Siri ya kimaumbile inayoelezea kwa nini watu hupata usonji

Chanzo cha picha, Getty Images
Hadi miaka ya 1970, imani iliyoenea katika taaluma ya matibabu ya akili ilikuwa kwamba usonji ni matokeo ya malezi mabaya ya wazazi. Lakini mwaka 1977, ndipo madaktari wa magonjwa ya akili walipofanya uchunguzi wa kihistoria ulioonyesha kwamba usonji unaweza kutokea kwa watoto mapacha wanaofanana.
Utafiti wao unasema, ikiwa pacha mmoja ana ugonjwa wa usonji, kuna uwezekano wa hadi 90% pacha mwenzake kupata usonji. Na mapacha wenye sura tofauti, ikiwa mmoja atakuwa na usonji kuna uwezekano wa hadi 34% mwingine kupata usonji.
Kwa sababu ya utafiti huo, wataalamu sasa wanakubali kwamba kuna uhusiano mkubwa wa kimaumbile (jeni) na usonji. Lakini ni chembe gani hasa za jeni zinazohusika, bado wana sayansi wanalifanyia kazi jambo hilo.
Sababu za usonji

Chanzo cha picha, Getty Images
Sababu za usonji zinatokana na mabadiliko ya jeni ambayo hutokea kwa mtoto mwenyewe anapokuwa tumboni kabla ya kuzaliwa na mabadiliko mengine ya jeni mtoto huyapata kutoka kwa mzazi wake.
Unaweza kujiuliza, ikiwa mtoto mwenye usonji amerithi mabadiliko ya nadra ya jeni kutoka kwa mmoja wa wazazi wao, kwa nini mzazi pia hana usonji?
Wataalamu wanasema, kinachotokea ni kwamba kwa mzazi, haitoshi kuwa sababu ya yeye kuwa na usonji, lakini kwa mtoto, mabadiliko hayo makubwa ya jeni yanachanganyika na aina zingine za jeni na kuleta mabadiliko makubwa.
Baadhi ya wataalamu wanaamini pia kuna sababu za kimazingira zinazohusika katika ukuaji wa usonji - hata miongoni mwa mapacha wanaofanana.
Kulingana na Taasisi za Kitaifa za Afya za Marekani (NIH), sababu za kimazingira zisizo za kijeni, ni pamoja na uchafuzi wa hewa kabla ya kuzaa na baadhi ya dawa za kuua wadudu, matatizo wakati wa uzazi na kukosekana kwa oksijeni katika ubongo wa mtoto - mambo ambayo hupelekea mabadiliko ya jeni kwa mtoto.
Usonji una athari nyingi, kuanzia wale walio na matatizo makubwa katika ukuaji wa kimwili na kiakili ambao huishi kuwa tegemezi, hadi wengine walio na mahitaji machache ya usaidizi ambao huona usonji kama sio tatizo kwao.
Wanajitahi kushughulikiwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa baadhi ya watu, usonji ni sehemu ya maisha yao - na si kitu kinachohitaji kutibiwa. Lakini Joseph Buxbaum, profesa wa magonjwa ya akili katika Chuo cha Tiba cha Mount Sinai, anaamini watu wenye usonji wanahitaji msaada. za kijeni, anahisi kwamba baadhi ya wanaharakati wa tawahudi wanakosa uhakika.
"Ninapoambiwa na mtu kuwa, 'Sawa nina ugonjwa wa akili ila sifikirii kuwa nahitaji kuchunguzwa,' mimi husema, 'sawa, vipi lakini kuhusu mtu mwenye usoni na hawezi kuzungumza, akili yake ni IQ ya 50 na hawezi kuishi peke yake na bila kusimamiwa,' "anasema "Kwa hiyo, ninapofikiria kuhusu uingiliaji kati, ninafikiri juu ya watu hawa."
Baadhi ya wataalamu wanaamini usonji, unahitaji kushughulikiwa kama vile ulemavu mwingine wowote, hasa wale ambao wameathiriwa zaidi - wanahitaji matibabu.
Moja ya njia inayopendekezwa na wataalamu ni kutumia teknolojia ya v Crispr, ambayo inaruhusu wanasayansi kuhariri DNA ya mtu, inaweza kutumika kuingilia kati hatua ya awali ya maisha ya mtoto mwenye dalili za usonji.
Kwa mfano, tiba ya chembe za urithi inaweza kutolewa kwa watoto ambao hawajazaliwa waliopatikana na mabadiliko ya jeni, wakiwa bado tumboni.
Wataalamu pia wana matumaini kuhusu uwezekano wa utafiti wa chembe za urithi wa kubuni matibabu mapya kwa baadhi ya matatizo ambayo watu wenye usonji hupata, kama kifafa, matatizo ya usingizi na matatizo ya utumbo.















