huchangia ipasavyo katika maendeleo ya maisha yetu ya mapenzi.

1.Kila mtu ana mpenzi mmoja pekee wa roho

"Imani kwamba kuna mtu mmoja tu kwako haijathibitishwa na hakika imekanushwa na uzoefu wa watu wengi."

"Hata hivyo, wazo la 'mwenzi wa roho' labda lina ukweli fulani."

"Sio juu ya hatima au kitu chochote , bali juu ya watu kuwa na hisia kali za kufanana na mwingine.

"Labda ni kwa sababu wenzi wote wawili walipata hasara ya mapema au wote wana wasiwasi sawa au wasiwasi juu ya nini maana ya kuwa karibu na mtu.

"Hisia hiyo 'pacha' mara nyingi huwa kama sehemu ya kupenda, na labda inakusaidia kumpa mtu penzi lako au moyo wako bila kuogopa sana."

2. Iwapo hujasikia mvuto mara moja, basi uhusiano huo hautaendelea

Ukweli ni kwamba hili linaweza kufeli

"Kuna uwezekano mkubwa utapata upinzani mkubwa unapojaribu kumbadilisha mwenzi wako, suala ambalo linaweza kuwa la kawaida badala ya wazi.

"Hata hivyo, uhusiano wa karibu hutubadilisha na kuna mambo mengi ambayo kila mtu hujifunza kutoka kwa mwingine katika nyanja ya kihisia, na pia katika nyanja za vitendo vya maisha ya kila siku."

"Mvuto huo huwa hisia ya ziada dhidi ya baadhi ya wasiwasi tulionao kuhusu kuingia katika uhusiano wa kimapenzi.

"Hata hivyo, unapaswa kukumbuka kwamba si tu kila mtu lakini pia kila uhusiano ni tofauti. Kwa sababu haujaingia katika uhusiano wa kimapenzi kwa shauku haimaanishi kwamba uhusiano wako hautakua ."

3.'Unaweza kubadilisha kitu usichokipenda kwa mpenzi wako'

. Ukweli ni kwamba hili linaweza kufeli

"Kuna uwezekano mkubwa utapata upinzani mkubwa unapojaribu kumbadilisha mwenzi wako, suala ambalo linaweza kuwa la kawaida badala ya wazi.

"Hata hivyo, uhusiano wa karibu hutubadilisha na kuna mambo mengi ambayo kila mtu hujifunza kutoka kwa mwingine katika nyanja ya kihisia, na pia katika nyanja za vitendo vya maisha ya kila siku."

4. 'Uhusiano mzuri unapaswa kuwa rahisi!

"Watu wengi hupata uhusiano kuwa wenye furaha na wenye changamoto.

"Takriban mahusiano yote ya muda mrefu hupitia nyakati ngumu, na kufanya kila uwezacho ili kusuluhisha uhusiano huo mara nyingi huimarisha uhusiano huo.

"Sasa, ikiwa mara nyingi unaishia kwenye mahusiano ambapo huna raha, au unahisi kama mambo yalifanyika kwa haraka na sasa unatamani usingefanya hivyo, kumbuka kwenda mbele ukiwa mtu anayehitaji wakati.

"Labda una tabia ya kukubali vitu ambavyo labda hutaki, kwa hivyo jifunze kujihusu na mambo ambayo ungefurahia.

"Sidhani kama kuna sheria ngumu na za haraka, lakini hakika usijiruhusu kuhisi shinikizo kufanya mambo ambayo hutaki kufanya."

5. 'Mahusiano mazuri yanapaswa kuwa ya kusisimua'

"Ikiwa umesisimka sana na kukimbilia katika jambo fulani, unaweza kuharakisha kujitoa katika jmabo hilo

"Kwa hivyo ni vizuri unapohisi kama unaweza kurudi haraka.

"Lakini kadri miaka inavyosonga, watu wanaweza kuhisi kutokuwa na uwezo wa kustahimili misukosuko hiyo ya kusisimua na yenye shauku katika kuvunjika kwa mahusiano.

"Ikiwa umekuwa na mahusiano mengi ya kusisimua lakini ya kukatisha tamaa kidogo, unaweza kuwa mwangalifu zaidi na kupeleka mambo polepole.

"Ni vyema kukumbuka kuwa msisimko ni mzuri, lakini raha pia ni muhimu sana. Na baadhi ya starehe hizo kadiri unavyozeeka, zinaweza kupungua ‘’

6. 'Ndoa au watoto wanaweza kuokoa uhusiano'

Ukweli ni kwamba huo si kweli’’

“Kupanga ndoa kunaweza kuleta ukaribu zaidi kwa baadhi ya wanandoa, lakini pia kunaweza kuleta mvutano mkubwa, kuoa hakuwezi kuokoa uhusiano ambao una matatizo.

"Na hivyo hivyo kwa kupata watoto.

"Inafurahisha sana watu wengi, lakini ushahidi wote unaonyesha kuwa haisaidii sana katika kuridhisha uhusiano. Kuanzia mbili hadi tatu kunaleta shida nyingi na mahitaji ya watoto mara nyingi huchukua nafasi ya kwanza badala ya mahitaji ya mwenzi.

"Ikiwa uhusiano ni thabiti na wanandoa wana njia ya kukabiliana na tamaa na tofauti, miaka ya uzazi inaweza kuwa ya ajabu.

"Na wanaweza pia kutarajia raha zaidi wakati watoto wanapoondoka."

7. 'Kilele chake ni ufunguo wa harusi au kupata watoto'

"Ni kamari ya kiwango cha juu, haswa ikiwa hauko makini kuhusu kuondoka.

"Lakini wakati mwingine unaweza kufikia hatua katika uhusiano ambapo lazima useme, 'Kuna vitu nataka na ikiwa hutaki, labda sasa ni wakati wa kuachana.

"Ikiwa wewe ni mwanamke mwenye umri wa miaka thelathini na unataka sana kupata mtoto na una mpenzi ambaye anakokota miguu, unaweza kukabiliana na ukweli, uchungu jinsi ulivyo.

"Lakini sidhani kama unapaswa kutoa kauli za mwisho mara kwa mara katika uhusiano. Zinahusisha tishio la kuachwa, na tishio la kuachwa linaelekea kudhoofisha uhusiano huo."