Ukomo wa hedhi: Mwiko unaowahangaisha wanawake wa Kihindi

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, meryl sebastian
- Nafasi, BBC News Kochi
- Author, Anagha Pathak
- Nafasi, BBC Marathi
- Akiripoti kutoka, Delhi
- Muda wa kusoma: Dakika 5
Wanawake wa Kihindi kwa wastani huacha kupata hedhi mapema ikilinganishwa na wenzao wa kutoka maeneo ya magharibi,tafiti zaonyesha.
Ripoti zimeonyesha kuwa visa vya wanawake ambao huacha kupata hedhi mapema ,hasa wale walio na umri wa kati ya miaka 30-39 zimeongezeka.
‘'Baadhi ya tafiti zinaashiria kuwa umri wa wastani kwa wanawake kukoma kupata hedhi nchini India ni miaka 47,'' anasema Dkt Ruma Satwik, daktari wa masuala ya uzazi katika hospitali ya Delhi Sir Gangaram.
Hii ni mapema kuliko maeneo mengine,kwa mfano Marekani ambapo umri wa wastani wa kukatika kwa hedhi ni miaka 51.
Madaktari wanasema kukatika kwa hedhi mapema kunasababishwa ukosefu wa lishe bora, mazingira na maumbile.
Lakini kwa mataifa ambayo mazungumzo kuhusu hedhi huzungukwa na unyanyapaa na tamaduni za kupotosha, hamasa kuhusu kukatika hedhi haziwafikii baadhi ya wanawake.
Sangeeta, alijikuta akifanya majukumu ya nyumbani na ulezi huku akiendelea kupitia mabadiliko makali ya homoni kama vile joto mwilini, chovu, kukosa usingizi, ya mgongo na tumbo.
‘‘Kuna faida gani kuishi hivi?,” anajiuliza mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 43,’'wakati mwingine nahisi maumivu yangu yataisha nikifa.”
Sangeeta, ambaye ni mfanyikazi wa masuala ya usafi katika Hospitali ya Dr. Ram Manohar Lohia, mjini Delhi, aligundua hapati tena hedhi mwaka mmoja uliopita lakini alijua hivi karibuni kuwa hospitali hiyo ina kliniki maalum kwa ajili ya kushughulikia masuala ya afya yanayohusiana na hali hii.
Maili kadhaa kutoka Delhi ni mkazi wa Mumbai, Mini Mathur alisema alijisikia kama alikuwa akipitia kila dalili inayowezekana alipotimia miaka 50.
Mtangazaji huyu wa televisheni alisema hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya na alifuata mtindo wa maisha mzuri.
Hali hiyo ilikumbusha ushauri aliopewa na rafiki yake miaka mingi iliyopita: “Inaathiri kila mtu. Tafadhali jizatiti.”

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Data ya sensa ya India ya mwaka 2011 ilionyesha kuwa nchi hiyo ilikuwa na wanawake milioni 96 walio na umri wa miaka 45 na kuendelea. Kufikia mwaka 2026, idadi hiyo inatarajiwa kufikia milioni 400, anasema Dkt. Anju Soni, rais wa Jumuiya ya kukatika kwa hedhi ya India.
“Wanawake wa India wanaishi theluthi moja ya maisha yao baada ya kukatika kwa hedhi,” anasema.
Wanawake wanachukuliwa kuwa wamefikia kukatika kwa hedhi wanapokosa hedhi kwa mwaka mzima. Hata hivyo, hili hutanguliwa na perimenopause, kipindi cha kupungua polepole kwa homoni za uzazi, ambacho kinaweza kudumu kati ya miaka miwili hadi kumi.
Dalili ni nyingi na mbalimbali, zikijumuisha mabadiliko katika hisia, kumbukumbu, mwelekeo wa akili, na pia athari kwa mifupa, ubongo, misuli, ngozi na nywele. Kulingana na athari zake , wanawake wanaweza kuona kupungua kwa ubora wa maisha yao.
Dalili nyingi zinaweza kudhibitiwa na madini ya kujaliza,mabadiliko ya mlo kamili,na pia ya muhimu Zaidi ni matibabu ya kubadilisha homoni ,madaktari wanasema.Kufikia sasa hakuna vipimo vya kubaidi hali hii bali wanategemea dalili wanazoelezwa na kina mama.
Madaktari pia wameibua wasiwasi kuwa kukatika kwa hedhi mapema hakufanyiwi utafiti wa kutosha duniani mafunzo yake yakitolewa machache katika shule za kusoma udaktari.Haya yanachangia kuwa vigumu kugundua hali hii kwa wakati na hutamausha wanawake wengi,anasema dkt Satwik.
Mathur anasimulia jinsi ilimbidi kutembelea vituo mbalimbali vya afya nchini India na Ng’ambo ndani ya miaka miwili kabla ya kufanikiwa kupata matibabu sahihi.
Alishangazwa namna dalili alizokuwa anapata -ambazo zilijumuisha kutokuwa na uchangamfu,kusahau,maumivu ya viungo na wasiwasi – alipata nafuu baada ya kuanza kutumia krimu ya homoni za kike .
‘'Ilinibidi kutafuta matibabu Austria ili kushauriwa na daktari na kuhakikishiwa kuwa kinachonisibu ni kawaida.”

Chanzo cha picha, Getty Images
Kutojieleza kwa mwanaharakati Atul Sharma ambaye alikuwa na wasiwasi baada ya kukatika kwa hedhi kulimsababisha kuwa na msongo wa mawazo na kukosa hamu ya kujamiiana lakini alimficha mumewe kwa miaka sita.
Sharma ambaye hufanyakazi na wanawake mashinani kuhusu masuala ya afya na uchumi katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh,alitambua kuwa hakuna msaada wowote uliotolewa kwa akina mama hao kuhusu kukatika kwa hedhi zao katika kliniki za serikali.Wafanyikazi wa Huduma za afya za kimsingi waliokuwa na ari ya kuwasaidia hawana ufahamu wa kutosha.
'‘Pia muuguzi ambaye huja hapa anasema ,sasa itabidi utafute dawa kwa hali hii pia vumilia tu hutokea kwa kila mwanamke.”
Mwaka wa 2022-24,dkt Satwik alichunguza wanawake 370 walio na umri kati ya 40 na 60 dalili wanazozipata na makali yake.
‘'Asilimia 20 hawakuwa na dalili zozote.Waliobakia walikuwa na dalili za wastani huu asilimia 15 hadi 20 wakiwa na dalili kamili za hali hii.”

Chanzo cha picha, Getty Images
Huku taarifa kuhusu kukatika kwa hedhi ikiwa finyu, wanawake wengi wamegeukia mitandao ya kijamii na jumbe za intaneti ambapo wanapata msaada mkubwa kutoka kwa wataalamu kuliko madaktari wao.
Marekani na watu maarufu kama vile Naomi Watts na Halle Berry, ambao wanachangia kuhamasisha mazungumzo kuhusu menopause.
Wengi wakifuatilia mtalaam wa Marekani dkt Mary Claire Haver ambaye aliwasilisha utafiti wake mitandaoni na watu mashuhuri kama vile waigizaji Naomi watts na Halle berry wakiangazia makala hayo yanayojulikana kama The M Factor: Shredding the Silence on Menopause.
Watts anaandika kitabu kuhusu kukatika kwa hedhi huku Berry anasukumia sheria mpya ya kuhamasisha utafiti mafunzo na elimu.
Mathur anafuraha kuwa alipata matibabu sahihi.’' Wanawake ambao wanafanya shughuli za nyumbani ikiwemo ulezi, kazi rasmi na kusafiri katika maeneo yaliyo na msongamana wanamudu vipi ?anajiuliza.
'‘Hatujawafikia mataifa ya magharibi “anasema.’' Hatuna dawa na krimu za kutosha za homoni za wanawake ambazo wanawake wengi India wanzihitaji.”
Kwa sasa anasoma kozi Marekani, iliyoidhinishwa na bodi ya kitaifa ya wakufunzi wa afya na ubora,akiwa na matumaini atakuwa kielelezo na msaidizi na kuhakikisha taarifa kuhusu hali hii zinafikia wanawake wote India.
‘'Gharama ya kupata matibabu ya hali hii ni ghali na wanawake wengi wa kipato cha chini India hawawezi kumudu matibabu hayo,” Sharma anasema.
Vile vile anafurahia kuwa ameepuka mfadhaiko na uchungu unaoambatana na hali hii baada ya kupata matibabu.
Hamasa zinapaswa kuendelezwa na madaktari.anasema Dkt. Satwik ,akiongezea kuwa kuna haja ya mazungumzo kuhusu kukatika kwa hedhi kama vile mijadala ya afya ya kubalehe.
Dkt Soni ameweka wazi kuwa serikali iko tayari kushirikiana na wahudumu wa afya haswa wa mashinani na vijijini.
'‘Kwa sasa wanawapatia virutubisho vya afya na huduma za afya kwa wanawake wajawazito. Pia hili litajumuisha kwa wanawake walio na matatizo ya homoni.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid na kuhaririwa na Ambia Hirsi












