Makabiliano DRC: Wasiwasi waikumba Goma huku kundi la M23 likipiga hatua

Idadi ya watu wa Goma imeongezeka siku za hivi karibuni huku watu wakiwasili kwa pikipiki na miguu wakiwakimbia wapiganaji wanaosonga mbele.

Chanzo cha picha, EPA

    • Author, Mayeni Jones na Samba Cyuzuzo
    • Nafasi, BBC

Emile Bolingo hana uhakika kuhusu muda ambao yeye na wakazi wengine wa mji wa Goma, uliopo mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wataweza kustahimili hali inayowakumba.

Mji huu mkuu na ambao ni muhimu katika eneo hili, ambalo lina wakazi milioni mbili, limekatizwa kwa siku kadhaa na maeneo ya mashambani ambayo ndio panapotokea chakula kinachowalisha wakazi wake.

Hii ndio hali ya hivi karibuni ya kuzuka kwa ghasia na mapigano ambayo yamewasababisha watu zaidi ya milioni saba kuwa wakimbizi wa ndani na kuhama makazi kwa sababu ya vita vya mara kwa mara.

Waasi kutoka kundi la M23 ambalo linaongozwa na jamii ya AbaTutsi wamefunga barabara mbili kuu zinazoingia na kutoka Goma kwa upande wa Kaskazini na magharibi na kutatitza hatua za kuingiza chakula mjini humo.

‘Tunaogopa kwamba tutakabiliwa na njaa ikiwa jeshi la DRC halitakomboa hata angalau barabara moja kati ya hizo mbili kuu hivi karibuni. Unaweza kuhisi hali ya wasiwasi ilivyojaa huku…watu wameogopa sana,’ Bolingo aliiambia BBC.

Mundeke Kandundao, ambaye ni mwendeshaji bodaboda, amefanyiwa upasuaji hivi karibuni baada ya kuathirika kwenye shambulizi la kombora.

 Mundeke Kandundao

Chanzo cha picha, GLODY MURHABAZI

Mji wa Sake uliopo kilomita 25 kaskazini magharibi mwa Goma, ulishhambuliwa jumatano iliyopita.

‘Nilipata jeraha kwenye kiuno, lililotokana na kukatwa na kipande cha kombora lililolipuka,’ Mundeke aliiambia BBC.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni mwendesha pikipiki za bodaboda amesema kwamba kombora lilirushwa na waasi kutoka kwenye kilima kilicho karibu na mji huo, siku ya jumatano.

‘Nilukuwa nimesimama nyuma ya kibanda na kulikuwa na watu wengi pale, n ani hapom ambapo kombora hilo lilipolipuka,’ alisema.

‘Tuna hofu na pia kuogopa, manake unavyoona, vita vinaendelea na havionekani kuwa na kikomo, n ani hali ambayo haina maana. Sisi tunausbiri kuona ikiwa vita vitakwisha ndiio turejelee maisha yetu ya kawaida na majumbani mwetu.’

Laurent Cresci kutoka shirika la kimataifa la mslaba mwekundu ICRC ameiambia BBC kwamba idadi ya wagonjwa katika hospitali ya Bethssheba iliyopi mjini Goma, iliongezeka maradufu siku hiyo ya jumatano: ‘Ilikuwa hali ya kupokea waathiriwa wengi. Kabla yah apo, tulikuwa na wagonjwa 80 waliolazwa kwenye wodi zetu, na sasa wako 130, kwa hivyo hali hii ni ngumu sana kuishughulikia.’

Kwa watu wengi yanayoshuhudiwa yanafanyika kama yaliwahi tena kushuhudiwa awali.

‘Ni kwa muda gani ambapo tutaishi hivi?’ Kila mara, tunajipata wakimbizi,’ Paschal Bashali aliiambia BBC baada ya kuwasili Goma. Watu wanaingia kwa foleni ndefu, kwa miguu au kwa pikipiki na kwenya mabasi.

Aline Ombeni amesema kwamba alikuwa katika hali ya kuhuzukishwa alipowasili mjini Goma: ‘Tumeondoka bila kitu, jinsi unavyotuona – bila chakula, nguo na tunahitaji makao ya kutuhifadhi na kupata chakula.’

Wapiganaji wa M23 wamejihami kwa silaha kali, ila kundi hilo limekanusha kutajwa kama kibaraka cha Rwanda.

Chanzo cha picha, AFP

Huku vita vikisogea karibu na Goma, kumbukumbu za 2012 ambapo wapiganaji wa M23 waliponyakua na kushika mji wa Goma kwa siku kumi, kabla ya shinikizo la jumuiya ya kimataifa kuwalazimu kusalimu amri na kuondoka.

Kundi hilo la M23 lilibuniwa kutokana na kundi jingine, lilianza kutekeleza shughuli zake mnamo 2012 likiwa na lengo la kuwalinda watu kutoka jamii ya AbaTutsi waliopo mashariki mwa DRC ambao kwa muda mrefu walilalamika kwamba walitengwa na kudhulumiwa.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesema kwamba kundi hilo linaungwa mkono na taifa la Rwanda, ambalo linaongozwa na jamii ya AbaTutsi, jambo ambalo Kigali imekanusha mara kwa mara.

‘Sote tunafahamu kwamba chanzo na sababu kuu ya vita hivi ni masuala ya kiuchumi. Rwanda, inaendeleza….kwa miaka 25 iliyopita….ufujaji wa madini na rasilimali zetu,’ alisema Patrick Muyaya, Waziri wa mawasiliano wa DRC katika mahojiano na BBC. Aidha ameiomba Uingereza kutumia ushawishi wake na Rwanda kudhibiti mambo.

Na sasa kuna hofu kwamba kundi la M23 ambalo limejiandaa kijeshi vyema, lina mipangilio inayofuatwa na wapiganaji wake ana ambalo pia limejihami kwa silaha kali na za kisasa kushinda makundi mengine ya wapiganaji, linaweza kunyakua mji wa Goma kwa mara nyingine.

Hivi maajuzi, Rais Felix Tshishekedi ambaye mwaka jana alichaguliwa tena kuhudumu kama kiongozi wa taifa hilo, aliwaambia wakazi wa Goma kwamba raia katika eneo hilo wanapaswa kuwa na Imani katika serikali yake kwamba haitokubali kamwe mji huo kuchukuliwa na waasi na kusisitiza kwamba majeshi yake yako katika hali ya ulinzi na wala sio ushambulizi.

‘Ukiona nguvu za kijeshi za M23, wanaweza kunyakua mji wa Goma ikiwa wanataka, lakini hatua hii inaweza kuleta changamoto nyingi,’amesema Onesphore Sematumba, mtaalamu na mchambuzi wa DRC kutoka shirika la International Crisis Group.

Waasi huenda wanaonyesha uwezo wao na pia ukirejelea yaliyojiri 2012 na makali ambayo jamii ya kimataifa iliwatolea baada ya kuunyakuwa mji huo wa Goma wakati huo.

Kilichojiri baada ya kundi hilo kuondoka Goma, lilikubwa na kushindwa makabiliano kadhaa dhidi ya jeshi la DRC ambalo liliungwa mkono na kikosi cha kimataifa cha kijeshi ambacho kiliwaondoa nchini DRC. Wapiganaji wa M23 wakati huo walikubali kujumuishwa kwenye jeshi la DRC kama hatua ya wao kukubali kuondoka vitani huku wakiahidiwa kwamba jamii ya AbaTutsi ingelindwa.

Ramani

Lakini 2021, kundi hilo lilirejelea vitani na kuchukua silaha zao upya , likisema kwamba ahadi ambazo zilitolewa zilikuwa zimevunjwa. Lilitokea kwenye miisitu iliyopo kwenye milima inayoweka mpaka wa DRC, Rwanda na Uganda na kukaribia mji wa Goma, wakinyakua maeneo kadhaa ya mashariki mwa DRC.

Hali ya kusitisha vita imekuwa ikiafikiwa katika makubaliano , lakini hata hii imekuwa ikivunjwa , huku pande zote mbili za serikali na kundi la m23 zikilaumiana.

M23 limekuwa likisema mara kwa mara kwamba liko tayari na linataka mazungumzo ya amanai na Kinshasa.’Tuliwaomba kufanya mazungumzo ili kutatua tatizo hili kwa amani,’alisema msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka katika mahojiano na BBC.

‘Makabiliano ya kila mara katika vita ….hayatoi suluhisho kwa chanzo cha kimsingi cha mzozo. Serikali ya DRC yenyewe haitaki hilo na inataka vita, na kuwaua watu hata zaidi.’

Rais Tshishekedi amesema awali kwamba mazungumzo, ni jambo ambalo halitawezenaka.

‘Ni muhimu kwamba jambo hili lieleweke wazi, kwamba sisi kama serikali hatutafanya majadiliano na M23. M23 si kundi ambalo lipo, ni Rwanda ambayo inatekeleza haya na kibaraka wake,’ Waziri wake wa mawasiliano aliiambia BBC.

Malefu ya watu wameshakimbia vijiji vyao kuishi katika kambi za muda; wengine wameanza safari tena ya kupata hifadhi salama.

Chanzo cha picha, Reuters

Mwaka jana, kikosi cha jumuiya ya Afrika mashariki kilikuwa ndani ya DRC kusaidikuwalinda rai ana kushika doria kwenye baadhi ya maeneo yaliyonyakuliwa na waasi na ambayo waasi hao waliyaondokea nchini humo kutokana na ombi la serikali.

Kuondoka kwa kikosi hicho cha EACRF mwezi Desemba, kulifuatia kusimamishwa kwa makuabaliano ya kusitisha makabiliano na kuzuka kwa mapigano yaliyohusu kundi la M23.

Rais Tshishekedi ana matumaini kwamba kikosi cha kijeshi kutoka jumuiya ya maendeleo ya mataifa ya afrika kusini SADC ambalo limewasili nchini humo hivi karinuni litakuwa na mafanikio makubwa na lina jukumu kuu la kuyashambulia makundi ya waasi.

Aidha ameiliomba kikosi kikubwa cha kijeshi cha umoja wa mataifa {MONUSCO} kuondoka. Kimekuwa na matatizo ya kutotakiwa kwa kukosa kudhibiti vita na kuvimaliza katika miaka 25 ambayo imekuwa ikihudumu ndani ya DRC.

Lakini kuna wasiwasi kwamba mzozo unaweza kuwa mbaya zaidi, hasa baada ya Rais wa DRC kutangaza vita dhidi ya Rwanda ikiwa makundi ya waasi watashmabulia tena.

Katika hali ya kujibu matamshi hayo, Rais wa Rwanda Paul Kagame, alipozungumza mnamo Januari alisema kwamba katika hali ya kuilinda taifa lake, watapigana kama watu ambao hawana chochote cha kupoteza.’

Wakati huohuo, Natalia Torrent, kutoka shirika la msaada la madaktari wasio na mipaka MSF ameonya kwamba jinsi ambavyo makabiliano yanavyokua makali katika maeneo tofauti na kwa maeneo kadhaa ya kivita , tangu katikati ya mwezi Januari inakuwa na athari mbaya kwa jamii ambayo tayari imekumbwa na hali ngumu.

‘Tuko katika eneo ambalo linashuhudia kusambaa kwa maradhi mbali mbali. Tayari tumekuwa tukishughulikia mlipuko wa kipindupindu, Ukambi na sasa tuna hofu kwamba wimbi jpya la milipuko na majanga yatazuka upya tena,’ aliiambia BBC.

Akiangazia makabiliano, mkazi wa Goma Bolingo alisema pia : ‘Ni sisi ambao tunathirika na kuhangaika.’

Bashali ambaye alikimbia mji wa Sake akiwa na mke wake na watoto wao tisa, amekiri kwamba : ‘Wanaume wanakufa, watoto na wanawake pia, nao wanafariki, na kwa sababu gani? Tunaomba kwamba taifa letu liwe na amani.’

Taarifa zaidi : Glody Murhabazi, mwandishi wa Habari kutoka Goma.

Imetafsiriwa na Laillah Mohammed na kuhaririwa na Lizzy Masinga.