Wawindaji haramu hulenga viboko kutafuta meno yao makubwa kama mbadala wa pembe za ndovu

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuongezeka kwa vikwazo vya usafirishaji wa pembe za ndovu kumesababisha kuongezeka kwa biashara ya meno ya kiboko, wanaharakati wa wanyamapori wanaonya wa uwezekano wa madhara makubwa kwa spishi ambayo tayari imeorodheshwa kama "katika hatari ya kutoweka".
Wakati Uingereza ilipotangaza mwezi wa sita mwaka jana kuwa inapiga marufuku biashara ya pembe za ndovu, shirika la usaidizi la ustawi wa wanyama lilichunguza kile kilichotokea katika soko la mtandaoni.
"Tuligundua ongezeko la biashara ya pembe za ndovu nchini Uingereza ndani ya mwezi mmoja baada ya kutagazwa kwa marufuku ya pembe za ndovu kuanzishwa," anasema Frankie Osuch, mwandishi mkuu wa ripoti iliyotolewa na Born Free mwezi Septemba.
Hii ilikuwa "inayohusu sana ushahidi wa ongezeko la mahitaji ya pembe za ndovu kutoka kwa viboko, ambao idadi yao porini iko hatarini" ilisema ripoti hiyo.

Watafiti wanasema mtindo huu ulikuwa wazi tangu mwaka 1989, wakati marufuku ya kimataifa ya biashara ya pembe za ndovu ilikubaliwa kwa mara ya kwanza, na imeongezeka tu huku serikali zikileta hatua mpya za kuimarisha marufuku hiyo.
Kama pembe za ndovu, meno ya kiboko ambazo mara nyingi hutumiwa kwa michongo ya mapambo, lakini ni ya bei nafuu na rahisi kupatikana.
Sehemu za mwili wa kiboko bado zinaweza kuuzwa chini ya Mkataba wa Biashara ya Kimataifa katika Viumbe vilivyo Hatarini Kutoweka (CITES), ingawa mauzo yote ya kimataifa yanahitaji kibali cha kuuza nje.
Imehesabiwa kuwa kati ya mwaka 1975, wakati rekodi za CITES zilianza, na 2017, kilo 770,000 za meno ya kiboko ziliuzwa kisheria. Lakini pia kuna biashara haramu.
Mnamo 2020, meno ya kiboko yalikuwa kati ya sehemu za mwili wa mamalia ambazo mara nyingi hukamatwa katika EU, kulingana na ripoti ya Tume ya Ulaya.
"Kuna visa vya mbwa wanaonusa kubaini meno ya kiboko katika viwanja tofauti vya ndege barani Afrika siku hizi, na kugunduliwa hakumaanishi kuwa wote wamekamatwa, labda ni nusu tu," anasema Philip Muruthy, makamu wa rais wa Shirika la Wanyamapori la Afrika.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Utafiti wa Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) mwaka 2016 ulikadiria kuwa idadi ya kiboko duniani kote ilikuwa kati ya 115,000 na 130,000 - kushuka kwa 30% tangu 1994.
Nchi kumi za Afrika Magharibi na Kati zinasema kumeendelea kupungua kwa kasi kwa idadi ya wanyama hao, kutokana na ujangili na uharibifu wa ardhi.
Walipendekeza kupigwa marufuku kabisa kwa biashara katika maandalizi ya mkutano wa CITES huko Panama mwezi uliopita, lakini hii ingewezekana tu chini ya sheria za CITES ikiwa kungekuwa na kupungua kwa zaidi ya 50% ya idadi ya kibokokatika miaka 10 iliyopita, na. uchambuzi wa IUCN haukuunga mkono hitimisho hili.
Nchi 10 za Afrika Magharibi na Kati kisha zilipendekeza hatua inayoitwa "dokezo" ambayo ingesababisha upendeleo wa sifuri kwa vielelezo pori vinavyouzwa kwa madhumuni ya kibiashara.
Lakini pendekezo hili halikuungwa mkono na EU au na nchi za Afrika Mashariki na Kusini, ambazo zinasema idadi ya viboko inasalia katika kiwango kizuri.
Baadhi ya nchi za Afrika Mashariki na Kusini - Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe - pia ni chanzo cha robo tatu ya viboko wanaokadiriwa kufikia 13,909 ambao sehemu na bidhaa zao ziliuzwa kati ya 2009 na 2018.

Chanzo cha picha, Getty Images
Joanna Swabe, mkurugenzi mkuu wa masuala ya umma na Humane Society International, anadokeza kuwa kazi ndogo imefanywa tangu 2016 kuanzisha nambari za viboko.
"Kumekuwa na utafiti mdogo sana wa kisayansi juu ya idadi halisi ya viboko katika nchi hizi zote," anasema. "Wakati huo huo, nchi mbalimbali zinajua kinachoendelea na viboko hao ndani ya maeneo yao, hivyo haipaswi kupuuzwa."
Viboko wana kiwango cha chini cha kuzaliwa, huzaa mtoto mmoja tu kila mwaka, hivyo kupungua kwa idadi yao kunaweza kuwa na athari ya muda mrefu.
Ukweli kuhusu Kiboko
- Viboko wote wanaishi Afrika - kuna aina mbili ya viboko wa kawaida ambao idadi yao inakadiriwa kuwa 115,000 hadi 130,000 mwaka wa 2016 na kiboko anayefahamika kama pygmy ambao wako 2,000-3,000.
- Kiboko wa kawaida aliainishwa kuwa "katika hatari ya kutoweka" kwenye orodha ya wanyama wanaotoweka ya Muungano wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN) mwaka wa 2016.
- Sehemu na mazao ya viboko wanaokadiriwa kufikia 13,909 yaliuzwa kihalali kati ya 2009 na 2018 - robo tatu ya viboko hao walitoka Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
- Kilo 770,000 za meno ya kiboko yaliuzwa kihalali kati ya mwaka 1975 na 2017 - ukubwa wa biashara hiyo haramu haijulikani.
Wataalamu wa wanyamapori pia wanasema kuwa biashara halali na haramu ya meno ya kiboko inahitaji kufuatiliwa kwa karibu.
Kiboko wa kawaida ameorodheshwa katika Kiambatisho II cha CITES kumaanisha kwamba anaweza kutishiwa kutoweka isipokuwa biashara itadhibitiwa kwa karibu.
Nchi 10 zinazotaka kupigwa marufuku duniani kote kwa noti ya biashara zinasema kwamba kuna ushahidi dhabiti wa "kuchanganya pembe za ndovu halali na haramu", zikipendekeza kuwa pembe za ndovu zilizowindwa "zinauzwa katika soko halali".
Bila udhibiti thabiti, wanakampeni wanaonya, viboko wanaweza kushiriki hatima ya tembo, ambao wamekuwa hatarini - au walio katika hatari kubwa ya kutoweka kwa tembo katika misitu ya Afrika - kwa sababu wengi waliuawa na wawindaji haramu kwa ajili ya meno yao.








