Dada waimbaji wa Afghanistan wanaokaidi Taliban

Dada hao wamepata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo cha picha, Kawoon Khamoosh

Maelezo ya picha, Dada hao wamepata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii. Hapa, walikuwa wakirekodi moja ya nyimbo zao za hivi punde
    • Author, Kawoon Khamoosh
    • Nafasi, BBC 100 Women

Wakati ulimwengu ulipokuwa ukishuhudia kurejea kwa Taliban madarakani mwezi Agosti 2021, dada wawili mjini Kabul walikuwa miongoni mwa mamilioni ya wanawake nchini Afghanistan ambao walihisi moja kwa moja utawala mpya ukiwabana.

Waliamua kwamba wasingeweza tu kusimama nyuma na kutazama, na kuanza kwa siri kutumia nguvu ya sauti zao kupinga.

Wakijiweka katika hatari kubwa, walianza harakati za uimbaji kwenye mitandao ya kijamii zijulikanazo kwa jina la Last Torch.

"Tutaimba lakini hatua hii inaweza kutugharimu maisha yetu," mmoja wao alisema kwenye video iliyorekodiwa, kabla ya kuanza wimbo huo.

Ilitolewa mnamo Agosti 2021, siku chache tu baada ya utekaji nyara wa Taliban, na kuenea haraka kwenye Facebook na WhatsApp.

Bila ujuzi wowote wamuziki, akina dada - wanaovaa burka ili kuficha utambulisho wao - wakawa waimbaji muziki maarufu.

"Harakati zetu zilianzia kulia chini ya bendera ya Taliban na dhidi ya Taliban," anasema Shaqayeq (si jina lake halisi), mwanachama mdogo wa wawili hao.

"Kabla ya Taliban kuingia madarakani, hatukuwahi kuandika shairi hata moja. Hivi ndivyo Taliban walitufanyia."

Last Torch inaongozwa na dada wawili wanaopingaTaliban

Chanzo cha picha, Last Torch

Maelezo ya picha, Last Torch inaongozwa na dada wawili wanaopingaTaliban
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Baada ya kurejea madarakani, ilichukua Taliban chini ya siku 20 kutekeleza maono yake ya kipekee kwa Afghanistan.

Kuweka Sharia (sheria ya dini ya Kiislamu) katika maisha ya kila siku na kuwawekea vikwazo wanawake kupata elimu ni miongoni mwa vipaumbele vyao. Wanawake waliingia katika mitaa ya Kabul na miji mingine mikubwa kupinga, lakini walikabiliwa na ukandamizaji mkali.

"Wanawake walikuwa nuru ya mwisho ya matumaini ambayo tunaweza kuona," anasema Shaqayeq.

"Ndio maana tuliamua kuendeleza pambano letu pamoja nao na kujiita Last Torch au Mwenge wa Mwisho. Kwa kufikiria kuwa hatutaweza kwenda popote, tuliamua kuanzisha maandamano ya siri kutoka nyumbani."

Hivi karibuni wawili hao walitoa nyimbo zingine, zilizoimbwa kutoka chini ya burkas ya bluu, kama wimbo wa kwanza ulivyokuwa.

Moja lilikuwa shairi maarufu la marehemu Nadia Anjuman, ambaye aliliandika kupinga unyakuzi wa kwanza wa Taliban mnamo 1996.

Nawezaje kuzungumzia asali wakati kinywa changu kimejaa sumu?

Oh mdomo wangu umepigwa gumi ya kikatili ...

Kuna siku ambayo nitavunja ngome,

Kuachana na kutengwa huku na kuimba kwa furaha

xx

Chanzo cha picha, Haroon Sabawoon/Anadolu/Getty Images

Maelezo ya picha, Wanawake wakiandamana

Taliban walipopiga marufuku elimu ya wanawake, Nadia Anjuman na marafiki zake walikuwa wakikutana katika shule ya chinichini, The Golden Needle, ambapo walijifanya kuwa wanashona lakini badala yake walikuwa wakisoma vitabu. Wao pia walivaa burka ya buluu, inayojulikana kama chadari nchini Afghanistan.

Mkubwa kati ya dada hao wawili waimbaji, Mashal (pia ni jina bandia), analinganisha burka na "'ngome inayotembea".

"Ni kama makaburi ambapo ndoto za maelfu ya wanawake na wasichana huzikwa," anasema.

"Burka hii ni kama jiwe ambalo Taliban waliwarushia wanawake miaka 25 iliyopita," Shaqayeq anaongeza. “Na walifanya hivyo tena waliporudi madarakani.

"Tulitaka kutumia silaha waliyotumia dhidi yetu, kupigana dhidi ya vikwazo vyao."

Mmoja wa dada hao
Maelezo ya picha, Akina dada hao hutumia burka zao kuficha utambulisho wao

Dada hao wametoa nyimbo saba pekee kufikia sasa lakini kila moja imewavutia sana wanawake kote nchini. Kwa kuanzia walitumia maneno ya waandishi wengine, lakini walifikia hatua "ambapo hakuna shairi lingeweza kueleza jinsi tulivyohisi," Shaqayeq anasema, hivyo wakaanza kuandika yao.

Nyimbo zao ziliangazia maisha ya kila siku ya wanawake, kufungwa kwa wanaharakati na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mashabiki wamejibu kwa kushiriki nyimbo zao kwenye mitandao ya kijamii. Katika baadhi ya matukio pia wamevaa burka kama njia ya kujificha, wakati kundi moja la wanafunzi wa shule wa Afghanistan wanaoishi nje ya nchi wapolirekodi toleo kwenye jukwaa katika ukumbi wa shule.

Hii ni kinyume na kile ambacho Taliban walitaka kufikia.

Moja ya hatua zake za kwanza baada ya kurejea madarakani ilikuwa ni kuibadilisha Wizara ya Masuala ya Wanawake na kuchukua nafasi ya Wizara ya Kueneza Utu wema. Wizara hiyo mpya haikulazimisha uvaaji wa burka pekee, bali pia imeshutumu muziki kwa madai ya kuharibu mizizi ya Uislamu.

"Kuimba na kusikiliza muziki kuna madhara makubwa," alisema Sawabgul, afisa aliyeonekana kwenye video moja ya propaganda za wizara hiyo. "Inawakengeusha watu kutoka kwa maombi ya Mungu ... Kila mtu anapaswa kukaa mbali nayo."

Hivi karibuni kulikuwa na video za askari wa miguu wa Taliban kwenye mitandao ya kijamii, wakichoma ala za muziki na kuwaonyesha wanamuziki waliokamatwa.

XX

Chanzo cha picha, Bakhter News Agency

Maelezo ya picha, Maafisa wa Taliban wanaonekana hapa wakichoma ala za muziki

Muda wote Shaqayeq na Mashal waliendelea kuachia nyimbo kutoka nyumbani kwao Afghanistan walikuwa wanahatarisha maisha yao.

Shaqayeq anasema amekosa usingizi usiku mwingi akikihofia kwambaTaliban wanaweza kuwatambua.

“Tumeona vitisho vyao kwenye mitandao ya kijamii: ‘Tukikupata tunajua jinsi ya kuutoa ulimi wako kooni,” anasema Mashal.

"Wazazi wetu wanaogopa kila wanaposoma maoni haya. Wanattusihi huachane na kazi yetu... Lakini tunawaambia hatuwezi, hatuwezi kuendelea na maisha yetu ya kawaida."

Kwa usalama wao, dada hao waliondoka nchini mwaka jana lakini wanatarajia kurejea hivi karibuni.

XX
BBC 100 Women logo