Je! kundi la Palestine Islamic Jihad ni nani na wana tofauti gani na Hamas?

cx

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marekani, Israel na nchi za Ulaya zimeiweka Palestina Islamic Jihad na Hamas kuwa ni makundi ya kigaidi

Mlipuko katika Hospitali ya Al-Ahli Arab huko Gaza uliua takriban watu 500 jioni ya Jumanne (Oktoba 17) jioni - Israel imelilaumu kundi la 'Palestinian Islamic Jihad' (PIJ) kwa mlipuko huo, huku mataifa mengine mengi yakiilaumu Israel kwa shambulio hilo.

Jeshi la Israel linadai roketi ya PIJ ilirushwa kimakosa na kugonga hospitali. Marekani imeunga mkono madai ya Israel.

Palestinian Islamic Jihad' (PIJ) ni nani?

'Palestinian Islamic Jihad' ni kundi la pili kwa ukubwa katika Gaza baada ya Hamas. Kundi hilo linajulikana kwa msimamo wake mkali. PIJ lipo Gaza na Ukingo wa Magharibi.

PIJ ni kundi ambalo haliamini katika aina yoyote ya mazungumzo ya amani ya kisiasa na inalenga ushindi wa kijeshi dhidi ya Israel.

"Baada ya ushindi dhidi ya Israel, Dola ya Kiislamu itaundwa kwa kuunganisha Israel, Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi," kundi hilo linaamini.

Dhana ya kuundwa kwa Islamic Jihad imechochewa na harakati ya Misri ya Muslim Brotherhood. Mwaka 1981 Fathi Al Shaqaki na Abd Al Aziz waliunda 'PIJ'.

Shikkaqi alizaliwa Rafah, Gaza. Rafah ni sehemu ya Ukanda wa Gaza unaopakana na Misri. Alizaliwa katika kambi ya wakimbizi, familia ya Shikkaki ilifukuzwa wakati wa Vita vya Kwanza vya Waarabu na Israeli (1948).

Kunzishwa kwake

dsc

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, IJP halina tawi la kisiasa, linatumia silaha pekee

Kulingana na ripoti ya The Economist, miaka ya 1980 PIJ ilikuwa ni mtandao wa wanamgambo kidogo waliotawanyika, likiwa na wanachama mia kadha tu.

Wanachama wa zamani wa Muslim Brotherhood, ambao waliamini vita dhidi ya Israel inapaswa kupewa kipaumbele, pia walishirikiana na kundi hilo.

Waanzilishi wake walikutana na wapiganaji wa Iran na wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran nchini Lebanon katika miaka hiyo.

Wanachama wa 'PIJ' walianza kupokea mafunzo kutoka Hezbollah na baadaye wakaunda kikundi chenye nguvu cha kijeshi cha Al-Quds Brigades.

PIJ imedai kuhusika na mashambulizi kadhaa dhidi ya Israel, lakini kubwa zaidi ni shambulio lao mwaka 1995 ambapo wanajeshi 21 wa Israel na raia mmoja waliuawa.

Viongozi wa awali wa PIJ waliathiriwa pakubwa na wanaharakati kutoka Misri wa Muslim Brotherhood. Kiongozi wa Iran, Ayatollah Rohollah Khamenei, pia alikuwa na ushawishi mkubwa katika kundi hilo.

Hamas na Islamic Jihad

dewsx

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, PIJ na Hamas ni tofauti kimawazo lakini yote yanaichukulia Israel kama adui wao
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Marekani, Israel na nchi za Ulaya zinazichukulia Palestina Islamic Jihad na Hamas kuwa ni makundi ya kigaidi. Makundi haya ni tofauti kimawazo lakini yote yanaichukulia Israeli kama adui wao.

Na hiyo ndiyo sababu ya umoja wao. Kumekuwa na mashambulizi kadhaa ambapo Hamas na Islamic Jihad wameungana.

Mkurugenzi wa zamani wa 'Masomo ya Mashariki ya Kati' katika chuo kikuu Jawaharlal Nehru, India, A. K. Pasha anasema, mtu hawezi kuielewa Islamic Jihad bila kuielewa Hamas.

1988 kiongozi wa Hamas, Mohammed al-Zahr, alipendekeza mazungumzo ya amani. 1988 Sheikh Yassin, mwanzilishi wa Hamas, alitoa maoni kama hayo.

Pasha anasema, "Wakati haya yakitokea, kikundi fulani ndani ya Hamas hakikuyaafiki hayo. Waliamua kujitenga na Hamas. Na hapo ndipo IJP ilipoanza."

Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi cha Marekani - 'NCT' kinasema mwaka 2019 na 2020, Islamic Jihad ilirusha makombora dhidi ya Israel bila msaada wa Hamas.

Kwa mujibu wa 'NCT', mwaka 2022 Islamic Jihad "ilirusha takriban roketi 1100 kwa Israeli kujibu kifo cha kiongozi wao."

IJP halina tawi la kisiasa, linatumia silaha pekee. Ni tofauti na Hamas, ambao wanashiriki katika siasa na wameshinda uchaguzi 2006, Hamas ilishinda uchaguzi katika maeneo ya Wapalestina huko Gaza.

Nchi nyingi zinaichukulia Hamas kama nguvu ya kisiasa, na Hamas pia inachukuliwa kuwa inawakilisha sehemu ya watu wa Palestina. Hamas imekuwa madarakani Gaza tangu 2007. Idara zote huko zinaendeshwa na Hamas.

Kwa upande mwingine, katika siku za hivi karibuni 'PIJ' imepata nguvu katika eneo la Ukingo wa Magharibi. Kundi hilo lilikumbwa na msukosuko mkubwa katika miaka ya 1990 wakati katibu mkuu wake, Fathi al-Shaqaki, alipouawa na kikosi cha siri cha Israel mwaka 1995.

Baada ya hapo, kundi lilidhoofika lakini 'PIJ' ilipata nguvu tena wakati wa Intifadha ya Pili yaani Vita vya Waarabu na Israeli (2000 hadi 2005). Hamas pia ilipata nguvu katika kipindi hiki na kuchukua udhibiti wa Gaza.

Nani anaifadhili PIJ?

fdc

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa mujibu wa Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi cha Marekani, PIJ inasaidiwa na Iran na Hezbollah ya Lebanon.

Lakini Profesa Pasha haamini katika hili. Anasema, "Hamas inaungwa mkono na Iran, kwa nini Iran imsaidie mshindani wa Hamas? Na kama PIJ wangekuwa wanasaidiwa na Iran, wagekuwa na nguvu kama Hamas.’’

"PIJ inachukua msaada kutoka kwa watu wa kawaida," anasema.

PIJ ina makao yake makuu mjini Damascus, Syria, ambako kiongozi wake wa sasa, Ziad al-Nakhlah, anaishi. Pia ana ofisi Tehran, Iran.