Mashine za kuua: Jinsi Urusi na Ukraine zilivyoboresha droni hatari zinazotishia ulimwengu

Chanzo cha picha, Getty Images
Silaha hizi za bei nafuu, zinazotengenezwa kwa wingi, zinakua kwa kasi, na wataalam wanaonya kuwa ni wakati wa kufikiria upya maswala ya usalama kwa ulimwengu wote.
Hii imeelezwa katika makala ya gazeti la Uingereza la The Guardian, ambayo inachambua ukuaji wa teknolojia ya ndege hizo zisizokuwa na rubani katika vita vya Urusi na Ukraine.
Makala hiyo inaangazia, jeshi la Ukraine ilipozindua roboti yake mpya ya kuua iitwayo GOGOL-M.
Kwa kubofya mara moja, ndege hii isiyo na rubani yenye urefu wa mabawa ya mita sita ilipaa kutoka eneo lisilojulikana hadi kwenye anga ya bluu.
Iliruka kilomita 200 ndani ya Urusi, kisha ikafyatua ndege mbili zisizo na rubani za kushambulia zilizoning'inia kwenye mbawa zake. Zinaweza kukwepa , na huruka kwa kimo cha urefu wa chini.
Droni hizi ndogo zilianza kukagua ardhi chini kwa uhuru ili kupata shabaha na kisha kuipiga. Droni hizi za FPV hufanya hivyo kwa uhuru kwa kutumia Akili mnemba.
Ushawishi wa kibinadamu hapa ni mdogo - tu kuifundisha droni juu ya aina ya shabaha inayolengwa na eneo la jumla mahali pa kulitafuta eneo hilo.
Ndege isiyo na rubani inayoweza kutumika tena na "watoto" wake hugharimu $10,000. Inaweza kusafiri hadi kilomita 300, wakati ndege zisizo na rubani zinaweza kusafiri kilomita 30 nyingine.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hapo awali, mashambulizi kama hayo yangehitaji mifumo ya roketi inayogharimu kati ya dola milioni 3 na dola milioni 5, mtengenezaji anasema.
"Ikiwa tutafadhiliwa ipasavyo, tunaweza kuzalisha maelfu ya ndege hizi zisizo na rubani kila mwezi," anasema Andriy kutoka Strategy Force Solutions, taasisi ilitengeneza teknolojia hii kwa ajili ya vikosi vya jeshi la Ukraine.
Ulimwengu ulishangazwa na Operesheni Spiderweb, ambapo mnamo Juni 1, ndege zisizo na rubani 117 za Ukraine zilishambulia vituo vya anga ndani kabisa ya Urusi, vikilenga ndege za Urusi za masafa marefu zenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.
Na hii, Guardian inabainisha, sio hata sehemu ya juu zaidi ya kile Waukraine na Warusi hutumia katika mapigano.
Zawadi isiyoeleweka kwa ulimwengu kutoka kwa vita vya Urusi na Ukraine ni silaha za bei nafuu, zinazoweza kuongezeka zinazojaribiwa kwa wakati halisi kwenye uwanja wa vita.
Na malengo sio tu mizinga, ndege, makutano ya reli, au miundombinu muhimu.
Kipaumbele ni kuawaangamiza watu.
"Kutakuwa na mifumo ya bei nafuu huru ambayo inaweza kufanya kazi ya silaha nzito, kwani hili ni lengo kuu, kwa sababu mafundisho ya vita yamebadilika, vifaa vizito vinatumiwa kwa kiwango kidogo," Waziri wa anayehusika na mabadiliko ya Dijitili wa Ukraine Mykhailo Fedorov alisema.
Na Warusi hawako nyuma hapa pia, aliongeza.
Mashine zenye nguvu na huru

Chanzo cha picha, PRESIDENT OFFICE/UKRAINE
Kwa miaka minane, wanadiplomasia wanaofanya kazi chini ya mwamvuli wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa aina fulani za silaha wamekuwa wakikutana huko Geneva, Uswizi, kujadiliana jinsi sheria za kimataifa zinavyopaswa kukabiliana na umaarufu unaoongezeka wa silaha hatari zinazojiendesha.
Miongoni mwa maswali ni kiwango gani cha uingiliaji wa binadamu kinapaswa kusisitizwa na ni nani anayepaswa kuwajibika ikiwa roboti itafanya uhalifu.
Juhudi hizi hazijazaa matunda. Bado hakuna makubaliano juu ya kile kinachojumuisha silaha hatari inayojiendesha, ukiachia kile kinachopaswa kupigwa marufuku na kile kinachopaswa kudhibitiwa.
The Guardian inamnukuu Alexander Kmentt, Mkurugenzi wa Idara ya Kudhibiti wa silaha katika Wizara ya Mambo ya nje ya Austria:
"Ujumuishaji wa uhuru katika mifumo ya silaha unafanyika haraka sana. Nyingi kati ya zile tunazoziona nchini Ukraine bado hazijajitegemea kikamilifu, lakini tayari inafanyik," anabainisha.
Mnamo Desemba 2024, Austria iliwasilisha rasimu ya azimio kwa Umoja wa Mataifa kuhusu mifumo hatari ya silaha zinazojiendesha na kusisitiza kwamba zinapaswa kudhibitiwa ndani ya mfumo wa Mkataba wa Silaha Fulani za Kawaida.
Mkutano Mkuu ulipitisha rasimu hiyo kwa kura 166 za kuunga mkono, nchi tatu zilipinga (Belarusi, Urusi, na Korea Kaskazini), na nyingine 15, ikiwa ni pamoja na Ukraine, zilijizuia.
Tishio linaloletwa na mifumo hatari ya silaha zinazojiendesha, mashine ambazo "zina nguvu na uhuru wa kuchukua maisha ya binadamu bila udhibiti wa binadamu, hazikubaliki kisiasa, zinachukiza kimaadili na lazima zipigwe marufuku na sheria za kimataifa," alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi












