Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 22.06.2023

Rice

Chanzo cha picha, PA Media

Manchester United wameungana na Arsenal kutika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, 24, kutoka West Ham, huku Red Devils wakizingatia mkataba wa mchezaji pamoja na pesa inayomhusisha mlinzi wa Uingereza Harry Maguire, 30, au kiungo wa Scotland Scott McTominay, 26. (Telegraph - usajili unahitajika)

West Ham wana nia ya kumleta McTominay kwenye klabu iwapo Rice ataondoka. (Talksport)

Newcastle United wanakaribia kufikia makubaliano ya pauni milioni 60 kumnunua kiungo wa AC Milan na Italia Sandro Tonali, 23. (Athletic -usajili unahitajik)

Sandro Tonali

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa AC Milan na Italia Sandro Tonali

Manchester City pia wanamyatia Rice, huku West Ham wakipendelea dili ambalo lingemfanya kiungo wa Uingereza Kalvin Phillips, 27, kuhamia London Stadium. (ESPN)

Kiungo wa kati wa City na Ureno Bernardo Silva, 28, anakaribia kuhamia Saudi Arabia. (Marca kwa Kihispania)

Bayern Munich wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 31, kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto, huku Newcastle ikimtaka. (Bild - kwa Kijerumani)

Sadio Mane akiwa Bayern

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sadio Mane akiwa Bayern

The Magpies pia wanataka kumsajili Ruben Neves, 26, kwa mkopo baada ya kiungo huyo wa Ureno kukubali kujiunga na Al Hilal kutoka Wolverhampton Wanderers kwa £47m wiki hii. (Football Insider)

Mshambulizi wa Tottenham na England Harry Kane, 29, bado ana matumaini ya kuhamia Manchester United msimu huu wa joto. (Mirror)

Spurs wamekubali mkataba wa pauni milioni 17.2 kumsaini kipa wa Italia Guglielmo Vicario, 26, kutoka Empoli. (Sky Sports)

Harry Kane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Harry Kane bado ana matumaini ya kuhamia Manchester United msimu huu

Manchester United na Bayern Munich wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt na Ufaransa Randal Kolo Muani, 24. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

The Red Devils wanafikiria kumnunua kipa wa Inter Milan wa Cameroon, Andre Onana, 27. (Sky Sports Italy - kwa Kitaliano)

Burnley wanatazamiwa kumsajili beki wa Jamhuri ya Ireland Dara O'Shea, 24, kutoka West Bromwich Albion. (Irish independent)

Bournemouth wanakaribia kukamilisha dili la £9.5m na Roma kwa ajili ya kumnunua mshambulizi wa Uholanzi Justin Kluivert, 24. (Talksport)

Andre Onana

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Andre Onana tayari amebeba kombe la Coppa Italia katika msimu wake wa kwanza akiwa na Inter Milan

Brentford wamepiga hatua katika mazungumzo ya kumsajili beki wa Jamhuri ya Ireland Nathan Collins, 22, kutoka Wolves. (Sky Sports)

Kiungo wa Bayern Munich na Uholanzi Ryan Gravenberch, 21, amesema huenda akalazimika kuhama ili kupata muda zaidi wa kucheza, na yuko tayari kujiunga na Liverpool. (Mirror)

Juventus wamempa kiungo wa Ufaransa Adrien Rabiot, 28, mkataba mpya kabla ya mkataba wakewa sasa kukamilika mwezi Julai, lakini angependelea kuhama Ligi ya Premia, huku Manchester United na Newcastle zikivutiwa. (Foot Mercado - Kwa Kifaransa)

Adrien Rabiot

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Adrien Rabiot anataka kuhamia Ligi ya Premia licha ya Juventus kumpa mkataba mpya.

Kiungo wa Italia Jorginho, 31, anataka kusalia Arsenal licha ya Lazio kuonyesha nia ya kuta kumsajili. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Chelsea na Morocco Hakim Ziyech, 30, anakaribia kuhamia Al-Nassr kwa pauni milioni nane. (Standard)

Kiungo mwenza wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 22, pia anaweza kuondoka kuelekea Saudi Arabia huku klabu mbili za Pro League zikimhitaji mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Usajili unahitajika)

Hakim

Chanzo cha picha, Getty Images