Zifahamu nchi 10 tajiri duniani

Countries

Chanzo cha picha, AFP

Mtu anaweza kuwa na jibu fulani kuhusu nchi hizi, lakini inaweza kuwa sio sahihi sana. Na je ni aina gani ya utajiri tunaouzungumzia? Lakini je kipimo ambacho hutumiwa kwa kawaida ni Pato la Taifa, au Pato la Taifa, ambalo linajumlisha uzalishaji wa bidhaa na huduma za nchi katika kipindi fulani na kuchukuliwa kama kiashirio cha kuonyesha utajiri wa eneo.

Ni mojawapo ya vipimo vinavyojulikana zaidi na kutumika katika Uchumi, na, miongoni mwa mambo mengine, inasaidia serikali kujua ni kiasi gani zitapokea katika kodi na, kwa hiyo, itajua ni kiasi gani zinaweza kutumia kwa huduma kama vile afya na elimu.

Kwa mujibu wa takwimu za Oktoba 2022 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa na Visual Capitalist, nchi hizo 10 tajiri duniani ni hizi hapa (angalia ikiwa kuna jambo la kukushangaza):

  • 10. Italia, yenye utajiri wa dola za Marekani bilioni 1.997
  • 9. Urusi - dola za Marekani bilioni 2.113
  • 8. Canada - dola trilioni 2.2
  • 7. Ufaransa - dola za Marekani bilioni 2.778
  • 6. Uingereza - dola za Marekani bilioni 3.199
  • 5. India - dola za Marekani bilioni 3.469
  • 4. Ujerumani - dola za Marekani bilioni 4.031
  • 3. Japan - dola za Marekani bilioni 4.301 Na sasa, ikipaa mpaka trilioni 14
  • 2. China - dola za Marekani bilioni 18.321
  • 1. Marekani - yenye Dola za Marekani 25,035

Lakini takwimu hizi zinamaanisha nini?

Wengine, wanaweza kusema hizi takwimu sio kila kitu, haimaanishi kitu. Kama baadhi ya wanaopinga kuhusu Pato la Taifa wanavyoonyesha, jambo muhimu hapa ni kuhusu taifa ama watu kwenye taifa husika.

Countries

Chanzo cha picha, Getty Images

Hata mgunduzi wake, mwanauchumi wa Marekani Simon Kuznets, hakujivunia hilo. Nia yake, katika miaka ya 1930, ilikuwa kutafuta njia ya kupima uchumi kwa ujumla ili kuwa na chombo cha kumsaidia kutoka katika Mdororo Mkuu.

Wazo lilikuwa kutathmini ni nini hasa kilikuwa na matokeo, yaani, kutafuta ni nini hasa kilileta ustawi. Lakini Vita ya pili ya dunia vilizuka na vipaumbele vilibadilika: jambo la haraka halikuwa ustawi bali maisha, na silaha zilihitajika kuyalinda.

Kwa mwanauchumi wa Uingereza mwenye ushawishi mkubwa John Maynard Keynes ilikuwa muhimu kujua ni nini uchumi unaweza kuzalisha na ni kiwango gani cha chini ambacho watu walihitaji kutumia, ili kujua ni kiasi gani kilichosalia kinaweza kufadhili vita. Aina nyingine ya hesabu ilihitajika, hivyo lengo la kipimo hicho lilibadilika. Na hivyo iliendelea kuwa.

Baada ya vita kumalizika, Marekani ilihitaji kujua jinsi wapokeaji wa misaada yake ya kujenga mataifa yao yaliyoathirika na vita wanaendelea, hivyo wote walianza kutumia Pato la Taifa (GDP0 kama kipimo.

Lakini baadaye chini ya Umoja wa Mataifa kikawa kinatumika kama kiwango cha kimataifa.

Countries

Chanzo cha picha, Getty Images

Kipimo cha 'kwa kichwa' au kwa mtu mmoja mmoja

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kipimo cha ustawi wa kiuchumi ambacho Kuznets walitaka kukitengeneza kiliishia kuwa kipimo cha shughuli katika uchumi. Tofauti ni kwamba kuna mambo mengi ambayo si mazuri kwa jamii lakini ni mazuri kwa uchumi, hivyo kuzalisha, kwa mfano, kitu ambacho kinaokoa maisha ya watoto ni sawa na kuzalisha risasi kwa silaha zinazowaua. Wala haipimi ubora, ni kiasi tu.

Unapolipia tiketi ya kupanda treni, kwa mfano, hiyo inahesabika katika hesabu ya Pato la Taifa, kisichohesabika ni ikiwa treni unayopanda ni chakavu, imejaza watu, huduma ni mbovu na chafu, au kama ni treni nzuri ambayo ilifika kwa wakati na inatunzwa vyema.

Kwa upande mwingine, haisemi chochote kuhusu mgawanyo wa mali: nchi inaweza kuwa na Pato la Taifa la juu lakini pia kusiwe na usawa. Angalia ni kwa kiasi gani orodha inabadilika ikiwa kipimo ni Pato la Taifa kwa kila mtu , ambayo hupima uhusiano kati ya mapato ya taifa (kupitia Pato la Taifa katika kipindi fulani) na wakazi wa eneo hilo.

Ingawa haionyeshi ukweli pia, inatoa -kulingana na wataalamu- angalau uhalisia wa ukaribu zaidi wa ustawi wa kijamii na kiuchumi. Kulingana na IMF (2023), nchi matajiri 10 kwa muktadha huo ni kama zifuatazo;

1. Luxembourg

2. Singapore

3. Ireland

4. Qatar

5. Macau

6. Switzerland

7. Norway

8. United Arab Emirates

9.Brunei

10. United States

Kuhusu nchi namba moja

Luxemburg, moja wapo ya nchi ndogo zaidi duniani, kwa suala la eneo na idadi ya watu, ndio nchi tajiri zaidi kwenye sayari kulingana na kipimo hiki.

Countries

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni kituo kikubwa zaidi cha benki duniani : zaidi ya benki 200 na uwekezaji mkubwa (1,000) unafanya kazi katika mji mkuu wake.

Ikiwa moja ya nchi zenye wafanyakazi wengi walioelimika na wenye ujuzi wa hali ya juu duniani, unaokidhi matakwa ya mashirika ya kimataifa, Luxemburg imetajirishwa na mseto wa viwanda na uchumi wa kuagiza na kuuza nje kulingana na huduma za kifedha.

Pia ina biashara ndogo na za kati, pamoja na sekta ndogo lakini yenye mafanikio ya kilimo. Utendaji wao wa hali ya juu unatokana na ukweli kwamba raia wa nchi jirani, kama vile Ufaransa, Ujerumani na Ubelgiji, wanafanya kazi huko lakini hawaishi nchini humo, kwa hivyo wanachangia ukuaji wa Pato la Taifa lakini hawajajumuishwa katika hesabu ya kila mtu.

Luxemburg huvutia wafanyabiashara wa kigeni kutokana na ushuru wa chini; kulingana na magazeti ya Le Monde na Süddeutsche Zeitung, asilimia 90 ya makampuni yaliyosajiliwa nchini humo yanamilikiwa na wageni.

Na wafanyakazi wake wanalipwa vizuri na ni watu wenye kipato cha juu zaidi.

Countries

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu na Utafiti wa Kiuchumi nchini Luxembourg, kima cha chini cha mshahara nchini humo ni dola za Marekani 2,488 kwa mwezi, hivyo mfanyakazi yeyote asiye na ujuzi anaweza kutegemea kiasi hicho.

Dola 14.40 kwa saa ni karibu mara mbili ya mshahara wa chini wa shirikisho wa dola $7.25 nchini Marekani, nchi ambayo inaongoza kwenye orodha ya kwanza ya juu kama nchi tajiri kwa kipimo cha GDP, na ni ya pili baada ya kima cha chini cha mshahara cha Australia ($14.54 kwa saa).

Mshahara wa wastani ni $5,380 kwa mwezi, lakini wataalamu wanaofanya kazi katika benki, kampuni za bima, tasnia ya nishati na teknolojia ya habari hupata zaidi ya hiyo.

Vipi kuhusu Amerika ya Kusini?

Naam, inabidi ushuke kidogo katika orodha hizi ili kupata nchi katika eneo la Amerika Kusini na Karibian.

Katika kipimo cha Pato la Taifa kwa kila mtu, nchi ya kwanza kuonekana ni Guyana ya Amerika Kusini, na kisiwa cha Karibean Aruba, kikifuatiwa na nchi nne Puerto Rico; Panama, Trinidad na Tobago, huku Chile na Uruguay zikitenganishwa kwa nafasi kadhaa.

Katika orodha ambazo nchi za Amerika ya Kusini zinaonekana katika 10 bora ni zile ambazo "Zina utajiri zaidi katika maliasili", huku Brazil na Venezuela katika utafiti huo zikiwa katika nafasi 7 na 10 mtawalia.