Ni kwanini hatari ya mshituko wa moyo huongezeka miongoni mwa wanawake waliofikia ukomo wa hedhi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Magonjwa ya moyo ni chanzo cha vifo vya wanawake kote duniani, lakini yamesalia kutobainika na kutotibiwa, kulingana wataalamu wa magonjwa ya moyo.
Kwa Dkt Susan Connolly, daktari wa magonjwa ya moyo katika Chuo cha Galway, ni muhimu kwamba wanawake watambue hatari zinazoweza kusababishwa na magonjwa ya moyo na mawazo kuwa magonjwa haya hayawezi kuwapata wanaume yanafaa kukomeshwa.
Hatari huanza, kutokana na mabadiliko ya homoni, wakati wa ukomo wa hedhi, anasema mtaalamu wa magonjwa ya moyo.
"Kabla ya ukomo wa hedhi(menopause), hatari za wanawake kupata magonjwa ya moyo ni ya kiwango cha chini zaidi kuliko wanaume, lakini baada ya ukomo wa hedhi hatari hiyo huongezeka na inadhaniwa kuwa ni kutokana na kupungua kwa estrogen,homoni ambayo kwa kawaida huulinda moyo. ", anafafanua.
Estrogen ni kundi la homoni ambazo hufanya kazi kubwa katika afya ya uzanzi ya mwanamke, mkiwemo katika vipindi vya kubalehe, hedhi , mimba na ukomo wa hedhi.
Homoni hizi pia ni muhimu kwa moyo, mifupa, na afya ya ubongo katika wanaume na wanawake, kulingana na taarisisi ya maktaba ya Marekani ya masuala ya tiba- US National Library of Medicine (NLM).
Kwa Dr. Sandra McNeill, kdaktari bingwa wa afya ya uzai aliyebobea katika magonjwa ya moyo , ni muhimu kwa wanawake kuwa katika hali bora iwezekanavyo ya kiafya wakati wanapofikia kipindi cha ukomo wa hedhi (menopause).
Hii ni pamoja na kuepuka uvutaji wa sigara, kuzingatia uzito wa mwili, na kufanya mazoezi ya mwili.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kwa kawaida, ilifikiriwa kuwa matatizo ya moyo huwapata wanaume pekee. Bahati mbaya, hilo sio sahihi. Wanawake kwa kiasi fulani hulindwa na estrogen kupata matatizo hayo hadi wanapofikia jukomo wa hedhi ," anasema.
Hata hivyo, wakati mwanamke anapofikia hatua hiyo ya maisha, na kushuka kwa viwango vya estrogen, moyo huumia, na kulingana na McNeill, matatizo ya moyo huwa mengi kuliko ya wanaume wenye umri huo.
Kutokana na athari chanya za estrogen, wanawake kwa ujumla hupata magonjwa ya moyo miaka 10 baada ya wanaume.
Iwapo ukomo wa hedhi-menopause, utafika katika umri wa miaka 40, hatari ya ugonjwa wa moyo ni ya juu zaidi kuliko wanawake wengine wenye umri saw ana wako.
Dalili tofauti
"Huenda tusiwe na dalili sawa na wanaume, dalili zinazofahamika ambazo tumejifunza shuleni. Lakini wanawake waliopita ukomo wa hedhi wana hatari ya juu zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wanaume, na magonjwa ya mfumo wa moyo katika wanawake waliovuka ukomo wa hedhi ni sababu inayoongoza ya vifo miongoni mwa wanawake hao ," anasema daktari huyo bingwa wa afya ya uzazi ya wanawake McNeill.
Dalili hizi kuu mara nyingi ni kubanwa kwa kifua, maumivu katika mkono, ukosefu wa pumzi ya kupumua, ambazo pia zinaweza kushuhudiwa miongoni mwa wanawake wenye magonjwa ya moyo. Lakini sio dalili hizo pekee. Wanawake pia huripoti dalili nyingine, kama vile kichefuchefu, mchoko, kushindwa kwenda haja kubwa, wasi wasi na kisunzi.
"Wanawake mara nyingi huenda hospitalini kulalamikia matatizo haya baadaye kwa sababu hawatambui kuwa wana mshituko wa moyo, hawajioni kuwa wamo hatarini ," Connolly anadai.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kutambua na kutibu mshituko wa moyo haraka huboresha nafasi zako za kuishi.
Mara nyingi wanawake hawachunguzwi haraka sawa na wanaume .
Hii ni kutokana na miongoni mwa sababu nyingine, ukweli kwamba wanawake wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na maradhi ya moyo yaliyo "jificha", ambayo hayana dalili, au kwa sababu wataalamu wa afya wakati mwingine hawatambui ugonjwa mapema na dalili zake huwa ni tofauti na zile za wanawake.
Wanawake pia wana uwezekano mkubwa wa kuumia kutokana na magonjwa fulani ya moyo ambayo ni vigumu kuyabaini, kama vile maradhi ya moyo yanayoshambulia mishipa midogo iliyopo kwenye ukuta wa moyo- (coronary microvascular disease), kupasuka kwa moyo (broken heart syndrome) na mengine ambayo hayagunduliki kwa urahisi.
Kuchelewa kugunduliwa kwa maradhi hayo kunaweza kupelekea kucheleweshwa kwa huduma ambako kungelisaidia katika kuzuia maradhi hayo kuwa mshituko wa moyo.
"Ni maradhi yanayowaua zaidi wanawake duniani," anasema daktari bingwa wa moyo. " Wanawake wanaokufa kutokana na maradhi ya moyo ni mara mbili ya wale wanaofariki kutokana na saratani, kwahiyo ni muhimu kwamba wanawake waelewe hatari hii, ambayo huanza kuongezeka katika kipindi cha ukomo wa hedhi, (menopause)."
Zaidi ya kutunza afya za mwili na akili, wanawake wanaotaka kutunza mioyo yao pia wanashaurriwa kufuatilia kwa karibu viwango vyao vya korestro.















