Jinsi ya kugundua ulaghai wa ofa za kazi kwenye WhatsApp na nini cha kufanya ili kuziepuka

Chanzo cha picha, Getty Images
Na Dario Brooks
BBC News World
Ujumbe wenye nambari kutoka nchi isiyojulikana na unaotoa mapato kwa kazi rahisi, pia ulifika kwenye WhatsApp ya David Guzmán.
Kama ilinavyotokea kwa maelfu ya watu duniani, aina hizi za ujumbe zilibadilika kwa kiasi fulani: "Mara kadhaa nilipokea ujumbe kutoka nambari nisiyoijua, kutoka Uchina au ," Guzmán anaiambia BBC.
"Siku moja nilisema, 'Sawa, nini kinaweza kutokea'. Ujumbe unasema kwamba wanakualika kufanya kazi kwenye jukwaa katika mji wa Wuhan, Uchina, na wanataja mtandao wa kijamii, sawa na TikTok ," anaelezea miaka 24.
Kazi ilijumuisha sharti la "kupenda" video na kutuma picha ya skrini kama uthibitisho. Kwa kufanya hilo ungepata malipo kwa akaunti yako ya benki.
"Kisha nikasema 'Ni sawa kuweka likes chache , sawa? Ni nini kibaya zaidi kinachoweza kutokea?'
Kwanza walimpa pesa sawa na dola 6 za Kimarekani kwa ajili ya kukamilisha "kazi" alizokabidhiwa na mtu aliyewasiliana naye upande wa pili wa simu, ambaye alitumia lugha ya Kihispania kisicho sahihi, ni kana kwamba alitumia tafsiri ya mtandaoni.
"Inashangaza sana kuzungumza nao," anasema Guzmán. Waliomba maelezo ya akaunti ya benki ili wafanya malipo.
"Walinitumia tuzo ya kwanza na kuniambia kuwa nilikuwa nafaa kwa kazi hiyo. Walinipa chaneli ya Telegraph. Na haikuwa mimi tu, bali tulikuwa washiriki 500. Ni vikundi vikubwa sana," anakumbuka.

Chanzo cha picha, DAVID GUZMAN/BBC
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Lakini kazi ilianza kuwa ya ajabu. Mbali na kumpa kazi mbili za "kupenda", walimtaka afanye kazi ya tatu: kuwekeza pesa zilizopatikana katika kile kinachofahamika kama jukwaa la pesa za kidigitali (cryptocurrency) .
"Niliendelea na likes na katika mpango huu wanakufanya uhisi unashinda vitu, kana kwamba unafanyia kazi hii. Nadhani hapo ndipo mchezo ulipo, kichocheo cha akili kwa watu unaowafanyia kazi. Imejaa emoji na ujumbe wa motisha kwenye Telegram," anafafanua.
Kisha wakamwomba aingie "ngazi inayofuata" ya "kazi" hii, ambayo alipaswa kuwekeza zaidi. Walimwomba karibu dola 60 za Marekani kuingia. Guzmán anasema ilimbidi kukopa pesa kutoka kwa marafiki ili kufanya malipo.
“Umeshinda!” wakajibu. Lakini ili kupokea ushindi wake, ilimbidi kuweka dola nyingine 12 za Marekani. Tayari zilikuwa zimetumwa pesos 1,200, au karibu dola 70 za Marekani.
"Niliwatumia pesa walizoniambia na ilichukua [mawasiliano ya mtu ] kunijibu kama dakika 3. Hiyo ilionekana kama saa moja na kwamba nilikuwa nimepoteza pesa," Guzmán anakumbuka.
Lakini hapana, walituma takriban dola 110 kwenye akaunti yake. "Nilikuwa na takriban 1,900 [pesos] kwenye akaunti na nilirudisha nilichokuwa nimekopa na kubakiwa na takriban 900."
Na alichagua kutoendelea tena na "kazi" au kuwekeza tena pesa mpya ambazo zilionyeshwa kwake. "Walisisitiza kwamba nitume angalau nusu yake katika , mawasiliano yakiwa kwa lugha ya Kihispania ambacho kilitafsiriwa vibaya," anakumbuka.
Wizi mbali mbali
Uzoefu wa Guzmán ni sehemu ya ulaghai mbalimbali unaoenea kwenye majukwaa kama vile WhatsApp.
Takriban zjumbe zole, lengo la kwanza ni kwa mtu anayepokea ujumbe kuangukia kwenye ndoano na kujibu aina hiyo ya ujumbe.
Aina nyingine za kashfa ni pamoja na utoaji wa kazi katika makampuni maalumu , na mishahara ya kuvutia sana, kwa lengo la kupata taarifa nyingi kuhusu mtu iwezekanavyo.
Data hii inaweza kutumika kwa njia mbili: moja ni wizi wa utambulisho , kwa kuwa walaghai tayari wameweza kupata taarifa nyingi nyeti za kibinafsi ambazo zinaweza kutumika katika kufanya miamala ya fedha, kama vile kuomba mkopo au kufikia akaunti ya benki ya muathiriwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Matumizi mengine ya data hii ni uuzaji wake kwa kampuni zinazotumia metadata hiyo kwa madhumuni ya utangazaji au uuzaji.
"Hapo awali ilikuwa kubofya ofa tu, na kukupeleka kwenye tovuti ya ulaghai, ambayo ilijifanya kuonekana kama tovuti rasmi, ili kuiba data yako. Sasa ni motisha," anaeleza mtaalamu wa usalama wa mtandao Verónica Becerra, kutoka kampuni ya Offensive Hacking & Security Networks.
"Unafanya hivyo na wanakupa pesa, lakini unapoanza kupanda ngazi, ngazi ya tatu, wanaanza kukutoza ili upate pesa zaidi. Na hapo ndipo ulaghai unakuja," anaongeza.
Ingawa sio waathiriwa wote wanaokabidhi pesa nyingi, wahalifu wa mtandao hutegemea watu wachache tu kufikia viwango vya juu vya mpango wa kupata nyara nzuri.

Kampuni kubwa kwa kawaida haziwasiliani na watu kupitia ujumbe wa WhatsApp au kwa njia ya nambari katika nchi za mbali.
Utekelezaji wa zana mpya za akili Mnemba au akili bandia (AI) pia umezalisha aina mpya za ulaghai.
Mtumiaji wa WhatsApp (au mifumo mingine) anapojibu Video kutoka kwa nambari isiyojulikana, sura yake inaweza kurekodiwa na kisha kutumika kwa njia ya siri .
Kupitia hilo, walaghai wanaweza kuifanya ionekane kama mtu huyo anasema jambo ambalo hajawahi kusema.
Wahalifu wa mtandao wanaweza kupora pesa kutoka kwa watu wanaowasiliana na muathiriwa au kuwauliza pesa katika za uongo katika nyakati za dharura.
"Nilijua kisa kwamba wakati wa kujibu simu ya video kwa mtu walicheza video ya watu wazima, na kuifanya ionekane kuwa mtu huyu alikuwa akiitazama kisha wakamnyang'anya ," anasema Becerra.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jinsi ya kuepuka wizi ?
Kwa mtaalamu wa usalama wa mtandao, WhatsApp ni mojawapo ya njia zinazotumiwa sana kwa uhalifu huu, si kwa sababu jukwaa lenyewe lina udhaifu wa kiusalama, lakini kwa sababu ndilo linalotumiwa zaidi duniani na watumiaji zaidi ya bilioni 2. Na hii ina maana kwamba kuna ulimwengu mkubwa wa waathirika iwezekanavyo.
Hata hivyo, jambo la kwanza ili kuepuka hatari zinazowezekana ni kusasisha programu kama hizi na matoleo mapya zaidi, kwa kuwa kunaweza kuwa na mianya mipya ya hatari kwa usalama.
La muhimu hata usijibu simu kutoka nambari za simu zisizojulikana , kwa sababu kwa maswali machache watajaribu kupata habari nyingi za kibinafsi iwezekanavyo.
"Wakati huo tayari wana data za kutosha kukuhusu, taarifa za benki, taarifa za anwani, mambo mengi," anaonya Becerra.
“Nilichoona ni kwamba vijana wadogo hawajali taarifa zao zikiibiwa, kwenye mitandao ya kijamii wanafikia hatua ya kusema ‘Haijalishi, kwa sababu tayari wamenipa pesa nyingi sana najua ni kiasi cha pesa ambacho kinaweza kupatikana kwa baadhi ya data,” anaongeza.
"Kwa watu wazima tatizo linabadilika na kuwa habari potofu na ufahamu mdogo wa aina hii ya zana. Ndio maana wahalifu wa mtandao huitumia fursa hiyo."
Vyovyote vile, makampuni kwa kawaida hayatawasiliana na waombaji kazi kupitia WhatsApp. Na inakuwa ni nadra zaidi iwapo mtu huyo hajawahi kuomba nafasi hiyo.
Na ikiwa uliomba kazi hiyo kweli au una nia ya kuiomba, inashauriwa kupiga simu moja kwa moja kwenye kampuni na kuuliza rasmi juu ya ujumbe au nia yao ya kukupatia kazi.
Makampuni makubwa hayatumii nambari zilizo na viambishi vya ajabu vya kimataifa au akaunti za barua pepe katika huduma za wingi (Gmail, Outlook au zingine).

Chanzo cha picha, PA AVERAGE
Ushauri mwingine ni kuwezesha uthibitishaji maradufu kwa akaunti ya WhatsApp au mifumo mingine, ambayo huzuia mlaghai kujaribu kuiba akaunti kupitia wizi wa utambulisho. "Ni safu ya ziada ya ufikiaji wa jukwaa lako."
Joshua Breckman, msemaji wa Meta (kampuni mama ya WhatsApp), anaieleza BBC Mundo kwamba usimbaji fiche wa mwisho hadi mwisho wa gumzo kwenye jukwaa hauruhusu kampuni kukagua yaliyomo kwenye mazungumzo ili kugundua ulaghai.
Lakini anapendekeza watumiaji wasome mwongozo ambao WhatsApp imetayarisha kuhusu ulaghai na kufuata maagizo ili kuripoti nambari zinazotiliwa shaka katika kiungo hiki .

Chanzo cha picha, PA AVERAGE
Becerra pia anasema kuwa inashauriwa kutokuwa na taarifa nyeti kwenye gumzo, kama vile picha za vitambulisho, nywira za siri za akaunti za huduma au data za kibinafsi, kwa kuwa wahalifu wa mtandao kwa kawaida hutafuta aina hii ya taarifa kwenye mazungumzo.
Na ingawa ni muhimu kuwa na chelezo ya historia yako katika iCloud, lazima uwe na manenosiri (nywila) thabiti katika huduma hizo (Hifadhi ya Google, iCloud au nyinginezo).
Ikiwa umeifunga kwa uthabiti programu yako, walaghai wanaweza pia kupata taarifa za kibinafsi za muathiriwa wanayemtafuta hapo.
Na ikiwa wizi wa habari tayari umetokea, inashauriwa pia kwenda kwa polisi wa mtandao wa eneo lako "ili kuacha rekodi, ikiwa kuna uhalifu mkubwa," anasema Becerra.
"Pia unapaswa kuepuka kutoa habari nyingi katika mazungumzo, hata kwa mawasiliano," anaongeza.
"Si mara zote hujui kwa hakika ni nani aliye upande mwingine."
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Yusuf Jumah












