Ghasia zaongezeka katika ukingo wa magharibi

Chanzo cha picha, Reuters
Abed Wadi alikuwa akijitayarisha kuelekea mazishini wakati ujumbe ulipoingia.
Ilikuwa picha aliowasilishiwa na rafiki yake, kundi la wanaume waliojifunika uso wakiwa wameshikilia mashoka, na vilipuzi huku kukiwa na ujumbe pembeni ulioandikwa kiyahudi na kiarabu.
"Kwa panya wote wanaoishi katika mabomba ya maji taka kijijini Qusra, tunawasubiri na hatutawaomboleza, " ujumbe ulisema.
"Siku ya kulipiza kisasi inawadia. "
Qusra ni Kijiji anakotokea Wadi, katika eneo la kaskazini la ukingo wa magharibi karibu na Nablus. Siku hiyo kulikuwa na mazishi ya Wapalestina wanne kutoka kijiji hicho.
Watatu waliuawa jana yake - Okotoba 11 - baada ya walowezi wa Israeli kuingia Qusra na kuishambulia familia ya kipalestina ikiwa nyumbani.
Wanne alipigwa risasi na kuuawa katika makabiliano yaliofuata na wanajeshi wa Israeli.
Siku iliofuata wanakijiji wa Qusra walikuwa wanajaitayarisha kuelekea hospitali umbali wa kiasi cha saa moja na nusu na warudi na maiti.
Ili kufanya hivyo, walihitaji kusafri katika eneo lililo na makaazi ya Waisraeli, ambapo hatari ya kushambuliwa hata katika siku za kawaida imeongezeka katika wiki mbili tangu Israel iingie vitani na Hamas.
Wadi aliweka simu chini na kuendelea na kujitayarisha kuelekea mazishini. Kulikuwa na maiti za wanaume wanne waliohifadhiwa ndani ya jokofu katika hospitali wanaohitaji kuletwa nyumbani. Anasema hangekubali kutishwa.
Wadi hakujua kwamba katika saa chache zijazo walowezi wa Israeli wangeukabili msafari wa waombolezi na kakake na mpwa wake mdogo wangepigwa risasi na kuuawa.
" Kama tungechelewa kwa siku moja au hata mbili, ingekuwa na faida gani? " Wadi alisema akiwa amekaa katika bustani ya nyumbani kwao Qusra.
"Unadhani walowezi wangeondoka hapa siku ya pili?"

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kwa mujibu wa ofisi ya mratibu misaada ya Umoja wa mataifa, wiki iliofuata shambulio la Hamas ilikuwa mbaya zaidi kwa Wapalestina walioishi katika ukingo wa magharibi tangu ofisi hiyo ilipoanza kunakili vifo mnamo 2005 huku takriban Wapalestina 75 wakiuawa na wanajeshi au walowezi wa Israeli, na ghasia za walowezi wa Israeli zikiongezeka kutoka visa vitatu kwa siku hadi visa vinane kwa siku.
Katika uvamizi mmoja dhidi ya kambi ya wakimbizi wa Palestina, na kombora la nadra katika eneo hilo, alhamisi ya Oktoba 12, vikosi vya Israeli viliwaua angalau watu 12, maafisa wa Palestina na polisi Israeli wanasema afisa mmoja aliuawa.
Kulikuwa na "hatari ya kweli" katika eneo hilo lililokaliwa "kutumbukia katika ghasia za kupindukia", Umoja wa mataifa umesema wiki hii.
Wakaazi wa Palestina katika ukingo wa magharibi wanasema wakati dunia inatazama janga linalojiri Gaza, walowezi wa Israeli wanatumia fursa kuingia vijijini na kuwatimua, n ahata kuwaua raia wa Palestina.
Katika visa vitatu, kwa mujibu wa kanda ya video na Ushahidi wa watu kutoka vijijini humo, Walowezi hao wamekuwa wakivaa magwanda ya kijeshi au wakindamana na wanajeshi wa Israeli wakati wa mashamabulio yao.

Chanzo cha picha, Getty Images
Msimu wa kuvuna zeituni ulianza juma lililopita katika eneo hilo, lakini wakazi wanaotegemea mavuno ili kupata kipato wanasema hawatokwenda misituni iliopo nje kidogo ya vijiji kutokana na hofu ya kupigwa risasi na walowezi.
Tayari kumeshuhudiwa ongezeko la mashambulio ya walowezi wa Israeli mwaka huu, hata kabla ya kufanyika shambulio la Hamas kwa mujibu wa data ya Umoja wa mataifa huku zaidi ya visa 100 vikiripotiwa kila mwezi na takriban watu 400 wakitimuliwa kutoka kwenye ardhi yao kati ya Januari na Agosti.
Shirika la kutetea haki za binaadamu la Israeli B'Tselem limeaimbia BBC kwamba tangu shambulio hilo, limenakili "mjumuisho na jitihada iliopangwa na walowezi kutumia sababu kuwa kuna angazio la kimataifa na ndani ya eneo hilo kwa kinachoendelea Gaza na kaskazini mwa Israel ili kunyakua ardhi katika ukingo wa magharibi".
BBC imeliuliza baraza la Yesha, shirika la walowezi katika ukingo wa magharibi na katika maeneo mengine, kutoa tamko kuhusu taarifa hizi lakini limekataa.
Moti Yogev, kaimu naibu kiongozi wa baraza la Binyamin ambalo pia linawakilisha walowezi katika eneo hilo, amesema walowezi wanaozusha ghasia "ni wa nje". "Iwapo wapo, wanastahili kuchukuliwa hatua kama ilivyo kwa wahalifu wengine wowote," alisema.
Jeshi na polisi ya Israeli hayakujibu maombi yetu mengi ya kupata tamko.
Hofu ya wapalestina wengi sasa ni kwamba hali katika ukingo wa magharibi itazidi kuwa mbaya. Waziri wa usalama wa ndani wa Israeli, Itar Ben Gvir, ametangaza wiki iliopita kuwa serikali itanunua bunduki kuwahami raia wa Israeli, wakiwemo walowezi katika ukingo wa magharibi – hatua ambayo inatishia kutofautisha kati ya walowezi waliojihami na wanajeshi katika eneo lililokaliwa.















