Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 16.03.2023

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, atapewa ofa ya euro milioni 220 (£193m) kwa mwaka ili kuhamia klabu ya Saudi Arabia mkataba wake wa Paris St-Germain utakapokamilika msimu wa joto. (Marca kwa Kihispania)
Mshambulizi wa Manchester City Julian Alvarez, 23, anatazamiwa kusaini mkataba mpya ambao utamweka mshindi huyo wa Kombe la Dunia la Argentina Etihad hadi 2028. (Mail).
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba anataka kusalia Juventus msimu ujao, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kucheza kwa dakika 35 tu kwenye ligi ya Serie A msimu huu kwa sababu ya majeraha. (90 Min)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Barcelona Xavi Hernandez tayari amezungumza na kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 32, kuhusu uhamisho. Mkataba wa Gundogan huko Manchester City unamalizika majira ya joto. (AS - kwa Kihispania)
Borussia Dortmund huenda ikampa winga wa kimataifa wa Ujerumani Julian Brandt, 26, kandarasi mpya katika jitihada za kuzuia nia ya Arsenal na Tottenham. (Bild ya Michezo - kwa Kijerumani)
Manchester United wanaweza kuwasilisha ofa ya pauni milioni 105 kumnunua mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt na Ufaransa Randal Kolo Muani, 24. (Sport Bild - kwa Kijerumani)

Chelsea wana nia ya kumsajili Manu Kone wa Borussia Monchengladbach huku kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 akivutia pia Paris St-Germain. (Sun)
The Blues wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa kimataifa wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 27, msimu huu wa joto na klabu tano za Premier League, pamoja na AC Milan na Roma zinazowania. (Football Insider)
Mshambulizi wa Ufaransa Karim Benzema, 35, ameripotiwa kukubali kusaini mkataba mpya na Real Madrid. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Chanzo cha picha, Getty Images
West Ham wanatazamia kumnunua mshambuliaji wa Werder Bremen na Ujerumani Niclas Fullkrug, 30. (Sport Bild via Sport Witness)
Newcastle, Aston Villa, Wolves na Leeds wana nia ya kumsajili beki wa pembeni wa kimataifa wa Ureno Raphael Guerreiro, 29, mkataba wake na Borussia Dortmund utakapokamilika msimu wa joto. (Dakika 90)
Fulham wanamfuatilia kiungo Mfaransa Edouard Michut, 20, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Sunderland kutoka Paris St-Germain. (Fabrizio Romano)














