Je, kula huku unatazama TV ni mbaya kwa afya yako?

s

Chanzo cha picha, Getty Images

    • Author, 제시카 브라운
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Siku hizi, kuna vipindi na sinema nyingi sana za kutazama kiasi cha kukufanya usitake kupitwa. Hata kama unakula inakuvutia kuwasha runinga (TV) unaendelea kula huku ukitazama TV. Je ni sawa kwa afya yako?

"Chakula cha jioni cha TV," unaweza kusema hivyo kwa maana ya kuhusisha kula wakati wa kutazama TV, kwa ujumla hiyo ni mbaya.

Kula ukitazama TV lilianzia Marekani mwanzoni mwa karne ya 20. Watu walikua wanaangalia picha za kukaa kwenye kochi na kuangalia TV huku watu wakila vyakula vilivyosindikwa na vilivyojaa chumvi

Lakini vipi ikiwa unakula kitu kingine unapotazama TV? Kula chakula chenye wingi wa mboga mboga na nafaka nzima inachukuliwa ni ulaji wa afya. Lakini nini kinatokea unapokula chakula hicho wakati unatazama TV? Je, kula chakula kizuri kunaweza kuleta madhara?

Ukiangalia utafiti, inawezekana kabisa. Uchunguzi unaonyesha kwamba kula wakati wa kuangalia TV ni mbaya kwa afya yako, bila kujali ni aina gani ya chakula unakula.

Inakuvuruga na kukupotezea kumbukumbu

Wazo kwamba mazingira yanayozunguka mlo yanaweza kuathiri ulaji wa virutubishi ni madai ya kawaida katika jamii ya kisayansi. Kwa mfano, tafiti nyingi zimehusisha kutazama televisheni na ongezeko la hatari ya kunenepa kupita kiasi (na sababu kuu ikiwa ni kupungua kwa mazoezi).

Kutazama TV wakati wa kula kunaweza pia kuathiri kiasi cha chakula unachokula. Monique Alblas, profesa wa sayansi ya mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Amsterdam, anataaj nadharia ya kueleza kwa nini unakula zaidi unakuwa unakula huku upotazama TV

Kwa kawaida tunazama simulizi za kusisimua, tunakuwa na wakati mchache wa kuweka fikra na mawazo yetu kwenye chakula. Hii inaweza kusababisha kula kupita kiasi kwa sababu hatutambui ishara za mwili zinazoonyesha kuwa tumeshiba. Pia kuna utafiti unaoonyesha kwamba unapokula chakula huku ukitazama TV, huenda usikumbuke ulichokula na huenda usihesabu kwa usahihi kiasi ulichotumia, ambayo inaweza kusababisha kula zaidi.

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wengi wanakula huku wanaangalia TV

Alblas alitafiti jinsi nyakati za chakula hubadilika watu wanapotazama TV huku wakila.

Utafiti huo ulitumia takwimu ziilizokusanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kijamii ya Uholanzi, ambayo iliwataka watu kuweka kumbukumbu kwa wiki kuhusu kile walichokula, walichotazama kwenye TV, na hata programu wanazotazama.

Alblas alichambua takwimu hizo na kugundua kuwa watu walipotazama TV huku wanakula, muda wao wa chakula uliongezeka.

Zaidi ya hayo, siku ambazo walitazama TV wakati wa kula, muda wa chakula ulikuwa mrefu kuliko siku ambazo hawakutazama TV. Alblas alisema hii inaweza kutafsiriwa kama ukosefu wa umakini na kutotambua ni kiasi gani wanakula.

Lakini utafiti hautsemi ikiwa watu walikula zaidi au walikula nini haswa, kwa sababu takwimu pekee iliyorekodiwa ilikuwa ni wakati wa chakula. Hata hivyo, inawezekana kwamba washiriki walivutiwa sana na kipindi cha TV na kuna uwezekano walihesabu vibaya muda(dakika au saa) zao za chakula.

TV

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Chipsi na vitafunwa vingine vinatumika sana wakati wa kutazama filamu
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mwanasayansi wa Van Meer amefanya utafiti wa shughuli za ubongo wa binadamu wakati akila. Katika utafiti mmoja, alikuwa na washiriki aliowataka kukariri nambari fupi na ndefu wakati wa kula. Wale ambao walilazimika kukariri nambari ndefu waliripoti kwamba chakula chao kilikuwa na ladha kidogo.

Van Meer alisema kuwa watu wanapopoteza umakini na jambo fulani ama jambo fulani linapoingilia ulaji wao, shughuli katika maeneo ya ubongo inayohusika na mtazamo wa ladha pia hupungua.

Mara nyingi vitu vya kukaanga, bisi, chips na vitafunio vingine hutumika sana na watu wanapokuwa wakitazama TV.

"Unapopoteza umakini kwenye chakula chako, unahisi kushiba kidogo. Ndiyo maana unaweza kutafuta vitu vya kutafuna hata kama umetoka kupata mlo wako wa kawaida."

Utafiti umeonyesha kuwa unapotazama kipindi cha ucheshi mfano, kuna uwezekano mdogo wa kutamani vyakula kama vile chokoleti au popcorn iliyotiwa siagi, ni tofauti na ukitazama vipindi vingine ambavyo sio vys kuchekesha.

Je, niepuke kula wakati natizama TV?

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nadharia za kitafiti zinaonyesha kwamba watoto wanaweza kula chakula kingi zaidi wakiwa wanaangalia TV kuliko mtu mzima

Kuna nadharia kadhaa zinazoelezea kwa nini tunakula zaidi tunapotazama TV, lakini utafiti juu ya mada hii kwa kweli umeingia katika matatizo fulani.

Watafiti mara nyingi hutumia shajara za chakula na tabia za kutazama TV kufuatilia ulaji wa watu, Lauber alisema, lakini washiriki mara nyingi huripoti matumizi yao ya chini ya vyakula visivyo na afya.

Katika data ambayo Alblas alitumia, washiriki walirekodi shughuli zao zote za kila siku, lakini hawakuwa na ufahamu hasa wa kile walichokula au kutazama kwenye TV.

Kula vitafunio mbalimbali Chanzo cha picha: Alamy

Maelezo ya picha, Unapotazama kipindi cha televisheni kinachochosha, unaweza kuishia kula chakula zaidi kuliko unapotazama kitu cha kuvutia.

다양한 간식을 먹고 있는 모습

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Ukiwa unakula na unatazama kipindi cha TV kisichofurahisha unaweza kula chakula kingi zaidi kuliko ukiwa unatazama kipindi kimnachokufurahisha

Pia kuna changamoto zinazojitokeza wakati wa kufanya utafiti katika mazingira ya maabara. TV kawaida ni njia ya kupumzika nyumbani. Kwa hiyo, si rahisi kuiga mazingira haya katika maabara.

"Njia za uchunguzi wa moja kwa moja zinaweza kusababisha washiriki kuwa na tabia tofauti kuliko kawaida kwa sababu wanafahamu kuwa wanazingatiwa," Lauber alisema.

Alblas alisema utafiti zaidi unahitajika katika mazingira ya ulimwengu halisi ili kuelewa tabia za ulaji na mambo yanayoathiri.

"Tunajua baadhi ya njia ambazo TV huathiri ulaji wa chakula, lakini bado kuna mambo mengi ambayo hayajulikani na yanahitaji ufahamu bora."

Stevenson alisema athari za TV kwenye matumizi ya chakula hutegemea mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na aina ya maudhui yanayotazamwa. Kwa mfano, unapoona wahusika wakila kwenye skrini, unaweza kuhisi hamu ya kula pamoja. Kasi ya programu pia inaweza kuwa na athari; Utafiti mmoja uligundua kuwa sinema za mapigano husababisha watu kula zaidi kuliko maonyesho ya mahojiano.