Vita vya Ukraine: Nato inavyofuatilia 'Zombies' za Urusi nchini Estonia

Scott MacColl anasema uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine umebadilisha mkondo wa operesheni ya kikosi chake.
Maelezo ya picha, Scott MacColl anasema uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine umebadilisha mkondo wa operesheni ya kikosi chake.

Katika chumba cha wanajeshi kilichosongamana, kwenye jumba linalokaribia eneo la ndege kupaa na kutoa katika kambi ya wanajeshi wa Amari nchini Estonia, televisheni inaonyesha msururu wa kipindi cha zamani cha Friends.

Miguu juu ya meza, vikombe vya kahawa mkononi, kelele za kawaida zinatawala chumba hicho. Kwenye skrini ya Runinga, Rachel amerudi tu kutoka kwa watengeneza nywele, Ross amekasirishwa na jambo fulani.

Kisha mfanyakazi wa ndege anainua kichwa chake karibu na mlango na kutangaza kwa utulivu: "Zombie inayoelekea kaskazini kutoka Kaliningrad."

Bila kupoteza muda watu wanasimama na kusogea karibu na Chumba cha Uendeshaji, ambapo skrini na ramani za kidijitali zenye alama ya "Siri ya Nato" inajitokeza na mitiririko ya data inayoingia.

Hiki ni Kikosi maalum cha oparesheni ya Azotize, ujumbe polisiwa Nato wa Polisi wa Anga wa Baltic ambao hulinda mipaka ya muungano huo wa kaskazini-mashariki ambapo ndege za Urusi huchunguza mara kwa mara mipaka ya eneo la Nato.

Tangu Aprili, Kikosi cha ndege za kivita za RAF IX Squadron kimechukua udhibiti wa misheni hiyo inayoongozwa kutoka Ujerumani, kihistoria ikijulikana kama Richthofen Squadron .

Uvamizi kamili wa Urusi dhidi ya Ukraine umelazimu muungano wa kijeshi wa Nato kuelekeza nguvu zake katika kulinda mipaka yake ya mashariki.

Lengo ni rahisi: kuzuia Urusi dhidi ya kuvamia mahali pengine popote, haswa nchi ya Nato kama moja ya mataifa matatu ya Baltic au Poland.

ROYAL AIR FORCE

Chanzo cha picha, ROYAL AIR FORCE

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

"Zombie" ni neno la siri linaloashiria ndege ya Urusi ambayo mienendo yake inatiliwa shaka.

"Neno hilo linaweza kuwa mojawapo ya mambo matatu," anaelezea Wing Cdr Scott MacColl kutoka RAF Lossiemouth huko Scotland. "Aidha haitakuwa imewasilisha mpango wa safari ya ndege, au hawakosi [kuwasiliana] au hawaitikii Udhibiti wa Trafiki ya Anga. Wakati inamaanisha yote matatu."

Katika halii hii inageuka kuwa ishara ya uwongo kwani Zombie inageuka kaskazini na mbali na mipaka ya Nato.

Uwanja wa ndege wa Amari wa Estonia, ambako ndege hizo zimewekekwa awali palikuwa eneo la Jeshi la Wanahewa wakati wa vita vya Soviet, na katika msitu wa karibu bado kuna makaburi ambapo marubani wa Sovieti wamezikwa pamoja na ndege za zamani za MiG-15 na MiG-17.

Leo misheni ya marubani hawa wa Nato ni ngumu na isiyo na huruma.

Huku Finland sasa ikijiunga na Nato, Bahari ya Baltic inapakana na wanachama saba wa muungano wa Magharibi, hivi karibuni kuwa wanane wakati njia itasafishwa kwa Uswidi kujiunga.

IF

Lakini Urusi bado ina maeneo mawili ya kimkakati katika eneo la Baltic: jiji lake la pili la St Petersburg upande wa mashariki na eneo lake la Kaliningrad, jiji la zamani la Prussia la Konigsberg na bara lake, mahali ambapo sasa kuna makombora na vifaa vingine vya kijeshi.

Ndege za kivita za Urusi aina ya Su-27 Flanker, Ndege za Amri na Udhibiti wa Anga na ndege za mizigo zote hupaa kila mara juu na chini ya Baltic kati ya kambi hizo mbili na kwingineko, na kuviweka vikosi vya anga vya Nato katika hali ya tahadhari kila mara.

"Kwa hivyo tunaweza kuketi hapo, kuweka miguu juu ya meza, tukinywa kikombe cha kahawa, na dakika inayofuata king'ora kinalia," anasema mmoja wa marubani wa Typhoon, ambaye ameomba jina lake lisitajwe.

"Tunaitikia ishara yoyote kana kwamba ni mpango wa kweli. Kwa hivyo tunakimbilia ndege, kutoa vifaa vyetu, kuchukua injini, kufungwa ndani, kuwasiliana na [Control] Tower, kuzungumza na Operesheni kwenye redio, kupata kibali chetu kisha tunatoka nje kwa teksi na kusafirishwa kwa ndege haraka tuwezavyo."

Marubani wa RAF wako tayari kupeperushwa hewani kwa ilani ya muda mfupi

Chanzo cha picha, RAF

Maelezo ya picha, Marubani wa RAF wako tayari kupaa anagani ndani ya muda mfupi

Kwa hivyo ni nini hasa hutokea wakati marubani wanakaribiana na Zombies hizi za Kirusi? Bila shaka hakuna mtu anataka kutangulia kudondosha makombora na kuanzisha Vita vya Tatu vya Dunia?

"Jukumu letu hapa ni kulinda anga ya Nato," anajibu Wing Cdr MacColl, akiongeza kwa mafumbo "Sheria zetu za kivita zimeainishwa".

Rubani mwingine anafafanua zaidi. "Hatujui ni ndege gani tutaenda kuzuia. Kwa hiyo tunasogea kando, tunatambua ndege na kisha tunapata maelezo zaidi, seti za ujumbe zaidi kutoka Kituo kikuu cha Operasheni na tunajibu kile wanachotuambia kufanya."

Ninachojua ni kwamba marubani hawa wa RAF wanapiga picha nyingi za Zombies, nzuri pia, wanapokuja pamoja na kuwasindikiza kupitia anga ya Nato.

"Tumefanya misheni nane ya kudhibiti mashambulizi," anasema Wing Cdr MacColl. "Zote hizo zimekuwa dhidi ya ndege za Urusi... Tumekuwa tukifanya ulinzi wa anga ya Baltic kwa miaka kadhaa lakini hakuna shaka kwamba uvamizi haramu wa Urusi nchini Ukraine mwaka jana umebadilisha hali ya mambo hapa."

Mambo yamebadilika chini, pia, ambapo kuna utaratibu mpya wa kuweka vikosi vya kutosha vya ardhi ili kuzuia uvamizi wowote wa baadaye wa Urusi.

Marubani wa Kisovieti wamezikwa pamoja na ndege zao za zamani za MiG-15 na MiG-17 kwenye msitu wa karibu.
Maelezo ya picha, Marubani wa Kisovieti wamezikwa pamoja na ndege zao za zamani za MiG-15 na MiG-17 kwenye msitu wa karibu.

Waziri Mkuu wa Estonia, Kaja Kallas, ambaye utotoni mwake alikulia katika Umoja wa Kisovieti, aliiambia BBC hakua na shaka kwamba ikiwa uvamizi wa Rais Putin nchini Ukraine hatimaye ungefaulu basi ingekuwa ni suala la muda tu kabla hajaelekeza malengo yake kwenye Mataifa mengine ya Baltic.

Kama sehemu ya sera ya Nato ya "uwepo kijeshi ulioimarishwa" katika mataifa hayo ya Baltic na Poland, kuna Kikundi cha vita cha kimataifa kinachoongozwa na Uingereza chenye makao yake huko Tapa kaskazini mwa Estonia.

Vifaru vya vita vya Challenger 2, Mifumo ya Roketi ya kurusha nyingi kwa wakati mmoja, helikopta za Wildcat na Apache na hata Kampuni ya Jeshi la Wanajeshi wa Kigeni wa Ufaransa zote zinakusudiwa kutumiwa kama kizuizi cha harakati zozote za Moscow.

"Changamoto ya Nato katika eneo la Baltic," anasema Brig Giles Harris, ambaye anaongoza Operesheni Cabrit, mchango wa Uingereza nchini Estonia, "ni kuzuia Urusi bila kuzua vurugu."