Je, Poland inajenga jeshi lenye uwezo mkubwa zaidi Ulaya?

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jeshi la Poland tayari ina zaidi ya wanajeshi 200,000, na kuifanya kuwa na jeshi la tatu kwa ukubwa katika NATO. Lakini wizara ya ulinzi inatarajia kuongeza idadi ya wanajeshi 300,000
Muda wa kusoma: Dakika 7

Na Svyatoslav Khomenko, Pavel Aksenov

BBC

"Tunahitaji miaka miwili zaidi, na kisha Jeshi la Poland litakuwa jeshi lenye nguvu zaidi la ardhi barani Ulaya," maneno haya yalizungumzwa na Waziri wa Ulinzi wa Poland Mariusz Blaszczak mwezi Aprili mwaka jana.

Tangu wakati huo, serikali ya Poland imebadilika, Blaszczak mwenyewe amejikuta katika upinzani mkubwa, lakini serikali ya sasa inaendelea na harakati za kuimarisha jeshi, kutumia kiasi kikubwa cha fedha na juhudi za kutekeleza hilo.

Bila shaka serikali ya Poland inatarajia kwamba kuwa na jeshi lenye nguvu kutairuhusu sio tu kuongeza uwezo wake wa ulinzi, lakini pia kuwa muhusika muhimu katika kanda yake.

Lakini, muhimu zaidi, baada ya kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine, Poland ina wasiwasi mkubwa kwamba jeshi la Urusi linaweza kuanza vita kwenye eneo lake.

Licha ya madai ya Vladimir Putin kwamba Urusi "haina maslahi" katika Ulaya ya Mashariki, uongozi wa Poland unasema wazi kwamba nchi hiyo inaishi katika "nyakati za kabla ya vita" na kutabiri kuanza kwa vita na Urusi katika miaka mitatu.

Unaweza pia kusoma:

Poland inajiendesha yenyewe. Sasa ni kiongozi kati ya nchi za NATO sio tu katika suala la matumizi ya ulinzi kama asilimia ya Pato la Taifa, lakini pia kwa suala la sehemu gani ya matumizi yake ya kijeshi hutumia silaha.

Hata hivyo, mamlaka zinakabiliwa na changamoto kubwa katika kuboresha mfumo wa ulinzi wa taifa, kutokana na uhaba wa wafanyakazi wa katika kuzalisha silaha ambazo ni kuu kuu katika sekta ya kijeshi na pia mzigo mkubwa kwa uchumi.

Jinsi Poland inavyojiendesha yenyewe

Katika mwaka 2024, Poland itatumia 4.12% ya pato lake la taifa kwa ulinzi, na mnamo 2025 inapanga kutumia karibu 5%.

Hii ni idadi kubwa zaidi katika nchi za Muungano wa Atlantiki ya Kaskazini.

Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa amani ya Uswidi (SIPRI) iliandika katika utafiti uliochapishwa mnamo Aprili 2024 kwamba matumizi ya ulinzi ya Poland mnamo 2022 yaliongezeka kwa 75% hadi $ 31.6 bilioni, likiwa ni ongezeko kubwa miongoni mwa nchi zote wanachama wa NATO.

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wapoland kwa ujumla wana mtazamo chanya kwa jeshi na huduma ya kijeshi.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Poland ilinunua kutoka Marekani helikopta ya 96 AH-64E Apache, ikiwa ni moja ya aina bora za helikopta za aina yake ; makombora ya 486 HIMARS, ambayo yameonekana kuwa na ufanisi sana katika vita vya Ukraine; vifaru vya 366 M1A2 250 ambavyo ni vya kisasa zaidi aina ya SEPv3; Makombora 32 , aina ya F-35A; mifumo miwili ya kuzuia mashambulia ya angani ya Patriot na mfumo wa kudhibiti ulinzi wa anga.

Muuzaji mwingine mkubwa wa silaha kwa Poland ni Korea Kusini. Warsaw imehitimisha makubaliano ya mfumo na Seoul kwa ununuzi wa makombora ya maangamizi ya 648 K9 Thunder ya Howitzers na mizinga ya 980 K2 Black Panther. Baadhi ya mifumo hii itajengwa nchini Poland.

Wapoland pia wamepata mafunzo kuhusu matumizi ya makombora yanayorushwa na ndege ya 48 FA-50 kutoka Jamhuri ya Korea na pia imeagiza ndege za kijeshi tatu za Mechnik kutoka Uingereza.

Kipindi kifupi cha uhusiano kati ya Urusi na Poland kilianza mwaka 2009 chini ya ushawishi wa "kurejesha" uhusiano kati ya Moscow na Washington. Na kilimalizika kwa ajali ya ndege ya serikali ya Poland karibu na Smolensk mnamo Aprili 10, 2010.

Lakini, licha ya historia mbaya, hadi 2014, mvutano wa uhusiano kati ya Poland na Urusi ulijikita zaidi katika eneo la maneno ya kisiasa.

Lakini kwa Urusi kulitwaa eneo la Crimea la Ukraine na kuzuka kwa uhasama huko Donbass, fikra za wasomi wa kisiasa wa Poland na njia yao ya maendeleo ya majeshi ya nchi hiyo ilibadilika sana.

"Uboreshaji wa Kisiwa"

Mwaka 2014, mada ya silaha za kisasa ilikuwa sehemu kubwa ya mjadala wa kisiasa wa ndani nchini Poland. Chama cha kihafidhina cha sheria na haki, ambacho kiliingia madarakani mwaka 2015, kiliifanya kuwa moja ya vipengele vya mpango wake wa kisiasa.

Mawaziri wa ulinzi Antoni Macierewicz na kisha Mariusz Blaszczak walitangaza mikataba mikubwa ya usambazaji wa silaha za kisasa zaidi, walitangaza haja ya kuongeza idadi ya vikosi na silaha, na kuhakikisha usalama wa Poland upo katika hali ya kisiasa isiyo na utulivu.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hapo awali, Jeshi la anga la Polandi lilikuwa na silaha hasa ndege za zamani za Usovieti, lakini sasa Poland ina silaha za F-16s za Marekani (pichani) na F-35s, pamoja na FA-50s ya Korea Kusini

"Lakini hata baada ya 2014, kwa miaka kadhaa tulikuwa tukishughulika kuliweka jeshi letu katika hali ya kisasa zaidi, yaani, jeshi halikuwa la la kisasa kabisa, vitengo tu vichache vya kibinafsi vilikuwa vya kisasa. Kwa mfano, mifumo ya ulinzi wa anga na makombora ilianza kuboreshwa kwa sababu mifumo ya zamani, ya baada ya enzi ya Usovieti ilikuwa imeharibika," anasema Dk Lukasz Stach kutoka kituo cha mafunzo ya kimataifa na maendeleo katika Chuo Kikuu cha Jagiellonian huko Krakow.

Hata hivyo, hata ndani ya mfumo wa kisasa wa "island" , mageuzi yalifanyika katika jeshi la Poland ambalo lilibadilisha muonekano na uwezo wake.

Miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na kuundwa kwa vikosi vya ulinzi vya Wilaya na ununuzi mkubwa wa silaha: kwa mfano, makubaliano ya usambazaji wa Patriot ulihitimishwa mnamo 2018, na makubaliano ya ununuzi wa F-35 yalihitimishwa mnamo 2020.

"Hatuwezi kusubiri kwa muda mrefu zaidi"

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwezi Februari 2022 ulikuwa mshtuko kwa Poland.

"Hii ilikuwa ishara kwa sisi sote: 'Hello, Poland , amka! Hatuwezi kusubiri kwa muda mrefu zaidi!" Ilikuwa wazi kwamba serikali ya Poland haiwezi tena kutegemea ukweli kwamba kwa namna fulani, Warusi watajizuia na kuishia Ukraine.

Kuangalia kile Moscow inafanya, tunapaswa kuzingatia matukio ya kutia hofu zaidi kwa Poland. Na hii inamaanisha kwamba tunahitaji kupanua uwezo wa ulinzi wa eneo letu - sasa, mara moja," Jenerali mstaafu wa jeshi la Poland Tomasz Bąk aliiambia BBC.

Kwa kweli, sauti ya viongozi wa kisiasa na kijeshi wa Poland imebadilika sana tangu Februari 2022. Katika moja ya mahojiano yake ya kwanza baada ya kuchaguliwa kama waziri mkuu wa Poland, Donald Tusk alitangaza kwamba "tunaishi katika nyakati za kabla ya vita" - tofauti kubwa na maneno yake ya awali.

h

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Poland hununua silaha nyingi kutoka Korea Kusini, kwa mfano, vitengo vya silaha vya kibinafsi K9

Mnamo Machi 2024, mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Kanali Jacek Severa, alisema kuwa Poland imebakiza miaka mitatu kujiandaa kwa mapambano na Urusi.

Licha ya Urusi kumvamia jirani yake, Kremlin inaendelea kusisitiza kuwa ni makosa kwa nchi za Magharibi kuhofia tisho la Urusi. Mwezi Februari mwaka huu, alipoulizwa iwapo Urusi inaweza kutuma wanajeshi wake nchini Poland, Vladimir Putin alijibu: "Ni katika kisa kimoja tu: ikiwa Poland itaishambulia Urusi. Kwa sababu hatuna maslahi katika Poland, Latvia, au mahali popote."

Sio Wapoland wote wanamwamini: mwezi Machi, data ya utafiti wa kijamii ilionyesha kuwa 48% ya Wapoland hufikiria hali ya Urusi kushambulia Poland inawezekana kabisa. Asilimia 41 ya waliohojiwa hawakuamini.

"Kuishi bila vita"

Jenerali Tomasz Bąk, baada ya kuondoka jeshi la Poland, akawa mwalimu katika moja ya vyuo vikuu huko Rzeszów.

"Niliwahi kuwaambia wanafunzi wangu: hebu tuwe waaminifu, inua mikono yako ikiwa utaondoka nchini wakati wa vita. Idadi ya mikono ilinishangaza," anakumbuka.

Kulingana na kura ya maoni iliyochapishwa mnamo Aprili, 59% ya raia wako tayari kukaa Poland ikiwa vita vitazuka, na asilimia 11 wako tayari kutoa upinzani wa silaha kwa mchokozi. Asilimia 20 ya watu wa Poland wanasema kuwa wataondoka nchini humo baada ya kuanza kwa uhasama.

Matokeo ya utafiti mwingine juu ya mada kama huo yalionyesha kuwa elimu ya mhojiwa ni kubwa zaidi, uwezekano mkubwa wa yeye kufikiria juu ya kukimbia vita nje ya mipaka ya nchi yake.

v

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwaka 2017, programu za kutoa mafunzo kwa raia katika jeshi zilianza kutekelezwa nchini Poland

"Nadhani ni suala la mabadiliko ya kizazi. Leo, vijana katika nchi yoyote - iwe Poland, Ukraine, Marekani, au hata Urusi - fikiria katika makundi tofauti. Jamii leo, zaidi ya hapo awali, inataka kuishi bila vita, inataka kuishi kwa amani na ustawi, na sio kumwaga damu, hata kwa nchi yao. Lazima tukubali hili kama ilivyopewa na tuzingatie tu katika kupanga kwamba tutapoteza sehemu ya rasilimali yetu ya uhamasishaji kwa sababu za lengo, "anasema Jenerali Bonk.

Waandishi wa BBC wanaona serikali ya Poland na sera yake ya habari kama sehemu ya kulaumiwa kwa hali hii ya mambo.

Mjadala wa usajili

Ni kwa sababu hizi kwamba suala la kurudi kwa usajili wa lazima wa vijana kwa huduma ya kijeshi linaibuliwa mara kwa mara nchini Poland. Mamlaka zinajitenga na hili kwa sasa.

"Tunahitaji kufikiria juu ya kurudisha huduma ya lazima ya kijeshi - sio lazima iwe ya muda mrefu, inaweza kuwa miezi mitano au sita. Wanaume, na labda wanawake wa kundi fulani la umri, wanapaswa kujiandaa na kufundishwa katika ngazi ya msingi kwa ajili ya hatua katika vita vinavyowezekana, "anasema Jenerali Tomasz Bąk.

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Suilaha inazozinunua Poland ni pamoja na vitengo vya 486 HIMARS

Silaha ni moja ya sababu muhimu zaidi zinazoathiri mwendo wa operesheni za kijeshi katika vita.

Mwaka mmoja na nusu baadaye, kama ilivyoelezwa katika makala kuu ya Kipolishi Newsweek, iliyochapishwa mwezi Juni mwaka huu, PGZ Dezamet hutoa makombora elfu 30-40 kwa mwaka.

Kama nchi nyingine yoyote, Poland haiwezi kutegemea tu msingi wake wa viwanda kwa ununuzi wa kijeshi, na kwa hivyo sio tu kuwekeza kijeshi na viwandani, lakini pia kununua silaha na vifaa vya kijeshi nje ya nchi.

Katika jamii ya Kipolishi, matumizi ya ulinzi bado hayajasababisha maandamano yoyote makubwa, kwani baada ya Februari 2022 tishio kutoka Urusi lilikuwa kubwa sana.

Lakini je, kuna ufahamu wowote wa jinsi vita kama hivyo vinaweza kushuhudiwa?

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Seif Abdalla