Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je unaweza kuzuia kuzeeka kwa kuishi kama 'mzee kijana'?
Wakati uzee unapoanza hutegemea mahali unapoishi duniani. Lakini pia inaweza pkutegemea kwa kiasi fulani jinsi unavyochukulia kuzeeka. Je, unaweza kuchelewesha uzee kwa mtazamo chanya?
Je, unadhani ni umri gani unaohesabika wastani wa umri wa kati? Ni miaka 40 hadi 60?, 50 hadi 70? ama ni mahali fulani hapo katikati?
Utafiti umebaini kuwa watu hutoa jibu ya swali hili kulingana na umri wao wakati wanapoulizwa.
Wakati watu nusu milioni walipokamilisha dodoso mtandaoni mnamo 2018 washiriki ambao walikuwa na miaka kati ya 20 na 30 walisema kuwa wastani umri wa kati ulianza miaka 40, huku uzee ulianza 62. Kwa upande mwingine, wale waliokuwa na zaidi ya miaka 65 walisema uzee unaanza mtu akiwa na umri wa miaka 71.
Kinachobainika hapa ni wazi kabisa. Hakuna mtu anayetaka kujifikiria kuwa anazeeka, kwa hivyo ukiwa na umri wa miaka 40 unafurahiya nakala zinazotangaza kwamba 40 ndio 30 mpya. Taswira hii pia inajitokeza kwa watu walio na umri wa miaka 70 na zaidi.
Pia, tunaelekea kutaka kujitenga na kundi lolote linalonyanyapaliwa. Hii ina maana kwamba tunakataa kuhusishwa na uzee, tunapowaonawazee wakionyeshwa kuwa wanyonge, wasio na utulivu, wagonjwa na hata mzigo kwa jamii.
Bila shaka, uzee ni jambo la kweli na wazee wanapaswa kuangaziwa kwa heshima na staha.
Kwa hiyo je, watu wanajidanganya ikiwa wanakataa kujiona kuwa wazee? Kwa kweli, inaweza kuwa mkakati wa busara, ambao unaweza kujitosheleza na kuboresha maisha. Mnamo 2003, watafiti Hannah Kuper na Sir Michael Marmot(maarufu kwa kuonyesha athari ambayo hali ya kijamii na kiuchumi maishani inaweza kuwa nayo kwa afya na matarajio ya maisha yetu) walifanya utafiti mpana ambapo washiriki waliulizwa tena swali: uzee unaanza lini?
Je miaka unayohusisha na kuanzia kwa uzee inawezaje kuwa na athari kubwa kwa afya yako?
Wazo moja ni kwamba jibu la swali la wakati uzee unapoanza hutoa maelezo mengi zaidi kuhusu mhusika kuliko unavyoweza kufikiria.
Huenda kwa mfano, swali hilo huwachochea watu kufikiria kuhusu afya yao ya kimwili, na ikiwa wana matatizo ya kiafya au mtindo mbaya wa maisha, wanaweza kufikiria hali hiyo inafanya uzee kuja mapema.
Wanaofikiria uzee ukuja baadaye maishani wanaweza kuwa na ufahamu zaidi kuhusu ya siha na maumbile yao.
Watu wanaosema uzee kwamba unaanza mapema maishani pia wanaweza kuwa na mtazamo mbaya wa maisha na uwezekano mdogowa kutafuta usaidizi wa kimatibabu au kutilia maanani muongozo wakiafya wikiamini kuwa kupungua kwa uwezo wa mwanadamu hakuwezi kuepukika.
Huenda, kwa mfano wakachukulia kwamba watu wazee ni wadhaifundiposa wanatembea polepole zaidi wakati hivi ndivyo wanapaswakufanya kwa ajili ya afya yao ya kiakili na kimwili.
Pia wakatarajia kusahau vitu kutokana na miaka yao, kwa hivyowanawacha kutegemea kumbukumbu zao. Aidha wanaweza kupata msongo wa mawazo kwa kuhisi kwamba uzee unachangia matatizo ya kiafya kwamuda mrefu. Kwa hivyo kuisha na kufikia miaka ya utu uzima kunawezakuongeza matatizo wanayoogopa.
Na yote haya yanaweza kuwa kweli kwa njia moja au nyingine.
Watu wanaofikiri uzee huanza baadaye maishani wanaweza kuwa na ufahamu zaidi kuhusu afya na siha zao na kwa hiyo kuchukua hatua madhubuti ili kubaki katika hali nzuri zaidi. Wanafikiri wao ni wachanga na hivyo wanaishi kama vijana.
Bila kujali maelezo, utafiti wa Kuper na Marmot sio utafiti pekee unaoonyesha faida zinazopimika za kufikiria vyema kuhusu kuzeeka.
Becca Levy kutoka Shule ya Yale ya Afya ya Umma, kwa kutumia data kutoka Utafiti wa Muda Mrefu wa Ohio wa Kuzeeka na Kustaafu, pia alitoa matokeo ya kushangaza.
Utafiti wa Ohio ulikuwa umeshirikisha zaidi ya watu elfu moja ambao walikuwa na angalau miaka 50 wakati huo.
Becca alibaini kuwa watu ambao walikuwa na mawazo chanya kuhusu kuzeekawaliishi kwa wastani miaka 22 na miezi sita baada ya kushiriki utafiti huo maraya kwanza.
Kwengineko watu waliokuwa mawazo hasi kuhusukuzeeka waliishi miaka 15 kwa wastani.
Watu ambao waliochukulia uzee kwa mtazamo chanya zaidi, wakati wa kujifunza vitu vipya na kupanga mipango mipya, kwa mfano na waliishi muda mrefu kwa wastani.
Tafiti hizi zote hazimaaishi tunaweza kuzuia au kurudisha nyuma mchakato wa kuzeeka.
Iwe ni uwezo wa kuona, kusika, kuwa na kumbukumbu, uimara wa misuli na mifupa au utaratibu wa kupona: vyote hivi vinapungua. Na watu walio na umri mkubwa wanakabilia na magonjwa tofauti.
Tafiti hizi kubwa zote zinategemea wastani, kwa hivyo kusema hujazeka hakutazuia kila mtu kuugua.
Lakini katika kitabu chake The Expectation Effect, mwandishi wa Habari za sayansi David Robson ameangazia vidokezo Fulani vinavyoweza kutusaidia. Anadokeza kwamba badala ya kusikitishwa na kifo cha ujana, tunapaswa kuzingatia uzoefu na ujuzi tunaopata tunapozeeka na kuona jinsi tunavyokuwa bora zaidi katika kushughulikia mambo .
Wazee wanapougua, hawafai kuhisi hali hiyo inatokana na umri wao mkubwa. Zaidi ya yote, hatupaswi kukata tamaa katika kujaribu kuwa na afya bora na kuamini kwamba bado kuna mambo mengi tunaweza kufanya. Tukichukua mtazamo huo, yaelekea tutaishi Maisha marefu na kufurahia miaka hiyo.