Waafrika Kusini bado wanapambana na 'ubaguzi wa kiuchumi' miaka 30 baada ya uhuru

Chanzo cha picha, Kyla Herrmannsen/BBC
Chumba cha Jamelah hapo awali kilikuwa chumba cha kuhifadhia maiti; Faldilah ilikuwa bafu; Bevil's - ofisi ya daktari ambapo alikuja kuchukua dawa yake ya ugonjwa wa kisukari.
Wote wamechuchumaa katika hospitali iliyoharibika katika mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini, wakiandamana kwa kile wanachokiona kushindwa kwa serikali kuwapatia nyumba za bei nafuu.
Mwisho wa ubaguzi wa rangi ulileta haki za kisiasa na uhuru kwa wote. Lakini wakati wanaposhiriki uchaguzi wa saba wa kidemokrasia nchini, kuvumilia ukosefu wa usawa bado kunagawanya nchi hii.
Na katika hali nyingi sera za makazi za chama tawala cha African National Congress (ANC) zimeimarisha bila kukusudia jiografia ya ubaguzi wa rangi, badala ya kuubadilisha.
Wanaharakati wa vuguvugu linaloitwa Reclaim the City walikalia Hospitali ya Woodstock usiku wa kuamkia miaka saba iliyopita.
Lengo lilikuwa kuchukua mali iliyo karibu na katikati mwa jiji, anasema mmoja wa viongozi, Bevil Lucas, kwa sababu upatikanaji wa kazi na huduma zinazotolewa na hii ni muhimu katika kurekebisha makosa ya ubaguzi.
"Aina mpya ya ubaguzi wa rangi ya kiuchumi" imechukua nafasi ya sheria za ubaguzi wa rangi ambazo ziliwaweka watu weusi na weusi (kama watu wa rangi mchanganyiko wanavyojulikana wa Afrika Kusini), wamenaswa katika umaskini katika vitongoji vya kingo za Cape Town, anaiambia BBC.
"Maskini na walio hatarini kwa ujumla wamesukumwa hadi pembezoni mwa jiji."
Sasa wana haki ya kuhama lakini hawawezi kumudu kodi ya juu inayodaiwa na waendelezaji wa majengo katikati mwa jiji.
Kwa Jameelah Davids, eneo lilikuwa kila kitu.
"Kuhamia kwangu hapa ni kwa sababu ya mtoto wangu ambaye ni mgonjwa," anasema. "Anaenda shule hapa karibu. Ilikuwa karibu sana kwake. Kila kitu kipo. Na amestawi.”
Aliamua kuishi na familia yake katika ofisi ya zamani ya chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali.

Chanzo cha picha, Kyla Herrmannsen/BBC
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mpangaji mwingine, Faldilah Petersen alinionyesha jinsi ambavyo amebadilisha bafu ya hospitali kuwa nyumba, kugeuza chumba cha choo kuwa jikoni, na eneo la beseni kuwa chumba cha kulala.
"Nilifukuzwa kama mara 10 kwa mwaka," ananiambia.
"Lakini kuishi katika kazi hii kulinipa fursa hiyo ya kuboresha maisha yangu, na niko huru zaidi kufanya kile ninachohitaji na ni karibu zaidi na jiji pia. Ni kama kurudi nyumbani."
Mamlaka ya jiji linaafiki kwamba eneo hilo linaweza kuendelezwa kwa madhumuni ya makazi, lakini inawaita wapangaji wa sasa kuwa wakaaji haramu na kusema wanahitaji kuondoka kabla ya shughuli ya uendelezaji wa jiji kuanza.
ANC ilichukua mamlaka miaka 30 iliyopita na Mkataba wa Uhuru ambao uliahidi makazi kwa watu walionyimwa makazi salama yasiyo na ubaguzi wa rangi. Tangu wakati huo, imejenga zaidi ya milioni tatu na kutoa umiliki bila malipo, au kwa kukodisha kwa viwango vya chini vya soko.
Lakini orodha za nyumba za serikali bado ni ndefu - Bi Davids amekuwa akisubiri kwa karibu miaka 30, Bi Petersen kupata nyumba.
Na nyingi zimejengwa mbali na katikati mwa jiji, ambapo ardhi ni ya bei nafuu, na kushindwa kugeuza mipango ya enzi ya ubaguzi wa rangi ambayo ilichangia ukosefu wa usawa.
Hakuna mahali ambapo hali hiyo imekithiri zaidi ya Cape Town, anasema Nick Budlender, mtafiti wa sera za miji, akiliita "pengine eneo la miji lililotengwa zaidi popote pale duniani".

Chanzo cha picha, Kyla Herrmannsen/BBC
Ilikuwa ni lango la kuingia kwa walowezi wa kikoloni na waliiunda kwa njia hiyo, anasema, hivyo kuigeuza ingehitaji uingiliaji kati wa kimakusudi. Lakini "tangu mwisho wa utawala wa ubaguzi wa rangi, hakuna nyumba hata moja ya bei nafuu ambayo imejengwa ndani ya jiji la Cape Town".
Kuna ishara za mbinu mpya. Serikali ya mkoa, inayoendeshwa na Muungano wa Kidemokrasia (DA) inajenga mtindo wa "maisha bora" kwenye ardhi ya serikali karibu na kazi na huduma za jiji.
Mradi wa Conradie Park pia unatokea kuwa tovuti ya hospitali ya zamani.
Awamu ya kwanza inatoa mchanganyiko wa chaguzi za ruzuku na thamani ya soko, na awamu ya pili inajengwa.
Waziri wa Miundombinu wa Mkoa Tertuis Simmers anakubali mrundikano wa watu 600,000 wanaosubiri usaidizi wa makazi, lakini anasema kuna mipango "kabambe" ya kuwasilisha miradi 29 kama hiyo ya makazi ya kijamii.
Lakini bajeti ni ndogo - anatafuta ushirikiano kutoka kwa sekta ya kibinafsi - na muda usiojulikana.
Na nyumba, ambayo mara nyingi ni mada kuu katika chaguzi, imeshuka katika orodha ya vipaumbele vya kisiasa.
Ilani ya DA, ambacho ni chama rasmi cha upinzani katika ngazi ya kitaifa, hakiitaji hasa, wala vyama vingine.

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












