Timu zinahitaji nini ili kufuzu Afcon 2025?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mali, mabingwa watetezi Ivory Coast na Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi ambazo zimebakisha ushindi mmoja kabla ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025.
Muda wa kusoma: Dakika 6
Pia unaweza kusoma

Kufikia wakati huu wiki ijayo tutajua timu 24 zitakazoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 2025, huku duru mbili za mwisho za mchujo zikiwa zimepangwa kuchezwa.

Ghana ndio jina kubwa lililo katika hatari ya kukosa kushiriki michuano hiyo nchini Morocco, huku Black Stars wakihitaji kuvuna pointi nyingi zaidi huku wakitumai Sudan itashindwa mara mbili.

Timu mbili za juu katika kila moja ya makundi 12 ya kufuzu zinasonga mbele, huku mabingwa wa zamani Algeria, Cameroon, DR Congo, Misri na Senegal wakiwa tayari wamehakikishiwa nafasi zao pamoja na Angola, Burkina Faso na wenyeji.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ndio timu pekee ambayo bado haijashiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, huku Botswana na Rwanda zikiwania kucheza mara ya pili.

BBC Sport Africa inaendesha sheria ya nani anahitaji nini ili kujinyakulia nafasi katika hafla kubwa zaidi ya michezo barani Afrika, ambayo itaanza tarehe 21 Desemba mwaka ujao na kuendelea hadi 18 Januari 2026.

Tunisia yatoa kijasho ili kufuzu

Kundi A ndilo lenye nguvu zaidi, huku mataifa yote manne yakiwa yakiwa na uwezo wa kufuzu.

Viongozi Tunisia wako pointi moja mbele ya Comoro na mbili mbele ya Gambia, huku wawakilishi Madagascar wakiwa nyuma zaidi.

The Carthage Eagles, ambao wanawinda rekodi ya kufuzu kwa mara 17 mfululizo kwenye fainali hizo, wamemweka Kais Yaacoubi kwenye wadhifa wa muda baada ya kumfukuza kocha mkongwe Faouzi Benzarti.

Madagascar lazima wawashinde Waafrika hao wa Kaskazini siku ya Alhamisi ili kuimarisha matumaini yao hafifu, huku Gambia wakikabiliana na pambano la ‘nyumbani’ dhidi ya Comoro siku moja baadaye mjini Berkane.

Kulingana na matokeo hayo, duru ya mwisho ya mechi, Tunisia itakapowakaribisha Scorpions na Comoro kuwaburudisha Madagascar, inaweza kuwatia wasiwasi mashabiki wa nchi zote nne.

Kundi B linaonekana kuwa moja kwa moja zaidi, huku Morocco ikiwa tayari imejihakikishia nafasi ya kwanza na Gabon inayotazamiwa zaidi kushika nafasi ya pili.

Panthers watakuwa wenyeji wa Morocco siku ya Ijumaa na watamaliza katika nafasi nzuri iwapo watalingana na matokeo ya Jamhuri ya Afrika ya kati dhidi ya Lesotho.

Super Eagles wanakaribia kufuzu huku Zebras wakitarajiwa kuweka historia

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Botswana huenda ikahitaji kuifunga Misri mjini Cairo siku ya Jumanne - baada ya kupoteza 4-0 nyumbani dhidi ya Mafarao
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Botswana wamo kifua mbele kunyakuwa nafasi moja iliyosalia katika kundi C, wakiwa na alama tatu mbele ya Cape Verde na Mauritania.

The Zebras wanawakaribisha Mauritania siku ya Ijumaa kabla ya Cape Verde kuwakaribisha Misri, ambao wamempumzisha nahodha Mohamed Salah.

Rekodi ya ana kwa ana inaweza kutekelezwa kusuluhisha mambo wakati Botswana itasafiri kwenda Misri na Mauritania kuwakaribisha wenyeji wa visiwa hivyo Jumanne.

Kocha Morena Ramoreboli anachukua mikoba ya muda ya Botswana baada ya Didier Gomes da Rosa kuachia ngazi na badala yale kuamua kuinoa klabu ya Al Ahli Tripoli ya Libya.

Wakati huo huo, Nigeria inahitaji pointi moja tu ili kufuzu kutoka Kundi D, baada ya kuzawadiwa mabao 3-0 dhidi ya Libya baada ya kukwama katika uwanja wa ndege nchini humo usiku kucha mwezi uliopita - ingawa adhabu hiyo inaweza kukatiwa rufaa.

Mmoja kati ya Benin na Rwanda anaonekana kuungana nao, huku Libya ikikaribia kuondolewa.

Mabingwa hao wa Mediterenean lazima wazishinde Rwanda na Benin na kutumaini kwamba Super Eagles watawafanyia wema kwa kushinda mechi zao zote mbili dhidi ya wapinzani wao.

Kufuzu kwao huenda kukafikia siku ya mwishoisipokuwa tu iwapo Benin italazimika kuifunga Nigeria na Rwanda itashindwa kuandikisha ushindi dhidi ya Libya.

Black Stars inaonekana kuwa tayari kuondoka

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambulizi wa Sierra Leone Kei Kamara, ambaye sasa anaichezea LA FC, amezindua ujio wake mpya wa kimataifa

Katika Kundi E, Togo lazima waishinde Liberia ambayo tayari imeondolewa katika mechi itakayochezwa mjini Monrovia siku ya Jumatano ili kuendeleza jitihada zao za kushindana na Equatorial Guinea siku ya Jumapili mjini Lome

Hata hivyo, National Thunder inaweza kufuzu ikiwa na mechi moja ikiwa itawashinda vinara Algeria siku ya Alhamisi.

Matumaini ya Ghana yanazidi kudorora katika Kundi F baada ya kuzoa pointi mbili pekee katika mechi nne.

Mabingwa hao mara nne wa bara wanaweza hata kuondolewa wakati watakapomenyana na Angola mjini Luanda siku ya Ijumaa, kwani Sudan itasonga mbele ikiwa wataepuka kushindwa ‘ugenini’ dhidi ya Niger mjini Lome siku iliyotangulia.

Mchezo wa mwisho wa Ghana ni dhidi ya Niger, lakini matumaini yao madogo yalipata pigo lingine wakati beki Alexandre Djiku na washambuliaji Antoine Semenyo na Inaki Williams walipokuwa miongoni mwa wachezaji wanane waliojiondoa kwenye kikosi cha kocha Otto Addo, huku kiungo wa Arsenal Thomas Partey akiwa hajaitwa.

Kamara arudi kuinua Leone Stars

Kundi G linaweza kuamuliwa siku ya mwisho kati ya Zambia na Sierra Leone, huku mabingwa watetezi wa Afcon Ivory Coast pia wakihitaji ushindi mmoja zaidi ili kuwa na uhakika wa nafasi ya kutetea ubingwa wao.

Leone Stars inaweza kunyakua hatua hiyo na kusonga mbele kwa pointi na Zambia ikiwa itashinda ‘ugenini’ dhidi ya Chad mjini Abidjan Jumatano.

Wachezaji hao wa Afrika Magharibi wameimarishwa na mshambuliaji Kei Kamara mwenye umri wa miaka 40 - mfungaji bora wa pili katika historia ya Ligi Kuu ya Soka ya Marekani - akitoka kustaafu kimataifa.

Zambia inawakaribisha Waivory Coast siku ya Ijumaa lakini wanajua kwamba sare kutoka kwa mechi yao ya ugenini dhidi ya Sierra Leone itatosha kuisongesha mbele baada ya kushinda mechi ya kwanza kati ya timu hizo mbili.

Guinea na Tanzania zinachuana kuwania nafasi ya mwisho katika Kundi H, huku wenyeji hao wa Afrika Magharibi wakiwa na pointi mbili.

Guinea itakuwa mwenyeji wa DR Congo huku Tanzania ikisafiri hadi Ethiopia, na Guinea kisha kwenda Tanzania katika raundi ya mwisho.

Ethiopia wana nafasi ndogo ya kufuzu, lakini lazima ishinde michezo yao yote miwili na wanatumai Guinea itapoteza mechi zao zote mbili.

Uganda Cranes inatafuta pointi moja

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uganda, ambao walitoka sare ya 2-2 katika ziara yao ya Afrika Kusini mwezi Septemba, wanatazamiwa kuandaa Afcon 2027 pamoja na Kenya na Tanzania.

Msumbiji na Mali zote ziko na pointi nane kileleni mwa Kundi I, na kila upande utajihakikishia kufuzu iwapo watashinda mechi yao mjini Maputo siku ya Ijumaa.

Guinea-Bissau wako nyuma kwa pointi nne na wanatumai kufaidika na matokeo yoyote, lakini vijana wa Luis Boa-Morte wanahitaji kurejea kutoka kwa safari yao ya Eswatini ambayo tayari imeondolewa na pointi tatu.

Guinea-Bissau itakuwa mwenyeji wa Msumbiji katika raundi ya mwisho ya mechi, wakati Mali watakapowakaribisha Eswatini.

Zimbabwe wanapigiwa upatu kuungana na Cameroon kufuzu kutoka Kundi J na watafanya hivyo iwapo wataepuka kushindwa nyumbani dhidi ya Kenya katika maechi ya sare ya bila bila katika uwanja wa Polokwane siku ya Ijumaa.

Harambee Stars lazima ishinde mchezo huo ili kuweka matumaini yao hai, jambo ambalo lingewaacha wakihitaji kuboresha matokeo ya Zimbabwe nchini Cameroon watakapoikaribisha Namibia Jumanne.

Katika Kundi K, Uganda wanahitaji pointi moja pekee kutoka kwa mechi zao mbili, nyumbani dhidi ya Afrika Kusini na ugenini Congo-Brazzaville, ili kurejea katika fainali kwa mara ya kwanza tangu 2019.

Afrika Kusini inahitaji ushindi mmoja na itakuwa na uhakika wa kuifunga Sudan Kusini ambayo haijashinda nyumbani Jumanne ijayo ikiwa itadondosha pointi nchini Uganda.

Congo inahitaji ushindi mkubwa mara mbili ili kuharibu sherehe

Mechi za kufuzu katika Kundi L tayari zimekamilika, huku Burkina Faso na Senegal zikiwa zimesalia na mechi mbili kufuzu dhidi ya Burundi na Malawi.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla