Vita vya Ukraine: Marekani yajitenga na uvamizi wa Belgorod ndani ya Urusi

Marekani imejiweka mbali na uvamizi wa Urusi, ambao Moscow inasema uliishia katika kushindwa kwa waasi wenye silaha walioingia kutoka Ukraine.

Maeneo ya eneo la mpakani la Belgorod yalishambuliwa siku ya Jumatatu, katika mojawapo ya mashambulizi makubwa zaidi ya kuvuka mpaka tangu Urusi ilipovamia jirani yake mwaka jana.

Urusi baadaye ilitoa picha za magari ya kijeshi ya Magharibi yaliyotelekezwa au kuharibiwa, ikiwa ni pamoja na Humvees yaliyotengenezwa Marekani.

Marekani ilisisitiza kuwa "haikuhimiza au kuwezesha mashambulizi ndani ya Urusi".

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje alikiri ripoti "zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kwingineko" kwamba silaha zilizotolewa na Marekani zimetumika, lakini akasema nchi yake "inatilia shaka wakati huu kuhusu ukweli wa ripoti hizi."

Katika taarifa ya habari Jumanne, Matthew Miller aliongeza: "ni juu ya Ukraine kuamua jinsi ya kuendesha vita hivi."

Vijiji vya Belgorod karibu na mpaka vilihamishwa baada ya kushambuliwa na makombora. Urusi inasema washambuliaji 70 waliuawa, na imesisitiza wapiganaji hao walikuwa wa Ukraine.

Lakini Kyiv inakanusha kuhusika na makundi mawili ya wanamgambo wa Urusi yanayompinga Rais wa Urusi Vladimir Putin yanasema yalihusika na uvamizi huo.

Uvamizi wa Jumatatu ulisababisha Moscow kutangaza operesheni ya kukabiliana na ugaidi, na kuipa mamlaka maalum ya kuzuia mawasiliano na harakati za watu.

Hatua hizo ziliondolewa tu alasiri iliyofuata, na hata wakati huo, moja ya vikundi vya wanamgambo ilikuwa ikidai bado inadhibiti "eneo dogo, lakini kipande chetu cha Nchi Mama".

Gavana wa Belgorod alisema raia mmoja alifariki wakati wa ghasia hizo, na kwamba wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Katika tukio la baadaye, Vyacheslav Gladkov alisema Jumanne jioni kwamba Belgorod ilishambuliwa upya na ndege isiyo na rubani ambayo ilidondosha kifaa cha kulipuka na kuharibu gari.

Alisema chombo hicho kilichokuwa kikiruka kilidunguliwa na kwamba hakukuonekana kuwa na majeruhi wapya.

Madai ya pande zinazozozana hayajathibitishwa kwa uhuru ingawa BBC iliweza kubaini kuwa jengo linalotumiwa na wakala mkuu wa usalama wa Urusi, FSB, lilikuwa miongoni mwa yaliyoharibiwa wakati wa ghasia hizo.

Haijabainika ni nini kilisababisha uharibifu huo.

Ikizungumzia uhasama wa Belgorod, wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema "kitengo cha uundaji wa kitaifa wa Ukraine" kilivamia eneo lake kufanya mashambulio.

Moja ya picha zake ilionesha gari lililoharibika na maneno "kwa Bakhmut" yameandikwa kwa Kirusi pembeni. Hii inaonekana kurejelea mji wa Kiukreni ambao Urusi inasema imeuteka hivi karibuni - dai lililopingwa na Kyiv.

Pamoja na kuua makumi ya watu waliowataja kama "magaidi wa Kiukreni" katika mashambulio ya risasi na angani, wizara hiyo ilidai kuwa imewarudisha wapiganaji wengine kwenye mpaka wa Ukraine.

Lakini maafisa wa Ukraine walisema washambuliaji walikuwa Warusi, kutoka kwenye vikundi vinavyojulikana kama Liberty of Russia Legion na Russian Volunteer Corps (RVC).

Machapisho ya mitandao ya kijamii kutoka kwa makundi hayo mawili ya kijeshi yalionekana kuthibitisha kuhusika kwao. Vikundi vyote viwili pia vililiambia shirika la utangazaji la umma la Ukraine Suspilne kwamba walikuwa wakiunda "eneo lisilo na kijeshi kwenye mpaka na Shirikisho la Urusi ambalo hawataweza kuishambulia Ukraine".

Mashambulio yoyote katika ardhi ya Urusi yanawafanya viongozi katika muungano wa kijeshi wa Nato wa nchi za Magharibi kuwa na wasiwasi.

Uvamizi huo wa kuvuka mpaka unaweza kuwa wa aibu kwa Moscow, na kwenda kwa njia fulani kumaliza mtazamo mbaya wa Ukraine wa kuripotiwa kupoteza udhibiti wa Bakhmut baada ya miezi ya mapigano makali na ya umwagaji damu.

Pia kuna uwezekano kuwa sehemu ya operesheni za kuunda sura ya Ukraine kabla ya mashambulizi yake yajayo, yanayolenga kuwavuta wanajeshi wa Urusi kutoka kusini ambako Kyiv inatarajiwa kushambulia.

Lakini sio maendeleo ambayo yanawezekana kukaribishwa na Magharibi.

Silaha za masafa marefu ambazo nchi hizi zimetoa kwa Kyiv - ingawa hazijatumika katika shambulio hili, bado zinakuja na masharti kwamba hazipaswi kutumiwa kulenga shabaha ndani ya Urusi.

Licha ya kukanusha rasmi kutoka kwa Kyiv, ni vigumu kuamini kwamba uvamizi huu ulifanywa bila usaidizi wa kijasusi wa kijeshi wa Ukraine.

Inashiriki katika maelezo ya Kremlin kwamba usalama wa Urusi yenyewe uko chini ya mashambulizi kutoka kwa vikosi vibaya vinavyoungwa mkono na Magharibi.

Ni simulizi ambayo huenda ikachochewa na ripoti kwamba baadhi ya wale walioshiriki wanahusishwa na itikadi kali za mrengo wa kulia, na kutilia nguvu madai ya Moscow kwamba inajaribu kuwaondoa Wanazi mamboleo Ukraine.