Dirisha la Uhamisho: Ni uhamisho gani mkubwa unaweza kutokea siku ya mwisho?

EF

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Dirisha la usajili la majira ya kiangazi linafungwa Ijumaa, huku uuzaji na ununuzi wa wachezaji ukiwa bado unaendelea kufanywa na klabu zinatazamia kukamilisha vikosi vyao kwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa uchambuzi kutoka Football Transfers, klabu za ligi kuu Uingereza zimetumia zaidi ya pauni bilioni 1.7 kufikia sasa, pungufu ya pauni milioni 600 ya mwaka 2023.

Pia unaweza kusoma

Muda na Kanuni za uhamisho

Dirisha la uhamisho litafungwa saa 05:00 usiku, siku ya Ijumaa kwa Ligi Kuu England, English Football League na Scotland.

Ulaya dirisha la Bundesliga litafungwa saa 01:00 usiku, Ligue 1 04:00 usiku na katika Serie A na La Liga ni 05:00 usiku saa za ndani.

Dirisha la uhamisho la Ligi ya Wanawake ya Super League bado liko wazi hadi saa 05:00 usiku saa za ndani, tarehe 13 Septemba.

Wakati mwingine mikataba haiko moja kwa moja na huenda isikamilike kabla ya tarehe ya mwisho. klabu huhitimisha mikataba katika dakika za mwisho.

Katika hali hiyo, karatasi ya makubaliano zinaweza kutumika na zinaruhusu klabu kuthibitisha kuwa makubaliano yamefikiwa na kupewa muda wa ziada wa kuwasilisha nyaraka zilizosalia.

Mara baada ya nyaraka kuwasili, klabu zina saa mbili zaidi, au hadi saa 07:00 usiku kutuma karatasi kamili.

Nani anaondoka?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Huenda Ivan Toney ameichezea Brentford mechi yake ya mwisho lakini atakwenda wapi bado haijajulikana.

Mshambulizi huyo amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia Saudi Arabia, dau la pauni milioni 35 kutoka kwa Al-Ahli lilikataliwa na Bees.

Mshambuliaji Raheem Sterling ameambiwa hana mustakabali ndani ya Chelsea, kumaanisha anaweza kuhama kabla ya dirisha kufungwa. Aston Villa na Manchester United zina nia ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.

Jadon Sancho ni mchezaji mwingine ambaye hana mustakbali mzuri United. Mshambulizi huyo, alitumia kipindi cha pili cha msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, baada ya kutofautiana na meneja Erik ten Hag, na hajaichezea United kwenye Ligi hadi sasa.

Paris St-Germain wanataka kumnunua Sancho.

Beki Marc Guehi aliichezea vyema England kwenye Euro 2024 na kiwango chake kwa nchi na klabu yake ya Crystal Palace kimetuvutia macho ya wengi.

Newcastle wamekataliwa mara nne kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, lakini wanaweza kurudi kuzungumza na Palace kwa mara nyingine tena.

Kwanini matumizi yamepungua?

dc

Ikiwa vilabu havitatumia pesa nyingi siku ya Ijumaa, msimu huu wa kiangazi huenda usivunje rekodi ya pauni bilioni 2.3 iliyotumika mwaka jana.

Vilabu vya Ligi Kuu England vilitumia pauni milioni 100 tu katika dirisha la uhamisho la Januari. Pesa hizo zilikuwa chini tangu Januari 2012 vilabu vilipotumia pauni milioni 60 - ukiondoa dirisha la Januari 2021 la pauni milioni 70 wakati wa janga la uviko 19.

Dirisha la majira ya joto limekuwa na manunuzi madogo, wataalamu wanasema sababu ni kanuni za faida na fedha katika ligi hiyo.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Seif Abdalla