Kwa nini DRC imepinga makubaliano ya vito vya thamani kati ya Rwanda na Umoja wa Ulaya?

g

Chanzo cha picha, JUTTA URPILAINEN/ X

Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta na Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Ulaya, Jutta Urpilainen, walitia saini makubaliano hayo mjini Brussels siku ya Jumatatu

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema imekataa makubaliano ya hivi majuzi ya Rwanda ya usindikaji wa madini na Umoja wa Ulaya (EU), ikisema ardhi ya Rwanda haina "madini yanayotafutwa zaidi duniani", kama vile coltan, cobalt, lithiamu na niobium.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Christophe Lutundula anasema uchunguzi wa taasisi mbalimbali likiwemo Bunge la Kongo na wataalamu wa Umoja wa Mataifa umeonyesha kuwa Rwanda inatumia njia za wahalifu na kampuni inayoitumia katika kuchimba madini na maliasili nyinginezo ambazo Kongo "inazo kwa wingi".

Serikali ya Rwanda inakanusha kuiba madini au maliasili ya Kongo. Inasema kwamba katika udongo wa Rwanda kuna vito vingi vya thamani, kama vile gesi, coltan, wolfram na dhahabu.

Wiki iliyopita, Wizara ya Madini, Mafuta na Gesi ya Rwanda ilitangaza kuwa mwaka 2023 sekta ya madini ilipata zaidi ya dola bilioni 1, ongezeko kutoka dola milioni 772 mwaka 2022.

Rwanda inasema inalenga kupata dola bilioni 1.5 kwa mwaka ifikapo 2024, kutokana na mauzo yake ya madini nje ya nchi.

Makubaliano hayo kati ya Rwanda na EU, yalitiwa saini Jumatatu ya wiki hii mjini Brussels, Ubelgiji, kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Vincent Biruta, na Jutta Urpilainen, Kamishna wa Umoja wa Ulaya kwa Ushirikiano wa Kimataifa.

Katika tovuti ya X, Waziri Biruta alisema kuwa Rwanda inavutiwa sana na makubaliano hayo ambayo yataleta "mustakhbali mwema na endelevu" kwa watu wa Rwanda na dunia nzima.

Kamishna Urpilainen alisema kuwa makubaliano hayo yanaanzisha "ushirikiano wa karibu" ambao utasababisha shughuli zaidi za kuongeza thamani katika uchimbaji madini.

Waraka wa Umoja wa Ulaya kuhusu makubaliano hayo unasema kuwa katika muda wa miezi sita ijayo pande hizo mbili zitaunda mpango wa ushirikiano wa kivitendo katika utekelezaji wa ushirikiano huo.

Hizi ni pamoja na kujenga miundombinu inayohusiana na uongezaji thamani wa madini, kuongeza mafunzo na maarifa, utafiti na uvumbuzi na kubadilishana maarifa na teknolojia.

EU inasema kutakuwa na hatua za kutambua asili ya madini, na ushirikiano wa kupambana na biashara haramu ya maliasili, na kufuata viwango vya kimataifa vya ulinzi wa mazingira.

'Si kazi nzuri hata kidogo'

f

Chanzo cha picha, CHRISTOPHE LUTUNDULA/X

Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Christophe Lutundula anasema nchi yake inatarajia "maelezo juu ya tabia hii ya kutatanisha" kutoka kwa EU.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa upande wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Waziri Lundula anasema, ingawa anatambua uhuru wa watia saini, makubaliano ya EU-Rwanda kuhusu uongezaji thamani wa maliasili muhimu zaidi "yawe hayana athari nyingine yoyote isipokuwa matumizi yake kwa sheria za maliasili za Kongo zilizotengenezwa na Rwanda".

Lutundula anasema kuwa uchumi wa Rwanda "unategemea uhalifu huo" na kwamba makubaliano na EU yanaipa rasilimali zaidi kuichokoza Kongo.

Alisema kuwa serikali ya Congo inachukulia kutiwa saini kwa mkataba huo "kama kitendo ambacho si rafiki hata kidogo", baada ya kutokea siku chache zilizopita wakati Rais wa Poland - nchi mwanachama wa EU - alipofanya ziara nchini Rwanda kuruhusu kutoa silaha katika kesi ya haja. Iwapo kutatokea na shambulio kutoka nje".

Aliongeza kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatarajia mamlaka ya EU kuipa "maelezo ya tabia hii isiyoeleweka wakati [EU] inaendelea kuthibitisha kwamba inataka kuchukua jukumu la kumaliza ukosefu wa usalama mashariki mwa Kongo na matumizi haramu ya maliasili yake. " , na kuimarisha ushirikiano" kati ya EU na Congo.

Katika mahojiano na Radio Okapi ya Umoja wa Mataifa nchini Congo, balozi wa Umoja wa Ulaya Nicolas Berlanga Martinez nchini humo alisema kuwa makubaliano ya Umoja wa Ulaya na Rwanda yatapelekea kuwepo kwa uwazi na kujua chimbuko la biashara yoyote ya madini.

Balozi Martinez aliongeza kuwa makubaliano hayo yatafaa sio tu katika eneo la Maziwa Makuu.

Ripoti ya wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi nyingi za Magharibi inaishutumu Rwanda kwa kuwasaidia waasi wa M23 dhidi ya serikali ya DRC, madai ambayo Rwanda inakanusha.

Ripoti hii pia inaishutumu DRC kwa kufanya kazi na kundi la waasi wa Rwanda wanaoendesha harakati zao mashariki mwa nchi hiyo (FDLR), ambayo inasema ni dhidi ya serikali ya Rwanda. DRC pia inakanusha madai hayo.

EU inasema kwamba makubaliano yaliyotiwa saini na Rwanda yanafuatia ule uliotiwa saini na DRC na Zambia mnamo Oktoba (10) mnamo 2023, na Namibia mnamo Novemba (11) mnamo 2022.

Nje ya Afrika, EU inasema tayari ina makubaliano na Argentina, Canada, Chile, Greenland, Kazakhstan na Ukraine juu ya uongezaji thamani ya maliasili.

Imetafsiriwa na Jason Nyakundi